Nahitaji msaada wa kifedha, nimekwama

Mara Huna Hata Kitanda, Mara Nitaweka Rehani Vitu Vyangu. Una Vitu Gani Sasa? Naona Wewe Ni Msanii Tu. Pia Nakushauri Nenda Pride Au Finca, Wao Wana Mikopo Ya Vikundi, Na Dhamana Yake Weka Hivyo Vitu Vyako Vya Ndani
mkuu ndio maana nikasema nitaweka rehani vitu vyangu ila ntakaa navyo kwa maana ya kwamba ndivyo ninavyovitumia katika biashara hii ya juice! vitu nilivyomaanisha ni freezer,brender,juice dispenser na hata baiskeli niliyotengeneza! nafikir umenielewa mkuu!!!
kuhusu pride na finca nilishaenda huko ila wanataka uwe na leseni,uzoefu mda mrefu na kazi uwe ushaanza inaendelea pia wanataka dhamana!
kuhusu vikundi ni kuanzia watu watano,ila kupata watu wenye mawazo,uchungu na wasio ogopa mikopo kama mimi imekuwa ngumu kwa sababu inatakiwa wote muwe mnakaa sehemu moja kama mtaa na biashara ziwe karibu!! ila mkopo ninaohitaji mimi ni wa haraka mkuu ingekuwa ni baada ya miezi kadhaa ningelijua nifanye nini
 
Nitafutie BANK inayo nunua MADENI ukiipata Niambie nikauze MADENI yangu then nitakukopesha.
 
. .samahani kama nitakua nakosea mimi niko moro kama kuna uwezekano niunganishe . mana me natafuta kaz yoyote ambayo nitaingiza hata kipato kidogo kwa siku
 
HAUNA HELA,ALAF UNA SIMU YA KUINGIA JAMII FORUM,ALAF UNAJIITA HAMIS,MBONA UNATUDHALILISHA WAJINA,TAFUTA KAZI,KUOMBA NI KUJIDHARIRISHA MDOGO WANGU,
 
HAUNA HELA,ALAF UNA SIMU YA KUINGIA JAMII FORUM,ALAF UNAJIITA HAMIS,MBONA UNATUDHALILISHA WAJINA,TAFUTA KAZI,KUOMBA NI KUJIDHARIRISHA MDOGO WANGU,
samahani kama nakuzalilisha mkuu ila natamani kama ungeliweza kujua hali iliyopo!!
mkuu usifikir labda sijawaza kitu kama hicho! nishawaza sana tu hata nishawaza kuuza hivi vifaa nilivyonavyo ili nipate cash! ila at the end ni kwamba nikishauza baadae nikiingia ndani nitavihitaji tena make ni vitu vya lazima kuwa navyo ili ufanye kazi!
simu hata nikiuza haitamaliza tatizo maana ni ya hela ndogo sana tu! hata hivo kuna shughuli natakiwa nije nianze kuifanya ambapo simu tena smartphone niblazima niwe nayo sababu ya camera, nishawaza kuuza vitu vingi ila naona ntakuwa najidanganya mwenyewe!
kufanya kazi sijashindwa mkuu, hata hivo mpaka kujipanga kupata hivi vifaa nayo ni kazi pia! na ndo maana nikasema kuwa kama hii hela ingekuwa inahitajika baada ya miezi kadhaa ningetafuta taratibu bila kuomba ila kwa sababu ni hitaji la haraka ndo maana nikaomba na tena nimeomba kukopeshwa!!!!!
mkuu mi sio mjinga kuja kuomba hapa! ni mitihani inakuwa mingi tu
 
Refa kauzu, uwanja wenyewe mkavu. Kilichobaki kucheza rafu!

Harakati za mtu mweusi zina changamoto nyingi sana kwakweli. Wengi wetu vijana tupo on the same shoes. Mwenyezi Mungu akufanyie wepesi inshaalah.

Bongo nyosso, Bongo balaa. Kaza jombaa.

-Kaveli-
 
powa wajina usiwaze sana,ndo ukubwa huo,si unajua wanaume tumeumbwa matesooo matesooo kuhangaikaaa,
 
nashukuru kijana mwenzangu,mambo magumu
 
Miss natafuta kaisha ufunga huu uzi labda mleta mada aje afungue uzi mwingine wa mrejesho hongera miss natafuta kwa mguso uliouonyesha.
mkuu nashukuru kwa wazo lako japo bado sijaonana na Miss Natafuta ,pia kanambia kuna kazi ila bado nitakuwa sijatatua tatizo lote kama hela ya kumalizia mradi wangu na kodi tu!!! ambavyo vyote vinahitaji laki sita (600,000), hii ni hela ambayo inahitajika haraka sana maana mda unakaribia kuisha!!! ila dada Miss natafuta kasema kunitafutia sehemu ya kibarua cha kulipia kwa siku angalau siku zisogee nipate ya matumizi ya mambo ya kawaida!!! nafikiri umenielewa Mkuu!!
kwa hiyo bado nahitaji mtu atakayeweza kunikopesha hiyo laki sita ili nitatue hili tatizo la haraka sana!!
 
Ni kweli ndugu yangu lakini kuna wakati sio kila jambo tunalo lipanga huja hivyo hapana ndio maana kuna neno kuakhirisha jambo au wahenga hunena maji yakizidi unga ugali haupikiki una koroga uji siku inapita.
Laki sita sio maji mafupi kwa usawa huu tulionao sisemei wengine ila kuipata kwa haraka haraka ni mtihani mkubwa endelea kupigana ila kwa maoni yangu ungejaribu kujikita kwenye mipango mingine kwanza hilo la project yako ungeliweka pending kwanza.
 
With all the due respect nathubutu kusema wewe ni Muongo! Na pia haupaswi kuaminiwa....nimepitia moja ya thread zako uliyowahi kuileta hapa....na humo ulituambia kwamba haukufanikiwa kumaliza chuo,uliishia mwaka wa pili kwa sababu ulizozitaja wewe! Lakini leo unaleta story kwamba chuo ulimaliza lakini bado haujapata Cheti.! Kwa Uongo huo tu nimejiridhisha kuwa haupaswi Kupewa dhamana! Naamini unajua vizuri naongelea nini
 
Huyu Kijana anaitaji Msaada. BAK nakukabidhi kwa huyu Kijana mkopeshee au MPE iyo hela anayouraji.Mungu atakulipa..Please tusipende kuwa Negative kwa kila jambo..Kuna Watu wanapitia Shida ninyi Acheni.Na Maisha ya Dar Hope mlioanzia Dar mnajua Ni Shida. Wizaea ya Vijana Kuna fungu la kuwawezesha vijana ila kupataaa. Nu URASIMU sana.All the best Young brother
 

Unge MPM kumwambia Haya nafikiri ingekuwa vyema! Umekuwa negative na pengine angekuwa mtu mwingine hapa wa kumsaidia lakini Kwa ujumbe wako huu akakata tamaa.
 
Mleta mada inafika wakati unakubali matokeo tu. Ridhika na utakachopata iyo elfu 15 kwa siku kwa kubeba zege siyo mbaya. Ukitaka vitu vikubwa chini ya uwezo wako utazidi kukwama. Maisha ya ujanjaujanja hayasaidii kabisa.

Laki sita siyo mchezo kwa wabongo sasa hivi na ukata wa Magu. Hakuna atakayekukopesha. Halaf ni hulka yangu kutomuamini mtu anayeomba msaada kwa kujielezaa saaanaa.


USHAURI

Fanya kazi Bro kazi haimuui mtu na Ridhika na utakachopata hata kama kidogo utaish kwa aman.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…