Sasa kama Hela za kumlipia unazo tatizo linatika wapi?Habari JF ,
Mpwa wangu ni Mtumishi wa serikali , katika harakati zake za maisha ,Amekopa taasisi mbili tofauti za ukopeshaji pesa kwa watumishi.
Dhamana ya mkopo wake ni mshahara ambapo kwa maelezo wanaacha kadi ya benk akaunt ya mshahara.
Kampuni moja inamdai 1,600,000 na nyingine 1,400,000 , Kilichotokea alikopa sehemu ya kwanza akaacha kadi , baadae kadi ikawa expired , akaitwa abadilishe , akatumia nafasi hiyo kwenda kukopa taasisi nyingine.
Sasa ya hii ya kwanza wamemshataki polis na aliwekwa lockup na nilienda kumtoa wiki iliyopita , na kukubaliana alipe hiyo pesa ,
Tumeenda taasisi ya pili hawataki kumlipia hili deni , na mshahara wake ni mdogo hauwez kugawanyw kwenda sehem zote.
Polisi anatusumbua sana , na anatak amkamate amweke ndani ,
Ndugu zangu naomba msaada kwenye hili shauri , Anatokaje huyu mwanangu , ukizingatia hana pesa , tumepambana hakuna kitu , Msaada tafadhali wa kisheria hapa. Ukizingatia ni mtumishi , anatokaje salama?
Kweli mjinga ni wewe (jina lako mwenyewe)! Mdaiwa ikifika wakati anafungwa!mdaiwa hafungwi.huyo polisi anataka hela tu.wana njaa haoo
Shukrani kwa maelezo mazuri , Kwa kuongezea ni kuwa hata mimi nilidhani hivyo , Ila hawa watumishi ukiacha na hizi benk kuna credit loan ambazo huwa wanakopa , Kwa hiyo hizo hazina haja ya kufuata zile taratibu za mikopo kama ya benk ,Mh
Mimi siyo mwanasheria lakini ngoja niongelee upande ninaohisi naujua.
Kama 3M imesababisha jamaa awe hawezi kukatwa tena yawezekana ana mikopo mingine zaidi ya hii miwili na anakuficha.
Taasisi ambazo zinajiheshimu kidogo hua zinafanya KYC kwa mteja mojawapo ni hiyo ya kuona ikiwa mteja anakopesheka na hizi taasisi hua hazina haja ya kubaki na kadi yako ya ATM kwakua zinakua zimeshafanya kiasi husika kiwe kinachepuka na kuingia kwenye akaunti yao.
Deni hua lina dhamana na kwa mtumishi wa serikali hapo ndiyo kitonga zaidi kiasi mdaiwa akifa au akikimbia kulipa deni hii taasisi haina haja ya kumtafuta jamaa ili impeleke jela. Kama hiyo taasisi ilimuamini jamaa dhamana yake iwe kadi ya ATM mbona sasa hivi hawaitaki tena?
Mdaiwa sugu taarifa zake hua zinapelekwa Credit Bureau hii husababisha mdaiwa huyu ashindwe kukopa sehemu zote zinazojiheshimu kidogo. Ndiyo maana ndugu yako imebidi aende kukopa huko ambako imebidi wakae na kadi yake.
Kwa namna anavyodaiwa hapo ndugu yako ni amekopa kwa loan sharks. Mfano wa loan sharks maarufu ni wale Oya ambao wakimfuata mdaiwa na kumkosa ila wakakuta madumu ya maji wanaondoka nayo au wanafunga mahema kumsubiri mhusika.
Mwisho kabisa, hakuna mkopeshaji ambaye target yale siyo kulipwa. Hata ukiweka nyumba kama dhamana wao hua hawalengi nyumba hua wanalenga kulipwa. Mwambie ndugu yako afike kwenye hiyo taasisi na akae nao chini na kutafuta suluhu ya njia mpya ya malipo kwakua ya awali imeshafeli.
Kwa sheria ipi hii hii ya civil law na contract law acha bhasi labda kama kudaiwa huko kumesababishwa na jinaiKweli mjinga ni wewe (jina lako mwenyewe)! Mdaiwa ikifika wakati anafungwa!
Habari JF ,