Nahitaji mpimaji wa Ardhi

Marealle

Member
Nov 2, 2010
8
10
Kwanza natoa pole kwa mihangaiko ya siku nzima ya leo.

Nina tatizo na mpima ardhi hawa wanaofanya zoezi za urasimishaji, wiki tatu zilizopita Nilikupigia kupima Kiwanja changu ambachonilinunua vile vya kupima kienyeji vinne kwa kimoja, yaani viwanja vinne kuwa kimoja.

Wakati wa kupima mpimaji alikuja wakati sipo, akagawa Kiwanja changu nusu na kuniambia eneo lililobaki ni eneo la barabara, kiuhalisia eneo aliloacha si labarabara na kama ni barabara si kwa ukubwa huo Kwani viwanja vya ndani kabisa huku chanika haviwezi kuchukuwa ukubwa huo.

Je, nitumie njia gani kurekebisha kasboek hii maana naona ni mtu ambaye ananikwepa na hataki kuonana na mimi?

Je, ninaweza kutafuta mtu mwingine wa kupima na anakanipimia upya?

Nitashukuru kama nitapata msaada wa kutatua changamoto hii na nipo tayari kuanza upimaji upya kama nitapata mtaalam wa kupima.
 
Back
Top Bottom