Nahisi sikufanya maamuzi sahihi, ukiwa na umri mkubwa familia ndio faraja pekee

Pole sana mkuu,I can wear ur shoes mzee,mim sijafika uo umri lakin swala LA upweke linanikandamiza mbaya najitaid kufanya kazi lakin jion narudi home,..no one there to say something special to,...inauma sana ila maisha yamebadilika mengine inabidi tuyaache yapite,..ila maisha ya mapenzi yamebadilika sana,..hasa uku kwetu mjini,..MTU unakua unashtuka shtuka tu,
Pole mkuu lakini napenda nikupe moyo tu kuwa ni swala la muda tu utampata aliye sahihi kwa wakati wake.Kuwa mwaminifu tu mbele za Mungu upweke na mengine yote yatakwisha.
 
Polee sana kaka, usikate tamaa Mungu ni mwingi wa rehema atukutendea sawa sawa na hitaji la moyo wako
 
Life ooh life oooooh life ooh life,Mungu yupo nasi wanadamu muda wote.yatakwisha magumu yote wakuu mpka utasahau
 
Familia ina umuhimu wake sio tu kwa wale wasio oa bali hata kwa wale waliooa(married bacholar) na wako mbali na familia zao. Wengi huishia kuwa na mpango a kando na kuwa walevi. Kwa hili lako mkuu bado hujachelewa tafuta unaeona anafaa na kuanzisha mahusiano ya muda mrefu Pia tukumbuke starehe ya peke yako ni upweke.
 
Mimi ni mdau mmojawapo ambaye mke wangu ametangulia mbele ya haki kama miaka minne iliyopita. Watoto wawili was kike wameolewa amebaki wa kiume. Hata hivyo wangu Sasa ni 56 nimeshindwa kabisa kufanya uamuzi wa kuoa sijui mnanishaurije wana Jf. Naona hali ni mbaya ila kila mwanamke ninayetaka kuishi nae anataka salio na pia kujengewa Nyumba. Wengine ni wadogo. Wengine tayari wanafamilia zao kubwa Hii kwa kweli ni changamoto. Nishaurini.
 
Huwa nawashangaa wanaokejeli swala la amilia! ..
Wewe na mtoa mada mmekariri kua familia lazima uwe na mwanaume au mwanamke unaishi nae ndani.

Anyway, kila mtu na mtazamo tofauti kuhusu mambo. Ukiweka akili yako kua furaha/faraja yako haijakamilika au nafsi yako haijakamilika bila kuishi na mwanaume au mwanamke ndani basi utaishi kwa shida sana na mateso ukitafta faraja yako.

Mimi binafsi, hilo sio tatizo kwangu, sijawahi kuwaza kuhusu hilo jambo, na ikitokea basi nitatafta mtoto mmoja au wawili.
 
Pole sana
Ila usikate tamaa bado furaha yako iko mikononi mwako wewe ndio wa kuamua si mtu mwingine akuamulie
 
Wewe na mtoa mada mmekariri kua familia lazima uwe na mwanaume au mwanamke unaishi nae ndani.

Anyway, kila mtu na mtazamo tofauti kuhusu mambo. Ukiweka akili yako kua furaha/faraja yako haijakamilika au nafsi yako haijakamilika bila kuishi na mwanaume au mwanamke ndani basi utaishi kwa shida sana na mateso ukitafta faraja yako.

Mimi binafsi, hilo sio tatizo kwangu, sijawahi kuwaza kuhusu hilo jambo, na ikitokea basi nitatafta mtoto mmoja au wawili.
Itakuwa umelelewa na mzazi mmoja ila kwa sisi tuliolelewa na baba na mama tunaelewa maana ya familia...subili ukuekue ipo siku utajua umuhimu.
 
Itakuwa umelelewa na mzazi mmoja ila kwa sisi tuliolelewa na baba na mama tunaelewa maana ya familia...subili ukuekue ipo siku utajua umuhimu.
Ndio maana nimekwambia umekariri na unataka kulazimisha mtazamo wako uwe hivyo kwa kila mtu. Hata ungekua umelelewa na wazazi 7 bado huo ni mtazamo wako. Hizi akili za kukariri sijui hata kama shuleni ulifaulu mitihani, kizazi cha divisheni faivu mna matatizo.

Umri wangu mimi labda nalingana na mama yako, hivyo sina cha kukua.
 
Kwa maneno yako tu inaonyesha una msongo Wa mawazo ila sikulaumu inaonekana una tatizo kubwa sana ambalo nimeliona kwa wanaume wengi wenye umri mkubwa alafu hawana familia wanalo!... pole hujachelewa punguza kupanic utapata mke.
 
Haaha, i was just reading your mind na nimefanikiwa. Ahsante kwa ushauri na uwe na siku njema.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom