Nahitaji kuacha kunywa pombe

Mkuu hongera kwa kuacha, watu wengi wanateseka
 
Swala linaanzia apo kwenye kiasi, nina ndugu yangu zamani alikuwa anakunywa jumapili pekee, saivi amekuwa chakari anakunywa mda wote mapombe machafu
 
Ukiamua kwa dhati unaacha, mimi ni shuhuda kupitia mimi mwenyewe. Nimekunywa sana kwa zaidi ya miaka 20 na sasa najisikia huru huu naenda mwezi wa 4, au hesabu nzuri ya muda nilioacha hesabu tangu siku ya mechi ya AFCON kati ya Egypt na Senegal waliofikia mikwaju ya penati ndio siku niliyokunywa kwa mara ya mwisho. Najichanganya nao rafiki zangu ambao wanakunywa na hata raundi nawaagizia lakini hata mzuka wa kutamani sina kabisa, hawaamini macho yao. Kwa kweli najisikia niko huru sana na hata baadhi ya mambo ya kazi nayazingatia kwa wakati, imani kwa wadau imeongezeka sio kama nilivyokuwa nakunywa, kwa ujumla nimegundua kuwa "pombe zilinichelewesha sana.." (in Magu's voice - RIP).
 
Punguza kunywa pombe ndugu uwe unakunywa asteaste usiache kabisa. Pombe inaongeza akili.
 
Asante sana kwa kunipa uzoefu, naamini ntaweza. Jana nimemeza piriton nmelala vizuri
 
Asante sana kwa kunipa uzoefu, naamini ntaweza. Jana nimemeza piriton nmelala vizuri
Piga chini kampani zote za tungi...
Oa..
Kama unakaa nyumba ya walevi hamaa...
Fikiri malengo mapya, kama huna nyumba anza ujenzi...kama huna watoto zaa...
Usikae na hela ambayo haina kazi...
Anza dose ya kutoa sumu ya pombe mwilini...
 
๐Ÿ˜‚
 
Umemaliza.

Bravo.
 
Ni uamuzi mzuri . ... Usiendelee kung'ang'ania kitu kisicho na manufaa kwako. Pombe japo nzuri , ikitumiwa vibaya huleta madhara yasiyoweza kurekebishwa . Chukua hatua !!! Ni kuacha... Huhitaji ushauri... Acha !!!

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Piga chini kampani zote za tungi...
Oa..
Kama unakaa nyumba ya walevi hamaa...
Fikiri malengo mapya, kama huna nyumba anza ujenzi...kama huna watoto zaa...
Usikae na hela ambayo haina kazi...
Anza dose ya kutoa sumu ya pombe mwilini...
Hii dozi ikoje mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