Nahitaji msaada jamani nakufa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nahitaji msaada jamani nakufa

Discussion in 'JF Doctor' started by OME123, Mar 21, 2012.

 1. OME123

  OME123 JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,434
  Likes Received: 191
  Trophy Points: 160
  sasa yapata wiki mbili sasa kuna vijipele vimenitoka karibu na sehemu za mapumbu,nimeenda hospitali nimepima hawajakuta tatizo lolote,wameeniambia kuwa inawezekana sababu naavaa nguo nyingi sana ndani,nimepunguza kuvaa nguo nyingi nimetumia dawa ya kupakaa sehemu iliyooadhirika na nyingine nimeambiwa kunya lakini kidonda hakijapona wala nini,naombeeni msaada jamani nduguzanguni
   
 2. vicent tibaijuka

  vicent tibaijuka JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  unavaa nguo nyingi za nini na joto hilo? Jasho jingi ni chanzo cha kusababisha magonjwa ya ngozi hasa katika nchi zetu hizi za joto. kama hubadilishi chupi kila siku na kuvaa nyingine safi yawezekana una fungus, ni skin irritations tu. cha muhimu ni kubadilisha chupi kila siku na kujiweka msafi. pia jaribu tumia medicated soap *detto* na anti fungal (dawa za fungus (nystatin), pia waweza kuwa unaweka powder kama unatokwa na jasho jingi!
   
 3. Kibukuasili

  Kibukuasili JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2012
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 858
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kama ushapunguza nguo subiri kidogo uone matokeo, si umesema wiki mbili tu?
  Vile vile badili nguo za ndani mara kwa mara na uoge kwa uchache mara mbili kwa siku. Pia punguza nguo wakati wa kulala. Usilale kama unatarajia kukurupushwa usiku
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  kama ulisha wahi kwenda hospitali na hujapona basi tumia dawa yangu hii. Uchukue kitunguu thomu Garlic ukitwange mpaka kiwe laini kisha achukuwe maji ya moto uoshe sehemu zenye vipele ufanye kama unasugua tumia asubuhi na usiku kwa muda wa wiki moja kwa uwezo wa Allah utapona.

  Au kama utapata Asali safi ya nyuki jipake katika hizo Sehemu zenye vipele inshallah kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu utapona pole sana Mkuu. Tumia hizo dawa kwa muda wa wiki moja kisha unipe feed back.
   
 5. vicent tibaijuka

  vicent tibaijuka JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  Au kama utapata Asali safi ya nyuki jipake katika hizo Sehemu zenye vipele inshallah kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu utapona pole sana Mkuu. Tumia hizo dawa kwa muda wa wiki moja kisha unipe feed back.
  [/QUOTE]
  Asali ni mwanzo wa kukuza fungus. kwani sukari ni sehemu mojawapo ya kukuza fungus
   
 6. k

  kamili JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 714
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60

  [FONT=&quot]Mkuu umenichanganya kidogo, mwanzo umesema kuna vipele vimetoka karibu na mapumbu, lakini mstari wa mwisho unasema kidonda hakijapona!!! Kiutalaamu ipo tofauti kubwa ya kidonda na vipele. Kwa sababu visababishi ya vipele yaweza kuwa tofauti na visababishi ya kidonda, pia vitu hivi viwili vyaweza kutofautiana sana hata kwenye tiba. Halafu umesema umepima hawajaona kitu, hiyo nayo imenichanganya kwa sababu hata hivyo vipele au kidonda ina maana wataalamu hawajaviona. Au umepima nini mwenzetu? Kama bado unahitaji msaada wa mawazo naomba nifafanulie hayo. Na pia kama hutajali waweza chukua picha ya hivyo vipelea au kidonda ukani PM. Pole sana.


  [/FONT]
   
Loading...