Nahitaji fundi mzuri wa TV

Nahitaji fundi mzuri wa TV

Lupweko

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Posts
25,093
Reaction score
27,181
Nilikuwa nina TV yangu Hitachi flat screen, rangi ya silver, bahati mbaya iliungua maeneo ya power supply kutokana na kuyumba kwa umeme, wakati huo nilikuwa sijaiunganishia umeme kupitia voltage stabilizer. Nilimpelekea fundi mmoja hiyo TV yangu, akabadilisha capacitor moja na transistor moja ambavyo vilikuwa vimegundulika kuwa vimeungua. Baada ya hapo alitafuta vitu vingine vilivyoathirika lakini kila kimoja kilionekana kizima, ila akiipa umeme kuna mahali unaishia, hauendi mbele. Alihangaika na akili ikamuishia, akaniambia kwamba amefika mwisho wa ujuzi wake wa ufundi wa TV. Akanishauri ninunue mashine (circuit) nyingine aipachike pale, nikakubali. Baada ya kununua na kupachika, TV iliwaka, akanikabidhi TV yangu pamoja na ile circuit ya zamani iliyopata tatizo.

Hata hivyo, focus ya TV baada ya kuweka circuit mpya haijatulia vizuri. Picha ziko out of focus, na nimefanya video settings zote kama vile color, brightness na contrast, lakini the best combination of the three parameters bado inaleta picha ambazo ziko out of focus (angalia mfano wa picha hapo chini). Ninaamini there is nothing to do with software video settings again, so ninahitaji fundi mzuri m,weledi wa TV atakayenifanyia moja au zaidi ya mambo haya:
i. Kufanya hardware video settings za TV iliyofungwa mashine (circuit) mpya
ii. Kuendeleza ufufuo wa mashine (circuit) ya zamani
iii. Kunishauri lolote lililo bora ili ni-enjoy picha za TV

Nipo Ukonga, Dar. Aliye tayari tuwasiliane hapa au katika PM.
Nawasilisha


attachment.php
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom