Nahitaji mkopo wa dharura

Loveeness78

JF-Expert Member
Oct 9, 2016
280
294
Salaam kwenu wana JF, hususani jukwaa la biashara, chumi na ujasiriamali.

Mwenzenu nimetingwa na nimekwama kidogo kwenye biashara yangu. Naombeni kujua ni sehemu gani nawezakupata mkopo wa dharura (ndani ya masaa 24 au 48) kwa riba nafuu. Mkopo ninaohitaji ni laki7 na nitarejesha ndani ya mwezi mmoja. Bank kuna mkolongo sana, na kwenye hizi microfinance nako kuna process zinazochukua wiki mpaka wiki mbili.

Dhamana au rehani ninazoweza kuweka ni kama zifuatavyo:
1. Biashara yangu ni ya vileo (pub) ipo bunju. Ina kila kitu kuanzia leseni, vibali vyote, vitendea kazi kama tv 42", music system, fridge na freezer, viti, meza, n.k. Ina fanya kazi
2. Biashara ya pili ipo under construction na ndo nimekwama hapo kukamilisha ianze hata keshokutwa.
3. Nina laptop mbili(moja inatumika hapo pub kupiga music, nyingine naitumia kwa kazi binafsi.

NB: Biashara zangu zote nimekodi eneo kwa mkataba mrefu nikajenga na bado nipo ndani ya mkataba(mikataba ipo unaweza kuona na kujikahikishia hata kwa mwenye eneo ukitaka)
Nina record nzuri ya pesa bank. Nimekubwa na tatizo kubwa la ghafka ambapo mfanyakazi aliniibia kiwango kikubwa cha pesa wakati nipo site, ikapelekea kuyumba na hivyo nahitaji emergency backup nisikwame kwani nimetumia akiba yote niliyokuwa nayo.

Kwa ambae anawezakunisaidia au kunielekeza ninapoweza kusaidiwa kwa leo nitashukuru sana. Anipe vigezo na masharti pamoja na riba.

Ili kuepusha kudhaniwa kukopeshwa na zaidi ya mtu mmoja, endapo ikitokea, basi nitaomba niwekewazi aliyenikopesha ili isitokee mwingine akasema nae kanikopesha. Naishi bunju, na biashara zangu ni hapahapa Bunju.
Ahsanteni
 
Mkuu si ufunguje hapa ili nasisi wengine mbeleni tukihitaji CHAP CASH tujue tunaelekea wapi? Maana inaboa mtu kumkopa msela wako mpaka uanze kujielezea. Bora hii mikopo ya chap chap mtu unaweka rehani kitu unaenda kutatua shida yako.
 
Mkuu si ufunguje hapa ili nasisi wengine mbeleni tukihitaji CHAP CASH tujue tunaelekea wapi? Maana inaboa mtu kumkopa msela wako mpaka uanze kujielezea. Bora hii mikopo ya chap chap mtu unaweka rehani kitu unaenda kutatua shida yako

Sent from my TECNO LC6a using JamiiForums mobile app
Ni binafsi mkuu sio taasisi sasa mambo ya binafsi ni makubaliano mkuu
 
Hakika mdada umejieleza vizuri sana, NO DOUBT UTASAIDIKA SOON, Bunju ni mbele la oko? Huwa nafika Kibo complex frequently.
 
Back
Top Bottom