Elections 2010 Nahitaji Ilani za Vyama

AK-47

JF-Expert Member
Nov 12, 2009
1,373
199
Wana JF nimehaha kutafuta Ilani za Uchaguzi za vyama vya siasa bila mafanikio nilienda CCM nikaambiwa zinauzwa lakini mara bado mara anayeuza hayupo..nikatia timu CHADEMA nikaambiwa hazijatoka mtu mwingine akasema nimuone Mwenyekiti. Kwa hiyo naomba kama kuna anaweza kupata japo soft copy za vyama kadhaa atutumbukizi jamvini ili tuzisome na tuzielewe kisha tufanye uamuzi sahihi Oktoba 31.
 
Manifesto za Uchaguzi siyo jambo universal kwamba kila chama lazima wawe nayo kwani hiyo siyo legal document kama katiba. Wengine huweza kutangaza sera zao kwa mdomo tu bila kuandika popote wakaukbaliwa. Siyo wapiga kura wengi wanaoweza kusoma kijitabu cha kurasa mia mbili na hamsini kutaka kujua Chama kitafanya nini. Shwarzenegger alitangaza sera zake kwa mdomo tu bila kuandika popote.


After alll ni makosa sana CCM kuendesha nchi kwa kutumia manifesto yao kwa vile haikuhidhinishwa na bunge; manifesto ni kama tangazo la biashara la kujinadi ili wachaguliwe. Inatakiwa baada ya uchaguzi waipeleke manifesto hiyo bungeni ili iidhinishwe kutumika kama sera (policy). Kuna ahadi ambazo Bush aliahidi kuhusu immigration lakini bunge aliposhika madaraka ya Urais hakuweza kuzitekeleza kwa vile bunge la nchi yake halikuafikiana nazo.
 
Pamoja na hayo yote mie nazihitaji kuzisoma bado zinamuhimu sana kwangu kama vyama vingine havitoi sawa lakini vinavyotoa nikipata nitashukuru sana.
 
Back
Top Bottom