Uko sahihi kabisa. Hapa kuna vitu vingi hatuvijui ila tunakimbilia kusema huyu mwanamke ni this n that. Ogopa sana mwanaume anaekupa stori kujionyesha kuwa ye ni victim wa matukio mabaya ya mkewe au girlfriend. Mtu wa namna hii mara nyingi ni mbaya na guilty consciousness yake kwa anayoyafanya humfanya kujivictimize ili aonekane ye ni mwema. Hivi unaweza ukawa na matatizo ya uhusiano tangu mnaanza kuishi pamoja then hamfungi ndoa, then mnapata two more kids bila ndoa. Na mnaishi tu, na haya matatizo mmejaribu vipi kuyatatua as in third part imehusishwa?(wazazi mmewahusisha matatizo yenu na walifanya nini?)Ulisema ulimrudisha kwao kwasababu gani? Je , hana hata kaka zake au babake ? Nashindwa kuamini sababu ipo familia yenye tatizo kama lako lakini mlalamikaji ndiye hasa tatizo.
Kwani kuchat na ex girlfriend wa kaka yao ni kosa...
Unajua wamemjualia wapi...?
Unajua kuna makaka wana date marafiki wa dada zao?
Jamani tujitahidi kuolewa kwetu kusiwe chanzo cha kusambaratisha familia za watu...
Kwani ukifanikiwa kumtenga mumeo na familia yake huwezi kuwa na amani kwenye ndoa yako kama huyu na mkewe...
Kwani mume akiwa hana amani wewe utaitoa wapi...?
kumbuka hao ni nduguze wewe ni mke ...kila mtu ana nafasi yake ...huwezi kuziba nafasi yao....moyoni anasononeka mwisho anakuchoka...
Kimsingi nimezungumza shida ya moyo wangu, kama ana shida ya moyo wake atazungumza kwenye jukwaa lake. Mimi na yeye tumeshakaa vikao vingi na mara nyingi huwa naishia kujuta kwa nini nimeanzisha mada. Kwa mfano, kuna kipindi nilitoka safari nikamkuta nje nikamsalimia nikaingia ndani, yeye alibaki nje. Nilitua vitu vyangu na kasha nikakaa chumbani. Baadae nilimpigia simu aje chumbani (ili nimuonyeshe kuwa nimemmiss) alipokuja nikaanza kumtania na kumchezea, baada ya muda akaniambia nimsubiri anakuja. Alitoka nje akaenda kukaa na housegirl, nilikaa chumbani kumsubiria mpaka nikapatwa na hasira nikaamua kuondoka. Nilimpita nje akiwa anapiga stori na housegirl wetu. Usiku niliporudi nikataka kikao naye, badala ya kuongea alikuwa anaangua kilio tuu, tukakaa siku mbili bila kulala. Badala ya mazungumzo ya kutafuta suluhu tunaishia kugombana.
N'way, una uhuru wa kuniona mkorofi kwa kuwa hunijui, hilo ni lako na huenda una experience na watu wa namna hiyo.
sina tatizo la uelewa kama unavyodhaniwe mtu bwana.....nani kakwambia huyo jamaa amefunga ndoa kanisani? hivi umeisoma vizuri posti yake au unaendeshwa na matukio tu hapa.....?
Ndoa hakuna pale....wanaishi bila kufunga ndoa kwa miaka kumi sasa....kwa hiyo mungu haitambui ndoa yao....wamezini kwa miaka kumi mfululizo hadi kupata w atoto watatu sasa....nadhani tuanzie hapo....
kwahiyo ushauri wangu kwake nimeuelekeza vilevile kama wanavyoishi(kishetanishetani)....hopeful umenielewa sasa
Wewe ni mpumbavu kweli!! Miaka kumi??! watoto watatu??! Yaani baada ya kumzeesha ndio umegundua humpendi au?! umejiita msomi wa digrii! Shenzy sana!!
Kaushauri kidogo tu. Talaka si dawa, pia kumwona mkeo kuwa ndo mbaya si vyema. Jiulize, umewapataje hao watoto wako 3?? Je, ulikuwa unamwekea kwa mrija au ni kukutana naye kimwili?? Lazima kuna kamapenzi flan hivi kati yenu.
Huenda huyu mama amekupenda mno kiasi kwamba anatafuta mbinu ya kukaa na weye kila saa. Hujatuambia kama unapokuja week ends huwa una nafasi zaidi na mkeo au ni kama mtu aliyekuwepo hapo nyumbani. Mkeo kukutuhumu kuwa una wanawake (Wake wengine) mpaka anakuona utamletea ukimwi. Ni mashitaka mabaya mno, huenda ukija hujui mwenzio amekungoja kwa hamu kuu. Unaingia na kuzama ghafla hujui katosheka unaanza mipango ya safari kesho kurudi kazini.
Mke si jengo la nyumba, ni zaidi ya hicho. Mke si kumzalisha watoto, ni zaidi ya hilo, mke ni wewe kupata nafasi na yeye. Kabla hujawaza kuachana, hebu tafuta njia ya kupata nafasi nzuri na yeye, umshibishe ukimwondoa genye zake. Mwanamke (Naomba msamaha kwa nitakaye mwudhi hapa) akiwa na hamu ya mumewe ni hatari. Anaweza kutumia chochote kilicho mbele yake na hataki kuguswa guswa bila mtu kumtoa hamu. Fikiri kwanza kabla hujachukua hatua.
Ndugu mbona majina yanafanana
Pole sana mkuu, mke wako yaweza kuwa anatatizo lakini pia utafute chanzo cha hayo matatizo ni nini? familia zetu nazo zinachangia kwa kiasi kikubwa kucreate tatizo na inapokutana na mke kasirani hali ndio inakuwa mbaya zaidi.
Nakuambia hivo kwasababu na mimi na experience hali ya mawifi wamekuwa hodari sana kuchat na x girlfriend wa kaka yao na ni kwa open ata ktk social networks naona, kwa vile mimi si mshari nanyamaza ila ukikutana na mtu ambae hawezi kuvumilia lazima reaction yake itakuwa kubwa, hivo mtu kama mimi nikimuambia mume wangu siwapendi wifi zangu hawezi kunielewa lakini kama ana busara inabidi anielewe sana tu.
Mara nyingi wanawake tunakuwa na upendo sana ukiona mwanamke anabadilika ghafla ujue kuna sababu inayompelekea kubadilika na once akibadilika kumbadilisha tena kazi sana, sasa kama unampenda tafuta njia ya kutatua na kufaham chanzo cha tatizo, lakini kama unahisi imeshindikana achaneni kwa wema
Hapana sema Babaaa, mbona majina yetu mamoja? Huenda weye ni mwanangu, ni PM nikujulishe yangu.