Bungeni ndo mahali penye kila aina ya fani, kuna madaktari, walimu, wanasayansi ,wachumi nk. Kwa ujumla wao sisi tunawaita wanasiasa. Katika hali ya kushangaza, sio kwa wanaojiita wapinzani, wala wanaojiita watawala, wote wanafanana. Ukianza kungalia session ya bunge utatamani mtoto asiwepo kwani lolote laweza tokea muda wowote ikiwemo maneno yasiyofaa kwa watoto wadogo.
Point yangu hapa ni kwamba namna bunge linavyoonekana ndivyo tulivyo hata sisi tulio nje ya bunge,- sisi ndo tumewapeleka mjengoni kupitia kura, sisi ndo tunaokaa nao huku mitaani, ni kaka zetu, dada zetu, mama zetu, baba na hata babu zetu. Kuna vijana wa kuanzia miaka 20 hadi wazee wa miaka takribani 80. Hawa wote tunaishi nao kwenye jamii moja. Hivyo kinachoonkana bungeni ni sampuli(sample) ya muonekano wa watanzaia jinsi tulivyo na busara zetu.
Ushauri wangu ni kwamba tuangalie tulipopotoka tujisahihishe sisi kama jamii ili hata viongozi wetu wa-reflect jinsi tulivyo. Kwa sasa hata kama ww ukaenda bungeni leo, hutakuwa tofauti na waliopo mle ndani maana kizazi chote kinafanana.....hakuna cha Wenje, Cheyo, Mrema, Sitta, Sugu, Mnyaa, Kilango wala nani, ndani na nje ya bunge, kwa wasomi na wasio wasomi, maskini kwa matajiri, watoto kwa wazee, tunafanana kimaadili. Kwa pamoja tunatakiwa tujitathmini na tuamue kwa dhati kuwa na jamii yenye mfumo utakaozalisha taifa lenye maadili mazuri na upendo, hatimaye kupata viongozi wenye maadili na upendo pia.Hili linatakiwa lianzie kwenye ngazi ya familia na kuendelea. Kwa wanaofuatilia bunge wanaelewa ninachosema. Nawasilisha.