Nahitaji kujiendeleza kielimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nahitaji kujiendeleza kielimu

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Kitabu, Jan 12, 2012.

 1. Kitabu

  Kitabu JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 257
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wakuu elimu yangu ni kidato cha nne,division (iii)ninania ya kusomea IT,kwa njia ya mtandao(on line)kutokana na nafasi yangu kuwa ndogo kuhudhuria darasani,je nichuo gani ninaweza kujiunga nacho ambacho kinatambulika na serikali.Nadhani ni vema nianze na diploma...!!!
   
 2. kingadvisor

  kingadvisor Senior Member

  #2
  Jan 12, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anyway sijui kwa nini ulipata division III wakati unataka kuchukua sayansi.Hujasema uko wapi lakini MASOMO YA online waajiri wengi hawatambui sifa hiyo hata upate PHD.Kuna vyuo vya masomo ya jioni kwa nini usisome huko hiyo kazi ambayo huna muda kabisa ni ipi hiyo? Kama uko Dar es salaam the best place kusoma jioni ni UNIVERCITY OF DAR ES SALAAM COMPUTING CENTRE (UCC) wana tawi chuo kikuu pale,POSTA mpya na maeneo mengine.Ila sasa ukienda usome kwa bidii IT ni fani inayobadilika mara kwa mara kutokana na maendeleo yake kwenda kasi sana kwa hiyo ukiingia huko uwe tayari kujiendeleza kusoma mara kwa mara.Yale uliyosoma mwaka huu usishangae mwakani ukienda na cheti chako kwa mwajiri mwingine akakwambia ujuacho ni outdated.Lakini kama lengo lako ni kusoma tu upate chetii/DIPLOMA usiendelee kusoma tena nakushauri tafuta fani ingine siyo IT.
   
 3. Kitabu

  Kitabu JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 257
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  asante KING,nitatafakari.Ajira tayari ninayo,ninania ya kujiendeleza,kwa kuwa ulimwengu huu naupenda
   
 4. C Programming

  C Programming JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 1,755
  Trophy Points: 280
  mimi nakushauri tafuta fani nyingine kozi ya IT ajira zake ni ngumu sana mi nakushauri ni heri uende muhimbili ukasome phamarcy au medical laboratory ......diploma zao zipo flesh sana
  tatizo IT inabadilika kila siku na soko lake la ajira ni gumu sana maana sasa hivi wanafunzi wa it wamejaaaa sana........na wengi wana burn nyimbo mitaabi
   
 5. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ukitaka cheti nenda UCC, ukitaka kujua nenda kwenye hivi vyuo vya WAHINDI (Learn IT, New Horizon, CATS n.k). Suala la vyeti kutambulika ni ufukunyuku wa serikali yetu na ndio maana hatuendelei. Haya matatizo unayoyaona tiGO mtandao mara uko hivi mara vile ni matunda ya vyeti.

  Huyo anayekwambia hbr za wewe kuwa na Div III hilo halimo. Division 5 ndio haina mashiko na kamwe usikatishwe tamaa na stupid academic rubbish. Go vocational dear boy na ukitaka kujua kuwa hao wanaojifanya wana high marks si kitu, angalia jinsi walivyoajiriwa kwa wingi na Bakhressa ambaye sidhani kama yeye ndio msomi saaaaaana. Go for skills, sio vyeti.
   
 6. Kitabu

  Kitabu JF-Expert Member

  #6
  Jan 15, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 257
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  nashuru sana mkuu kwa ushauri wako,nimeufurahia sana,ubarikiwe
   
Loading...