Uchaguzi 2020 Queen Sendiga ametaka atakayeshinda kiti cha urais asiache kuwatumia wagombea wenzake wala kusita kutumia ilani za vyama vyote

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Dar es Salaam. Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha ADC, Queen Sendiga amemshauri mgombea atakayeshinda kutowaweka kando wagombea wenzake walioshiriki kinyang’anyiro hicho.

Mgombea huyo amesema Serikali shirikishi ndiyo chanzo cha maendeleo, hivyo ni vema rais atakayeshinda akawaweka karibu washindani wake, ili kupata mawazo yao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 27,2020 amesema licha ya kuwa dhamira ya ADC ni kuchukua dola, anatambua mgombea atakayeshinda ni mmoja hivyo anaweza kuwa yeye au wa kutoka chama kingine.

Sendiga ameeleza kuwa endapo atashinda yeye, atazitumia ilani za vyama vyote hata kwa kuchukua mambo machache.

“Mgombea atakayefanikiwa kuchukua kiti cha urais, washauri wake wa kwanza wawe watu ambao ameshindana nao, kwani Serikali shirikishi mara nyingi huleta matokeo mazuri na ya haraka katika jamii,” amesema.
 
Anatamani uteuzi huyo dah njaa hizi
emoji23.png
emoji23.png
 
Ndicho alikuwa anatafuta maana hata mwenyekiti wa chama chake alikuwa waziri kwenye serikali ya SMZ.
 
Hapo sasa kila eneo limejaa unajikuta kuna li rc moja linakufa na kupona kuiba kura afu bada ya mwez halina kazi na dhambi limepata
 
Huyu mgombea ameendesha kampeni zake kistaarabu sana, mwelekeo wake kisiasa ama wa chama chake una dhima ya kujenga zaidi kuliko kubomoa. Namshauri JPM atakapoingia madarakani tena, amchague huyu mgombea kwenye nafasi za ukuu wa mkoa..... Huyu mgombea angetufaa sana kwenye mkoa mmoja kati ya mitatu inayopakana na Congo-DRC. 🤔
 
Kutoka ndani ya moyo wangu nasema huyu mama amefanya kampeni nzuri sana tena pengine kuliko wagombea wooote wa nafasi ya urais

Ningependa tu aendelee kuwa mwana siasa wa namna hio, hii itamfanya kuwa mwanasiasa bora wa upinzani kwa nyakati zijazo.

Ningekua karibu nae ningemshauri asikubali teuzi zitakazo mfanya abadili chama ama msimamo wake ama kaliba yake.

Kama alivyosema leo atashirikia na mshindi kwa namna itakayo faa, Ni heri na ni jambo jema na ndilo wengi wetu tunalolitamani yaani umoja wa kitaifa, lakini kama akipata teuzi kwenye chama kilicho madarakani ingependeza kama asingebadilika Kama kwa mama Anna.

Lakini pongezi nyingi sana kwake , na kwa vile kwa mwonekano bado ako na umri mdogo, naamini atafika mbali katika siasa za Tanzania.
 
download (2).jpeg

Queen umeniangusha usingeomba Kupewa nafasi kienyeji vile, Tayari umeshajenga exposure ya kutosha kazi yako imeonekana hata Anna umemfunika, Umepiga kazi Upo Technical Sana.

Ungekaa tu kimya Sasa hapo Ni wazi unaonekana mchumia tumbo, Wewe vipi ukienda ugenini kwani ukikaribishwa Mara ya kwanza msosi si unazugazuga kuwa umeshiba.

All n all Hongera Sana siyo tu kampeni Ila kuna kitu umekijenga kwa wanawake wenzako, Hususani mwaswala ya Usawa wa Jinsia.
 
Dar es Salaam. Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha ADC, Queen Sendiga amemshauri mgombea atakayeshinda kutowaweka kando wagombea wenzake walioshiriki kinyang’anyiro hicho.

Mgombea huyo amesema Serikali shirikishi ndiyo chanzo cha maendeleo, hivyo ni vema rais atakayeshinda akawaweka karibu washindani wake, ili kupata mawazo yao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 27,2020 amesema licha ya kuwa dhamira ya ADC ni kuchukua dola, anatambua mgombea atakayeshinda ni mmoja hivyo anaweza kuwa yeye au wa kutoka chama kingine.

Sendiga ameeleza kuwa endapo atashinda yeye, atazitumia ilani za vyama vyote hata kwa kuchukua mambo machache.

“Mgombea atakayefanikiwa kuchukua kiti cha urais, washauri wake wa kwanza wawe watu ambao ameshindana nao, kwani Serikali shirikishi mara nyingi huleta matokeo mazuri na ya haraka katika jamii,” amesema.
Hongera Queen Sendiga kuteuliwa RC.
Pasco
 
Back
Top Bottom