Nahisi simpendi mke wangu

Nahisi simpendi mke wangu

Goboshi

Member
Joined
Jul 15, 2013
Posts
63
Reaction score
27
Nilifanikiwa kuoa miaka kumi iliyopita na katika maisha yetu ya wawili tumefanikiwa kupata watoto watatu, wote wa kiume.

Migogoro katika maisha yetu ilianza mara baada ya kuanza kuishi pamoja. Mimi na mke wangu tulianza kuishi pamoja kabla ya kufunga ndoa. Binafsi nilimpenda sana na nilitamani kumfanyia kila ninaloweza ili awe na amani na furaha.

Kiukweli tulianza kuishi kwa amani na furaha mpaka pale mke wangu huyu alipoanza chokochoko dhidi ya mama yangu. Alianza kuniambia kuwa mama yangu hampendi na wala alikuwa hataki aolewe na mimi na kisha akaanza kwashambulia wifi zake. Nilijiuliza maswali mengi na baade nikagundua kuwa ni maneno ya kutunga.

Kilichonifanya niamini ni baada ya kukumbuka kwamba mimi na mke wangu tumechukuana kwa maamuzi yetu binafsi (mimi siwashirikishi wazazi) na pili ni kwamba wazazi wangu wanaishi mbali na anapoishi huyo mwanamke, na tatu hapajawahi kuwa na mahusiano yoyote na wala mawasiliano yoyote baina ya familia hizi mbili.

Hapo nikaanza kumuona mke wangu kama mtu wa shari. Mke wangu nilimtoa bara kuja kuishi naye Dar es Salaam na nilitamani kuja kufunga nae ndoa.

Baada ya kuishi naye kwa mwaka mmoja jijini Dar es Salaam na tukiwa tumefanikiwa kupata mtoto mmoja tulipanga safari ya kwenda kijijini kuwasalimia wazazi pamoja na kujitambulisha kwao. Ilipofika Jumapili nilimwambia tutaenda kanisani na tutajitambulisha tukiwa pamoja ili kanisa litupokee na baadae tuanze mchakato wa ndoa.

Tulikubaliana kwa ajili ya hilo ila tulipofika kanisani kabla ya kuingia kwenye ibada huyu mwanamke akaniambia nisimtambulishe kanisani na wala nisijaribu kumtaja. Nilipatwa na hasira iliyoharibu ibada yangu na tuliporudi nyumbani ikawa ni ugomvi tu.

Mimi ni msomi mwenye digrii na mke wangu ni mama wa nyumbani. Niliamua kuoa mama wa nyumbani kutokana na nature ya kazi yangu inayonihitaji kuwa mbali na nyumbani kwa kipindi kirefu nikiwa kwenye camp.

Maisha yaliendelea hukutukiwa na migogoro isiyoisha kila mara akinituhmu kwa mambo mbalimbali, mara nyingine alinituhumu kuwa nina mke mwingine na nimemjengea nyumba na mara nyingine ananituhumu kuwa namuua kwa UKIMWI.

Sikujisikia vizuri na mara kwa mara nilikuwa naenda kupima ili awe na amani na kuna kipindi nilikuwa namchukua kwenda kupima ila yeye anachukua vipimo vingine na kukataa kupima UKIMWI.

Mimi huwa napima na majibu namuonyesha. Katika hali hizo nilijikuta maisha yangu nyumbani yanakosa furaha na mara kwa mara ni mizozo mara huu mara ule. Hata tendo la ndoa ilikuwa nadra kulipata kwa hiari na wakati mwingine nahisi ana mwanamume mwingine anayemzuzua.

Mbali na kuwa mbali kwa muda mrefu, muda mfupi tunaopata kuwa pamoja unakuwa na majonzi tele. Kuna kipindi nilisafiri kwa wiki sita 6 na niliporudi nikadhani mwenzangu amenikumbuka ila nilichokiona usiku ni kibaya. Tulienda kulala na alipojilaza tu akavunga amesinzia usingiz mzito, nilijaribu kumuamsha ila akavunga kufa. Nilijaribu kulala ila sikuweza kupata usingizi nikaamua kwenda kulala kwenye sofa sebuleni ili nijisikie niko safarini.

Kuna kipindi nilipoteza kazi akaniambia ameonyeshwa kuwa hayo ni mapigo na wala sitakaa nipate kazi tena. Wakati huo nilikuwa nimepata kiwanja hapa Dar es Salaam na nikiwa najipanga kuanza ujenzi.

Nilikaa mtaani miezi miwili na baadae nikapata kazi mpya. Baaada ya kupata nilimwambia nataka kuanza ujenzi, yeye aliniambia ni vema nikaacha kujenga kwani nitapata hasara.

Nilimuuliza hasara gani nitapata akasema hiyo nyumba itakuja kuuzwa ili tugawane hela. Mi nilimambia simsikilii yeye ila naangalia mahitaiji ya watoto wangu kwamba wanatakiwa kuwa na nyumbani kwao.

Nilibahatika pia kupata gari na siku moja nikiwa safarini peke yangu kwenye gari nilipata ajali ya kugongwa na gari nyingine. Bahati nzuri ni gari iliharibika ila mimi nilibaki salama.

Baada ya tukio hilo siku moja tukiwa kwenye mzozo alinitolea neno kali kuwa nilipata ajali kwa maombi yake. Anadai aliomba nikipakia mwanamke kwenye gari yangu nipate ajali. Nilijisikia kumrukia nimle nyama mbichi lakini nikajizuia.

