Nahitaji counseling

florence

JF-Expert Member
Mar 5, 2011
423
159
Tafadhali nisaidienimwenzenu boyfriend wangu ambaye ndiye mchumba ameniacha bila sababu za msingi, nilimpenda sana na kibaya zaidi nimepata ajali ndo akaanza visa mpaka kuniacha. siwezi hata kula napata msongo wa mawazo mpaka kulala inakuwa tabu. Naombeni ushauri ambao utanisaidia nirudi katika hali ya kawaida nateseka sana kisaikolojia. Natanguliza shukrani kwa ushauri mtakaonipatia
 

utantambua

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,367
319
Shukuru tu kaonyesha his true colours mapema bado mkiwa boyfriend/girlfriend. Ingekua mko katika ndoa tayari ungekua umepatikana lakini kwa sasa kiroho safi kabisa ruhusu hali halisi ichukue mkondo wake.
 

hayaka

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
474
100
pole sana but unatakiwa ujue hayo ndo maisha. kaza buti, songa mbele. hebu jiulize kama angekufa leo ungekufa naye??? maisha bila yeye inawezikana.
 

Makindi N

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
1,066
173
Duuuuuuh! Pole! Wanaume at the worst part us............. Hope u gotta close friends/relatives tumia muda mwingi ku-socialise nao.... Toka Dar for sometimes au hamia sehemu nyingine ya Dar for another experience of lyf... Na mengi utakayoshauriwa humu jamvini.........
 

Vonix

JF-Expert Member
Apr 23, 2011
2,886
1,435
Pole sana,ila kuoa/kuolewa mara zote mtangulize Mungu usijaribu kwenda kwa hisia zako tu utakwama Mungu amekuonyesha huyo si mchumba wako wa ukweli alikuwa anatimiza tamaa zake tu kwako.Pia dada na kwa wote tuliopo jamvini tuepuke kupenda sana siku mambo yamehalibika moyo unaumia sana kama yalivyompata huyu dada,inawezekana wewe ulikuwa unampenda sana kumbe yeye nakupenda kiasi tu yalipotokea hayo yaliyokupata akasepa kirahisi tu.Mwachie Mungu dumu kwenye maombi atakusahalisha nae tu.
 

Mtalingolo

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
2,182
408
Pole sana huwezi kujua mtu moyon mwake anawaza nini. Pengine hakukupenda sana kam wewe ulivodhania. Piga moyo konde maisha uyashinde..
 

mayoscissors

JF-Expert Member
Nov 24, 2009
975
471
Pole sana ndugu kwa tatizo hilo,naliita tatizo kwani linakusumbua,nafurahi pia kwani umegundua kuwa ni tatizo na tiba umeanza mwenyewe kwa kutambua tatizo na kuomba msaada,swala la msingi hapa ni wewe kufahamu kuwa unadhamani kubwa sana wewe ndo wa kwanza kujijali hivyo huyo ambaye kakukimbia kwa kupata ajali kaona kuwa wewe si wa msaada kwake.Watu wengi wanafanya hivyo ila kuna wachache kama wewe ambao hawawezi kufanya hivyo na ndo maana unashangaa na kuumia.
Nakushauri kwa kuwa una uzima na utu wako msamee huyo bwana bure na anza maisha mengine na mwisho wa siku utaishi kama kawaida na mungun atamleta mwingine.
hangera kwa kuomba msaada ni ishara ya kujipenda.
siku njema
 

Pius Kafefa

Member
Aug 9, 2011
88
20
Pole kwa ajali. Lakini tafuta kwanza matibabu kwa maumivu ya mwili, huyo hawara (wewe unamwita boyfriend) siyo dawa kwa matatizo yako ya sasa yaliyotokana na ajali. Ukipona au kupata nafuu tutakupa ushauri. Hata hivyo si busara kuwa na 'hawara', vile vile tumia muda wako kukaa na kuongea na ngugu au jamaa wako wa karibu - sio boyfriend mdadala.
 

sweetlady

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
16,947
8,355
Bila sababu ya msingi?!! Hebu sema sababu aisee.
Amesema amepata ajali ndio mpenzi a.k.a mchumba akaanza visa na hatimaye kumwacha... Kuanzia kesho naanza kukutengenezea juice ya mchicha manake naona Sayona imeanza kukuharibu macho! Sema sante!
 

Husninyo

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
23,735
9,119
Amesema amepata ajali ndio mpenzi a.k.a mchumba akaanza visa na hatimaye kumwacha... Kuanzia kesho naanza kukutengenezea juice ya mchicha manake naona Sayona imeanza kukuharibu macho! Sema sante!

sante bodyguard. Nitengenezee na juice ya mlenda.
 

Nyalotsi

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
6,931
4,910
ngoja nimwambie kloro akufukuze kazi. Unamjibu vibaya bosi.

mmh!! Nyie watu kwa kuchakachua siredi za wa2! Mi napita tu,ila aangalie asije akatumbukia kwetu tunaosubiri mtu aachike kisha tumlie mingo!
 

Beautiful Lady

Senior Member
Jun 8, 2011
135
43
Tafadhali nisaidienimwenzenu boyfriend wangu ambaye ndiye mchumba ameniacha bila sababu za msingi, nilimpenda sana na kibaya zaidi nimepata ajali ndo akaanza visa mpaka kuniacha. siwezi hata kula napata msongo wa mawazo mpaka kulala inakuwa tabu. Naombeni ushauri ambao utanisaidia nirudi katika hali ya kawaida nateseka sana kisaikolojia. Natanguliza shukrani kwa ushauri mtakaonipatia

Pole sana. just know kwamba huyo ni binadamu wala sio Mungu. kama amekuacha huna sababu ya kuumia sana .tulia utapata mtu mwingine atakayekupenda kwa dhati na sio msanii kama huyo.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom