nahitaji kua na galfriend ila nashindwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

nahitaji kua na galfriend ila nashindwa

Discussion in 'JF Doctor' started by komredi ngosha, Aug 6, 2011.

 1. k

  komredi ngosha JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 381
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  salaam jf
  Leo nimeamua na mimi kupost hapa kuhusu tatizo la kukosa mwenza mpenzi kwa muda mrefu. Well, nina miaka 26 sasa, niko chuo kikuu mwaka wa 3 nasoma computer engineering. Katika maisha yangu sijawahi kua na galfrnd, nimejaribu mara kadhaa kua nae kila binti ninaemtaka aidha anakua na mtu au havutiwi na mimi na hivyo jibu la hapana nishalizoea. Wanataka tu urafiki wa kawaida, hakuna ambaye anakua yuko tayari kua na mimi. Jambo hilo linaninyima raha sana, nimeanza kuogopa kutongoza na kuna wakati nikiwaona au kusikia watu fulani ni wapenzi nakosa furaha na kujiuliza sana why not me?! Naombeni ushauri wenu.
   
 2. GABOO

  GABOO Senior Member

  #2
  Aug 6, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  usikose furaha bro,wala usikate tamaa,iko day switi wako utampata,it's just a matter of time.
   
 3. k

  komredi ngosha JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 381
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  <br />
  <br />
  thanks!
   
 4. M

  Mwinga Member

  #4
  Aug 6, 2011
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pole sana kaka, ni hata kama ningekuwa mimi nisingejisikia vizur kwa kutopata girlfriend, wala usikate tamaa kuwa na subira utampata.
   
 5. MKUNGA

  MKUNGA JF-Expert Member

  #5
  Aug 6, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 443
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tulia dogo upate mchumba uoe utakufa bila kufaidi shule yako, wadem wengi wameungua siku hizi. Sali sana mwombe mungu atakupatia mke swaafi kabisa.
   
 6. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,131
  Likes Received: 3,320
  Trophy Points: 280
  Watoto wakike mbona wako wengi.kula kitabu then ukishakamata $$ mwenyewe mbona utakimbia.
   
 7. Aggrey86

  Aggrey86 JF-Expert Member

  #7
  Aug 6, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 856
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wala usiogope kaka ni mda2 ipo dei utampata ila pia Mwombe Mungu umpate aliyemwaminifu na mwenye malengo na ww naamini utampata2 wala usiumie kaka
   
 8. Arvin sloane

  Arvin sloane JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 963
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  pole sana kaka usikate tamaa endelea kutafuta utapata tuu galfriend coz wapo w wengi saana unakuta mwanaume mmoja ana wanawake watano iweje ww ukose hata mmoja kwa hyo uckate tamaa utafanikiwa tuu.
   
 9. Gobret

  Gobret JF-Expert Member

  #9
  Aug 6, 2011
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nikiangalia umri wako; naona kuwa hunahaja ya kuwa na wasiwasi wa hayo unayoyafikiria. Bado ni mapema sana. Jihakikishie maisha yako vizuri. Pata kazi na hapo unaweza kufikiria suala la kuoa siyo kuwa na girlfriend. Rafiki wa kike wa kazi gani au unataka wengine wakuone kuwa na wewe si haba. Hilo ukilitekeleza linaweza kukusumbua mambo yakikuchengia maana kuna wazoefu wa kuwa na ma-girlfriend.

  Ukiwa na kazi nzuri watajileta wenyewe tu na wewe sasandio uchague. Weka mbele zaidi sala na umwombe Mungu sana akupe mke unayeendana naye si ilimradi mke. Wanawake wengi wanaangalia usalama wa maisha yao ya sasa na ya baadaye; sasa pengine kutoka kwako kwa jinsi ulivyojiwekea misimamo yako wanaona kuwa hutawakidhi haja zao. Kumbuka wanawake wana vigezo vyao vya kuchagua lkn kubwa zaidi ni usalama wa maisha yao pia kama unaintertain mambo fulani fulani kama tutoke zetu- twenzetu bichi----gharama hizo. Unaona!!! Subiri!!!!!!!!!

  Mi ningekuwa wewe ningeshukuru sana kwa nafasi hiyo, maana mi walikuwa wananitokea lkn nashindwa kuamua naishia kuharibu. Dunia ya leo ni ya magonjwa sana. Hali ikiwa hivyo hata silaha hukumbuki maana na wewe unajisikia ahaaa! Mi napendwa mie, kesho kifo.

  Kwa hiyo kaza buti usome sana na upate kazi yako na sasa utafute mke. Mke wa kuoa hayupo chuoni kwako peke yake, hatuoi elimu au mali unaoa mtu (kwa upendo wake kwako). Wapo wasichana wa vyuo vya chini, kwa hiyo wapo wengi sana ni wewe tu mtu wangu.

  Kila la kheri
   
 10. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #10
  Aug 6, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Hili tatizo linahitaji dokta.
   
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Aug 6, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  wewe unatongoza ambao sio level zako
  ndo maana unakataliwa
  hebu shuka chini
  anza na akina mama ntilie hivi wa maeneo ya kwenu upate uzoefu.....
   
 12. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #12
  Aug 6, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,331
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  duh mama ntilie?? no. anza na madent
   
 13. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #13
  Aug 6, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Da Wewe Eng. wa CoET kweli??? Shukuru mungu unavyokataliwa,Kata Nondo Malizia mwaka mmoja huo au unapenda sapu wewe,Pata kazi utawakimbia wewe sasa kama wadau wanavyokwambia,pili kama boss alivyokwambia unawafata matawi ya juu,mimi nakushauri tafuta VIDU(Viwango Duni) au FUSP,lakini kuwa makini vyuoni kuna watoto wa mama Ki.kwe.te(waathirika),Wapo Chuo cha Mwalimu na UDOM na CoET Hapo.....
   
 14. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #14
  Aug 6, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Boss jamani mbavu zangu!!!!!!!!!!!! unanichekesha hasa leo,mbona una mpelekea mwenzio huko kwa mama ntilie? ebu mwambie akupe pic yake ili umpe darsa lilotimia mama ntilie anaweza kumkata akasema umri wake mdogo sasa basi akishakutumia pic yake ndio utamwambie nini afanye nakuaminia ww mjuzi wa mambo.
   
 15. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #15
  Aug 6, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Kwa kampany au yale mambo yetu yale? Kama ni yale basi endelea kuvumilia usiwe na haraka subiri NDOA vinginevyo uta frustrate mdogo wangu ukiingia kichwa kichwa!
   
 16. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #16
  Aug 6, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  ha ha haa
  wewe bana...
   
 17. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #17
  Aug 6, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Au unafanana na Dr. Remy
   
 18. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #18
  Aug 6, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Au unafanana na the late Dr. Remy?
   
 19. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #19
  Aug 6, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,315
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  <br />
  <br />
  umeona ee! Huyu msela inaonyesha ni bakhili.
   
 20. CHE GUEVARA-II

  CHE GUEVARA-II JF-Expert Member

  #20
  Aug 7, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 531
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Jamaa inaonekana boom lake hapendi kuligawa kwa watoto! Wengine huwa wakitoka out (au hata kama imetokea mko na dent wa chuo pamoja mnakula msosi) unamlipia! Ikifika wiki mbili tu boom kwishney!
   
Loading...