Habari zenu wakuu,
Nimekuwa nikisoma post za watu wengi humu Jf na wakati mwingine kuchangia,kwa kweli kuna mambo yananichanganya sana mpaka najiona sina bahati ya binti wa kujenga nae maisha,nilikuwa na mchumba ambae nilidumu nae kwa mda wa miaka minne na tulikuwa na mipango ya kuoana ila badae wazazi wake walikuja kwenda kumsomesha mkoa mwingine na amemaliza kusoma na sasa anafanyakazi huko nakuishi huko.
Miaka mi3 imepita sijamuona na amekata mawasiliano kabisa. Nina umri wa miaka 32 na nimeshapata wachumba zaidi ya 7 ila huwa wananiacha katika hata bila kugombana,sivuti sigara wala sinywi pombe ya aina yoyote pia kipato changu ni cha kawaida tu. Umri unaenda nahitaji kuwa na familia yangu ila sijapati mwanamke aliyesiriazi na maisha.
Je, nitakuwa nakosea wapi wakuu?Izingatiwe imepita miaka mi3 sina mchumba anayeeleweka sababu huwa wanabadisha uamuzi wa mwishoni? Au nitakuwa nimeumbwa niwe single tu nini?
Ushauri plz