Nahitaji msaada wa mawazo kuhusu Baclays Benk!

zovyonzoziginzi

New Member
Nov 7, 2011
2
0
Nilijiunga na benki hii takriban miaka mitatu iliyo pita, na nikachukua mkopo,lakini cha ajabu makato ya hii benki nayaona kama ni ya kijanja kijanja sana, makubaliano yaliyopo ilikuwa mshahara wangu upitie kwao ili wakate pesa yao,lakini mshara ukiingia wanakata pesa yao,na kuzuia kiasi kingine cha pesa kilicho baki mpaka uende kulalamika ndo wanaachia,hali hii imekuwa ikijitokeza mara kwa mara,na nimejitahidi kupata ufumbuzi wa hili wahusika wananikwepa kwepa kwa kuniambia system zipo chini so niondoke kisha watanipigia, then they don't call back! Na nikiwapigia hao wahusika hawapokei simu yangu.Nina tatizo hili yapata wiki Mbili sasa.Naweza pata Mdau yeyote wa Bacrays Bank ambaye atanisaidia kwa hili?cause am stranded and I need the money.
 
kwanza hujaeleweka, unadai hili tatizo la mda sasa na huku unasema una matatizo yapata wiki mbili sasa which means mshahara wako mmoja ndo umekuwa na matatizo nao! kiufupi hayo matatizo yapo na hii nchi lazima ujifunge mkanda mwenyewe kutafuta haki yako!
 
hata mimi yamenikuta exactly kama ilivyonikuta wewe. nilichukua mkopo na imenitokea kama ulivyoelelzea. nilichukia one day walikata deni lao ila walikwapua salary yooteee kwenye akaunti (nikimaanisha badala ya say kukata laki 3, wao walikomba mara 3 yake) halafu cha ajabu statement ikaonyesha eti nadaiwa deni la kama laki 7 hivi!!! duuuuu! nilichoka halafu ilikuwa wikiend!!!!!! sikusaidiwa lolote nilipofuatilia, nilikuwa napigwa chenga tu! sasa hivi nimejitoa huko, mshahara sipeleki huko!! wahuni sana hao jamaa!!!!
 
Ki msingi Bacrays hawataki wateja tena maana jamaa wana huduma mbovu sana,makato yao tu kwa mwezi hayaeleweki ukienda kuchukuwa statement za akaunti yako chenga zake hata Ronaldo hafiki mara network iko chini,nenda chukuwa hii namba tutakupigia baadae utapiga simu yako hawapokei khaaaaaa wanaboa sana atm card yao nilishatupu muda mrefu cha kufanya jaribu head office yao posta!ikishindikana ndo ufanye maamuzi ya kuwa na akaunti kwa benk nyingine!
 
Usumbufu kama huo hata CRDB nao wanao; kwa mfano umechukua mkopo kwao kwa makubaliano kwamba unakatwa kwenye mshahara wako kila mwisho wa mwezi na kizuri zaidi ni kwamba mwajiri wako anakata moja kwa moja mkopo wao na kwa maana hiyo pesa yao haingii kwenye akaunti yao, LAKINI mara tu mshahara wako unapoingia nao wanakata kwa kusema kwamba ni AUTOMATIC DEDUCTION inapofika tarehe ile uliyopewa mkopo nao, haijalishi wameshapokea toka kwa mwajiri wako. Mimi walinisumbua sana na unapofuatilia wanakuambia watarefund lkn sometimes wanapitiliza. Hivyo, nililazimika kukomba pesa zote kwenye akaunti kabla ya ile tarehe niliyochukua mkopo kufika, kwani tayari marejesho yameshafanywa na mwajiri.
WAY FORWARD; nilishauriwa na accountant anayehusika na mishahara kwamba kwa kweli kuna usumbufu mkubwa sana kwenye hizo benki, hivyo option pekee nzuri ni mshahara wako kupitia akaunti nyingine, kwani marejesho yao wanapewa na mwajiri wangu kila mwisho wa mwezi. Jaribu kuangalia huo uwezekano, kwani imenisaidia sana na sasa sipati tena usumbufu wowote kutoka kwao-CRDB.
 
mnalalamika tuu lakini hamjatueleza ni benki gani haina uo usumbufu. Au hamtaki kulipa mkishakopa?
 
hao jamaa wa barclays hata mimi nahis manyota manyota mbeleni koz siwaelewi kabisa ya chenga live mimi walikuja wale sales person wao kwa ofis nikajiunga nikajaza form za mkopo leo yapata mwez wa tatu wakat wale sp walitupromise tukujaza mkopo within one wk unapata mkopo bt hola ukiwapigia simu wanakujibu system tumebadil so now formu tuna scan that y inachelewa kila siku same nyimbo baada ya miez miwil wakanitumia account kuwa hela imeingia kny account hadi leo cjapa hela ukiulza wanadai cheque bado tun
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom