Wewe bado kijana mdogo sana kufikiria mambo ya mapenzi sasa,ukizingatia ni mwanaume unakimbilia nini? Utayakuta hayo muda ukifika. Labla nisiusemee moyo pengine una lengo zuri tu lakuoa mapema sana baada tu ya masomo,na unaona huu ni wakati muafaka wa kutafuta mwezi wa maisha, kama ndivyo vyema coz ni afadhali kuoa kuliko kuanza uasherati. Lakini kama sivyo na lengo ni kutafuta mtu wa kufanya nae mapenzi, mdogo wangu sikushauri,soma kwa bidii sana achana na vishawishi hivyo kwa sasa havitakusaidia, after all baada ya kumaliza masomo nakushauri ujikaze usioe mapema sana,jipange vizuri kimaisha kwanza coz ndoa inakwenda kukuongezea majukumu makubwa zaidi( usifikiri ni kwenda kupata ile raha tu vijana wengi wanayoifikiria).