Mizozo imekuwa mingi mpaka najisikia kumtapika, sina amani wala furaha niwapo
 
pole sana bro, hayo yalikuwapo, yapo, na yataendelea kuwepo. ungeanza kujiuliza pale tu alipokuambia usimtambulishe kanisani. muda umepita na watoto 3 mnao.....? ukimuacha kwa sasa kama alivyokueleza mtagawana mali. tumia zaidi busara na wala si nguvu, huyo hayuko pekeyake.
 
Pole na maswahibu inaelekea huyu mama ana ka wivu ka kijinga au ana mtu ana mzuzua kwa nin msende kwa wazaz wenu waweke chini kuona tatizo lipo wapi
 
pole sana kwa yaliyokukuta wewe ndiye unayejua ni kiasi gani unaumia .. na ni kiasi gani unapata maumivu ya moyo... maamuzi yako yaweza kuwa sahihi japo bado inakubidi ukubaliane na jamii itakuchukulia vibaya .... kumwacha ni moja na ni sahihi lakini pia je watoto wenu wataishije uwe tayari kutoa matunzo ya mtto....

Na pia sikushahuri kukimbilia kuoa mke mwingine kumbuka kuoa ni masaa macahache sana ila ila impact itaweza last for more than a years...... make sure unafanya uwezalo upate upate furaha yako......usisikilize jamii zaidi lazima lawama zitakuja kwako ila kubaliana ni yatakayokuja mbele yako.................

narudia tena wewe ndiye unayejua moyo wako umejeruhika kiasi gani ... jamii itakushauri bla bla nyingi... ukweli unaujua moyoni mwako...
 
Dah! Pole sana kaka. Huyo mkeo mbona kama mshirikina flani vile!? Anyways, kumuacha sio too late, ila angalia mustakabali wa watoto kwanza. Huna haja ya kuishi stressful life while life is too short. Kuishi kwako isiwe adhabu kwako. No matter how far you have gone down the wrong way.....TURN BACK.
 
Nimeshafikiria kuachana nae na hilo limekuwa wazo linalozunguuka kwenye kichwa changu kwa muda sasa, nimepoteza mapenzi na yeye kabisa. Naona kama tunaishi nyumba mbili tofauti na ninatamani akae mojawapo ya nyumba zetu na mimi nikae nyingine. Ukweli kuna kipindi nilimwambia achukue kila kitu aniache huru tu, kwani najua hana moyo wa kutafuta.

Nimejaribu kumpeleka shule nikijua tatizo litakuwa ujinga akaamua kuacha. Akawa ananilaumu kuwa simpendi kwa kuwa hana kazi nikamwambia afungue biashara nimpe mtaji akakataa. Kuna rafiki yangu amemfungulia duka mke wake aliniomba nimkutanishe mke wake na wangu ili amfundishe biashara, mke wangu akakataa.

Nikajaribu hata kumwambia afungue salon awe anasimamia akakataa. Kila kitu yeye ni mpinzani kwangu na kila ninachofanya yeye anapinga. Nikijaribu ku-support huduma za kijamii anakuja juu kama mbogo. Hakutaka hata nichangie harusi ya ndugu yangu na nilipochanga hakuhudhuria harusi ile. Naishi maisha ya kujitenga na jamii mpaka najiona mpweke. Nimempa hela akafungue akaunti benki ili niwe namuwekea hela ya matumizi huko lakini fomu zina miaka miwili ndani hazijajazwa.
 
Nilifikir kukushaur hivo ila mwisho wa sik mwenye maamuz n wewe
 
Pole sana mkuu, mke wako yaweza kuwa anatatizo lakini pia utafute chanzo cha hayo matatizo ni nini? familia zetu nazo zinachangia kwa kiasi kikubwa kucreate tatizo na inapokutana na mke kasirani hali ndio inakuwa mbaya zaidi.

Nakuambia hivo kwasababu na mimi na experience hali ya mawifi wamekuwa hodari sana kuchat na x girlfriend wa kaka yao na ni kwa open ata ktk social networks naona, kwa vile mimi si mshari nanyamaza ila ukikutana na mtu ambae hawezi kuvumilia lazima reaction yake itakuwa kubwa, hivo mtu kama mimi nikimuambia mume wangu siwapendi wifi zangu hawezi kunielewa lakini kama ana busara inabidi anielewe sana tu.

Mara nyingi wanawake tunakuwa na upendo sana ukiona mwanamke anabadilika ghafla ujue kuna sababu inayompelekea kubadilika na once akibadilika kumbadilisha tena kazi sana, sasa kama unampenda tafuta njia ya kutatua na kufaham chanzo cha tatizo, lakini kama unahisi imeshindikana achaneni kwa wema
 
Ninaposisitiza kuoa au kuolewa siyo lazima wengi huwa hawanielewi.

Mleta mada kama atadivorce nadhani anahitaji sex parter ambaye naye ameshamaliza biashara ya kuzaa na kila mtu aishi kwake.

Ila inaonekana kuna wanaume dhaifu sana maisha yao hayakamiliki bila kulala na kuamka na mwanamke kila siku.
 
Mkuu kanisa kwani linaruhusu zinaa?.... Je madhehebu ya kanisa lenu yanatambua Talaka?....
 
Maisha ni mara moja tu kama hakufai na umejiridhisha timua tu!!!
 
Aisee Pole wengi huwa tunavutwa na rangi na sura zao, huyu hakuwa type yako ndio maana unapata naye shida,uliponzwa na sura yake? Suala la Ndoa ni gumu sana kushauri!!! Niliwahi shauri wakati fulani mahali fulani! Najuta mpaka leo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom