Nahitaji maombi!!!!!!!!

Nahitaji maombi!!!!!!!!

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2009
Posts
6,157
Reaction score
4,454
Jamani kwa watu wa imani zote naombeni msaada wa maombi yenu. Miaka ya hivi karibuni kuna roho ya chuki mbaya imeibuka moyoni mwangu dhidi ya binaadamu mwenzangu.
Kabla ya Mkapa na kikwete kuingia madarakani nilikuwa na tabia ya kupenda kufuatilia hotuba za Rais Ali Hasan Mwinyi kila anapohutubia taifa na wakati mwingine nilikuwa nasitisha shughuli zangu ili nimsikilize rais, baada ya kumaliza mda wake akaingia Mkapa, huyu mtu alijiwekea utaratibu wa kulihutubia taifa kila mwisho wa mwezi ni katika kipindi hiki iliibuka shauku kubwa zaidi ya kufuatilia hotuba za viongozi wa nchi kiasi kwamba hata mimi nililazimika kuweka katika ratiba zangu ilimradi tuu nisiikose hotuba ya rais hata moja, siyo kila alichohutubia Mkapa nilikipenda lakini nilikuwa nafurahishwa sana na namna alivyokuwa anapangilia vizuri hotuba zake na kuzi-address hoja kisomi.
Alipoingia Kikwete madarakani niliendelea kufuatilia kwa karibu hotuba zake za kila mwezi, tofauti na miaka ya nyuma taratibu nikawa sivutiwi kuendelea kusikiliza mpaka hotuba yake iishe, baadaye nikawa simsikilizi hata kama nipo karibu na TV au redio, hii hali iliendelea kwa mda kidogo, mbaya zaidi katika kipindi hiki cha kuanzia 2011 tatizo limekuwa kubwa zaidi kila nimsikiapo rais aidha nitazima Tv au nitalazimika kubadiri stesheni, na mahala nisipo na mamlaka ya kufanya hivyo nimekuwa nalazimika kuondoka eneo hilo. Hili tatizo linazidi kuwa baya zaidi kwasasa hata nikimsikia mtu anazungumzia habari zake huwa nakasirika, najua tatizo kubwa laweza kuwa ni uwongo wake alio ufanya katika kampeni akiwa anawania kuingia madarakani kwa mara ya kwanza, pale aliponidanganya “maisha bora kwa kila mtanzania” nikajikuta nampatia kura yangu bila kujua kwamba huyu mtu ni wa mzahamzaha”. Naombeni msaada wa maombi roho yangu ijirudi kidogo kwa huyu mtu
 
:happy:

God will honor your request....he bestows to the humble and fill them with His delights......
 
ndugu yangu pole sana, jitaidi kukwepa kusikiliza hotuba zake na mabo yote yanayomwusu ikiwa haitakusidia msikilize lakini mchukulie kama kiongozi wa kawaida sana ambaye ufanya mambo kwa mazoea so chochote atachoongelea do not take it seriously na sio wewe tu mwenye hilo tatizo wapo wengi ambao wamemchoka wanaomba ata hiyo miaka minne iliyobaki ihishe kesho, uchaguzi mkuu mpya uje!!!!
 
Unahitaji kubadilika,
1. Badili "SIMTAMBUI JK KAMA NI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA" kuwa "Namtambua JK KAMA NI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA"

2. Huwezi kubadili moyo wako, ila unaweza kubadili nia (mind) yako. Mungu hawezi kubadili nia yako ila ukiibadili ataugeuza moyo wako umpende Mungu na JK

3. utakuwa mwanakondoo
 
Pole sana mkuu
usiangalie wakati anahutubia kila mwezi
usisome magazeti yenye taarifa zake
kama ............me

Unahitaji kubadilika,
1. Badili "SIMTAMBUI JK KAMA NI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA" kuwa "Namtambua JK KAMA NI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA"

2. Huwezi kubadili moyo wako, ila unaweza kubadili nia (mind) yako. Mungu hawezi kubadili nia yako ila ukiibadili ataugeuza moyo wako umpende Mungu na JK

3. utakuwa mwanakondoo

Ni wazo zuri sana, ngoja nisifanye haraka kwanza, nalifanyia kazi
 
Jamani kwa watu wa imani zote naombeni msaada wa maombi yenu. Miaka ya hivi karibuni kuna roho ya chuki mbaya imeibuka moyoni mwangu dhidi ya binaadamu mwenzangu.
Kabla ya Mkapa na kikwete kuingia madarakani nilikuwa na tabia ya kupenda kufuatilia hotuba za Rais Ali Hasan Mwinyi kila anapohutubia taifa na wakati mwingine nilikuwa nasitisha shughuli zangu ili nimsikilize rais, baada ya kumaliza mda wake akaingia Mkapa, huyu mtu alijiwekea utaratibu wa kulihutubia taifa kila mwisho wa mwezi ni katika kipindi hiki iliibuka shauku kubwa zaidi ya kufuatilia hotuba za viongozi wa nchi kiasi kwamba hata mimi nililazimika kuweka katika ratiba zangu ilimradi tuu nisiikose hotuba ya rais hata moja, siyo kila alichohutubia Mkapa nilikipenda lakini nilikuwa nafurahishwa sana na namna alivyokuwa anapangilia vizuri hotuba zake na kuzi-address hoja kisomi.
Alipoingia Kikwete madarakani niliendelea kufuatilia kwa karibu hotuba zake za kila mwezi, tofauti na miaka ya nyuma taratibu nikawa sivutiwi kuendelea kusikiliza mpaka hotuba yake iishe, baadaye nikawa simsikilizi hata kama nipo karibu na TV au redio, hii hali iliendelea kwa mda kidogo, mbaya zaidi katika kipindi hiki cha kuanzia 2011 tatizo limekuwa kubwa zaidi kila nimsikiapo rais aidha nitazima Tv au nitalazimika kubadiri stesheni, na mahala nisipo na mamlaka ya kufanya hivyo nimekuwa nalazimika kuondoka eneo hilo. Hili tatizo linazidi kuwa baya zaidi kwasasa hata nikimsikia mtu anazungumzia habari zake huwa nakasirika, najua tatizo kubwa laweza kuwa ni uwongo wake alio ufanya katika kampeni akiwa anawania kuingia madarakani kwa mara ya kwanza, pale aliponidanganya "maisha bora kwa kila mtanzania" nikajikuta nampatia kura yangu bila kujua kwamba huyu mtu ni wa mzahamzaha". Naombeni msaada wa maombi roho yangu ijirudi kidogo kwa huyu mtu

