Nahitaji msaada wa kisheria

Jodeo

JF-Expert Member
Mar 10, 2015
1,286
1,328
Salaam wana JF.

Nianze kwa kukushukuru kwa mchango wako. Asante sana!

Kuna watu wanaendesha mradi Fulani Wa wakulima hapa Mwanza. Ni mradi unaodhaminiwa na watu Fulani kutoka US.

Sasa mwishoni mwa February 2016 walinipigia simu nikiwa Dodoma na wakanambia hitaji lao kwamba wanataka MTU Wa kusaidia baadhi ya mambo Fulani ya kitaalamu. Sijui walipata wapi CV yangu lakini nikasema sawa nitaenda tuongee nione kama kuna ulaji mzuri. Nikaenda interview DSM kisha nikaenda na Mwanza ili kuijua kazi yenyewe na makubaliano ya kazi.

Nilipofika Mwanza tukajadiliana, tukaelewana kila kitu. Lakini walikuwa hawajaandaa mkataba wakati huo na kazi yenyewe ilikuwa ni consultation job kwa muda Wa miezi mine(4). Ikabidi nianze kazi wakati wanaendelea na kuandaa written contract.

Baada ya siku kama week mbili nikaambiwa kuna mtu (partner) wanafanya nae kazi. Huyu partner ana makampuni ambayo yanasupply pembejeo kwa wakulima. Hivyo nikaambiwa pia huyo nitakuwa nikishirikiana naye kwa ukaribu na nikapewa option ya kutumia ofisi yoyote kati ya hizo mbili. ( MOJA IKO JENGO LA NSSF NA NYINGINE PPF hapa Mwanza).

Kadiri muda ulivyokuwa ukienda nikawa nakumbushia kuhusu mkataba, lakini jamaa hawataki kutoa mkataba. Hapa juzi nilipoulizia kuhusu mkataba jamaa Wa kwanza akawaka sana akisema kama hutaki kufanya bila mkataba acha kazi nenda nyumbani. Pia kulikuwa na huuni Wa kufoji data zisizo za kweli ili kuandaa ripoti, kitu ambacho niliwakatalia ndo jamaa akamaindi sana akasema " kama huwezi kuandaa data tutapata wapi ripoti njema" kama huwezi kitafuta data(ambazo Si halisi) no job.

Hivyo nikachagua kwenda home kuliko kuficha ukweli Wa kinachoendelea kwa wakulima wetu ukizingatia hawa jamaa wenye mradi ni wahindi na ktk uhalisia hakuna wanachofanya kusaidia wakulima zaidi ya kuwafanya kama kivuli then wanapiga hela. No output at all.

Basi nikaamua kuomba iliyo haki yangu kwa muda wote niliowafanyia kazi. Jamaa wakagoma. Wakawa wanasukumiana Mpira.

Nikaamua kwenda mahakamani, nikaeleza ilivyo kisha nikajaziwa fomu ambayo ilitakiwa mmoja Wa Hao partners ( waajiri) azisaini kisha nirudi na kopy mahakamani. Jamaa alipoziona akagoma kusaini akisema yeye hizo hazimuhusu (lakini yeye ndiye aliyeniita kazini japo sikuomba hiyo kazi na kuna ushahidi kwamba aliniita kazini na kunipa majukumu). Wakati nataka kurudi mahakamani nikaona muda umeisha tayari na Leo ni ijumaa, hivyo mpaka next week.

Sasa je, katika mazingira haya, haki inaweza kupatikana ?

Summary:

Umeitwa kazini, kazi ambayo hukuomba, kisha unaanza kuwajibika kwa sababu ni very urgent huku ukisubiri writte contract. Ktkt ya kazi, aliyekupa kazi anakuzingua kwa kuwa hauko tayari kufuata njia za magumashi. Unakubali kuacha job lakini jamaa hataki kukulipa unachostahili akisingizia partner wake ndiye mwajiri wako.

Kisheria naweza kupata haki yangu? Agreement ilikuwa ni miezi minne tu.

ASANTE.
 
Back
Top Bottom