Ishindwe na ilegee hiyo roho maana nimegundua inaambukiza kwa njia ya Hewa. Cha kunisikitisha zaidi ni kuwa sijui lini na wapi lakini ushaniambukiza zamani tatizo lako. Tena kwangu ni baya zaidi. AGHRRRRR...
 
nadhani unisamehe kwani ntakuwa ni mimi nimekuambukiza! Mimi nilikuwa na hasira tangu alipopitishwa 2005. nilijitahidi kuwaeleza nilioweza kuwa hapa tumekula wa chuya. hamna kitu hapa. sikusikilizwa na nilipuuzwa kwa sababu ya propaganda zake alizokuwa kajipanga nazo. lkn i could see kwenye macho yake kuwa hakukuwa na heri yoyote mbele kwa nchi hii. hata walipokuwa wakisema ni chaguo la mungu nilishika kichwa. kwamba hivi watu wote hawa hawawezi kuuona ukweli, mbona unaonekana kwenye macho yake kwa wazi kabisa.

sikuwahi na sijawahi kumpa kura yangu. nashukuru 2010 wengi walikuwa wamegundua ukweli ambao nilishauona enzi na enzi. na kweli legitimately sio rais halali wa nchi hii, ingawa constitutionally he is (pity...!)
 
Mambo mengine falsafa yako nimeeipata mkuu,Kwa kifiupi ni kuwa blabla zimekuwa nyigi sana kinachoongelewa si ndicho kinaccchotendwa pole sana ndiyo yaliyofanywa na wananchi na kuchakachua .
 
Ishindwe na ilegee hiyo roho maana nimegundua inaambukiza kwa njia ya Hewa. Cha kunisikitisha zaidi ni kuwa sijui lini na wapi lakini ushaniambukiza zamani tatizo lako. Tena kwangu ni baya zaidi. AGHRRRRR...

Pole sana ndugu, hili tatizo lipo kwa Watanzania wengi lakini mimi ninahitaji maombi ya haraka, haiwezekani kumchukia binadamu mwenzangu kiasi hiki kwani yeye alipenda awe muongo? si ni maumbile tuu
 
nadhani unisamehe kwani ntakuwa ni mimi nimekuambukiza! Mimi nilikuwa na hasira tangu alipopitishwa 2005. nilijitahidi kuwaeleza nilioweza kuwa hapa tumekula wa chuya. hamna kitu hapa. sikusikilizwa na nilipuuzwa kwa sababu ya propaganda zake alizokuwa kajipanga nazo. lkn i could see kwenye macho yake kuwa hakukuwa na heri yoyote mbele kwa nchi hii. hata walipokuwa wakisema ni chaguo la mungu nilishika kichwa. kwamba hivi watu wote hawa hawawezi kuuona ukweli, mbona unaonekana kwenye macho yake kwa wazi kabisa.

sikuwahi na sijawahi kumpa kura yangu. nashukuru 2010 wengi walikuwa wamegundua ukweli ambao nilishauona enzi na enzi. na kweli legitimately sio rais halali wa nchi hii, ingawa constitutionally he is (pity...!)

At least sasa nahisi ugonjwa wangu ni common, hivyo matibabu yaweza patikana. duu nilianza kuchanganyikiwa
 
Pole sana mkuu. Ulisoma seminary? Unaimba kwaya kanisani?
Huo ugonjwa ulianza kuambukiza mwaka jana mara baada ya Padri Slaa kutangaza kugombea urais!
Ila ni wa msimu utaisha taratibu!
 
Pole sana mkuu. Ulisoma seminary? Unaimba kwaya kanisani?
Huo ugonjwa ulianza kuambukiza mwaka jana mara baada ya Padri Slaa kutangaza kugombea urais!
Ila ni wa msimu utaisha taratibu!

Ahsante ndugu yangu, binafsi nilikuwa sifahamu kama " Padri Slaa kutangaza kugombea urais!" ingeweza kuniletea matatizo kiasi hiki maana akiwa alhaji Ali hasan mwinyi madarakani sikuwa na matatizo naye na nilikuwa namsikiliza vizuri tuu kama rais wa nchi, iweje ustaadhi Kikwete nimchukie?, nadhani hii ni serious case kuna haja ya kujikita zaidi katika maombi.
 
Nimeifuatilia vizuri thread ya mtoa mada nimejizuia kuchangia haraka maana inahitaji uwezo mkubwa kuitafakari kabla hujachangia lolote, kwanza imekaa kama utani. Naomba nisichangie lolote
 
WAKUU!
kama ni maombi basi mimi nahitaji maombi zaidi yako mkuu!
mpaka wanaovaa tshet za pic ya jk namchukia!
NAMCHUKIA YEYOTE ANAYEMFAGILIA HUYU JAMAA!
NIOMBEENI PIA NDUGU ZANGU!
 
Back
Top Bottom