Nahisi ninatumika kupita uwezo wangu

Nahisi ninatumika kupita uwezo wangu

Cruel mpole

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
282
Reaction score
106
Asalaam wana jf.

Mimi ni kijana wa umri wa miaka 23,naishi kwangu ,sina familia wala mke wala grfriend,nafanya kazi serikalini,elimu yangu form 6 na nina certificate ya accounts ambayo nimejisomesha mwenyewe.

Napenda sana kuendelea na masomo lakini kuna masuala yanaingiliana ambayo niyakifamilia pale ambapo najihisi navunjika moyo kama ipo siku nitaendeleza elimu yangu,kwasababu zisizo na msingi za wanafamilia kunitumia kama mtatua matatizo ya kifamilia.

Kipato changu kidogo,napata kwa mwezi mshahara usiopungua laki 6 kwa mwezi,lakini sioni faida yake coz unafika wakati nakosa hata pocket money kwa matumizi yangu ya kukidhi mahitaji ya kila siku,coz ndugu na jamaa wanalia matatizo kila kukicha,mara huyu hivi mara huyu vile,nakosa raha,majukumu yananiandama,nahisi hata mwaka huu sitoweza kuingia chuo kujiendeleza kielimu coz it has been too much.

Najaribu kuwafumbia macho term hii ili nami nipate nafasi yakujiendeleza kielimu,ila sijajua watanielewaje,na nimejaribu kuwaelewesha lakini waaapi,hawakomi kuleta shida zao kwangu.

Zamu hii mimi sitaki kabisa,na ninabadiri namba yangu ya simu wasinipate kwa muda wa mwaka mzima,nimenuia kufanya hivyo,nimewaendekeza vyakutosha,naomba wanisamehe kwa hili.

HAYA NDIYO MAAMUZI YANGU,ILA NIMEONA SI VIBAYA NIKAPATA MAONI YENU JUU YA JAMBO HILI.

KARIBUNI.
 
Pole sana mdogo wangu, haya matatizo yapo kwa wengi tu na uamuzi wako wa kubadili simu sikushauri ila waambie kila mtu ana matizo nawe pia una madeni unayolipa nao wakusaidie wageuzie kibao watakuacha, kama hiyo tactic itashindikana uwape ukweli siwasaidii yangu menyewe mazito. NB; usiache kusaidia wasiojiweza kabisa
 
Hizi extended family hizi we acha tu.

Saidia pale ambapo unahitajika kusaidia tu. Pili usiogope lawama maana hata maandiko yanasema tufanye kwa kadiri.. (wema usizidi uwezo)

Pili:ndugu hata umlambe miguu.... kamwe hatakaa aone umemsaidia kitu.. anajua ni wajibu wako.... Kwa hiyo unaposaidia ndugu lazima uiambie akili yako unatoa sadaka. wachache wataona umesaidia.

Tatu: Kumbuka kusaidia ni kama kuwa golikipa.. haijalishi golikipa ameokoa magoli mangapi.. watu huona lile alilofungwa tu. ndivyo ilivyo kwenye kusaidia... hawataona watu au mambo yao mengi uliowasaidia na jinsi ulivyojinyima.. ila wataona pale ulipokosa kusaidia na watakulaumu wakati wote kwa hilo''

Bye.
 
Ubinafsi ni kitu muhimu katika maisha ya binadamu embu kua na mipaka kijana kuna watu ambao ni lzm uwasaidie km wazazi na wadogo zako ambao wanakutegemea tu mm siwezi kua natoa msaada kwa ngd yng ambae ana uwezo wa kufanya kazi vinginevyo utaishia hapo ulipo,ujamaa ulishazikwa zamani.
 
  • hakikisha unasave
  • unaweka hela ya kufanya starehe
  • hela ya nauli
  • na hella ya kuwapa ndugu yako zikiisha achana nao
 
nafikiri kuwaambia umelipa ada ya wewe kusoma ni excuse nzuri tu ya wewe kutotatua matatizo yao. waambie kwa sasa huna uwezo sbb unatarajia kusoma. usipokuwa makini na hizi extended family hautapiga hatua kimaendeleo
 
Pole kijana lakn c wewe 2 wapo weng xana wa namna hyo lakn fanya Maamuzi magum yatakusaidia kijana, tmza yako ya wengne yafuate
 
Hili ni tatzo linatuface wengi. Focus on what is good for you especially by helping those whom you are blood related kama mama baba na your youngs attending schools.
Mfungulie kijimladi mama yako cz yeye ndo engine ya family hapo utaokoa uombaji wa pettycash. Wengne potezea.
 
nafikiri kuwaambia umelipa ada ya wewe kusoma ni excuse nzuri tu ya wewe kutotatua matatizo yao. waambie kwa sasa huna uwezo sbb unatarajia kusoma. usipokuwa makini na hizi extended family hautapiga hatua kimaendeleo

kweli kabisa,yaani kweli mtu anadiriki hata kuniomba pesa ya nauli!!?hata kunitaarifu mapema kwamba anasafari,eti naenda mkoa flani leo,naomba uniongeze elfu 60,ukimwambia sina,utaona kimbembe.
 
Pole sana mkuu. Niwengi wanakumbana na hili jambo.

Halafu ngoja nikuchekeshe!!! Hao hao unaowasaidia siku ikitokea kibarua kimeota nyasi ndio wa kwanza kukucheka

utasikia ........

Ooooh mtu hana hata kiwanja,
Oooooh hajajenga
Ooooo hajafanya hili....

Hivyo basi achana na wazo la kubadili namba ila cha msingi timiza ndoto zako

pia weka akilini kuwa unapoamua kutimiza ndoto zako kuna watu wataathirika ( ambao watakosa msaada wako )

na utakuwa mtu wakulaumiwa kila siku.

It is better wakulaumu now lkn baadae uwasaidie pakubwa
 
kweli kabisa,yaani kweli mtu anadiriki hata kuniomba pesa ya nauli!!?hata kunitaarifu mapema kwamba anasafari,eti naenda mkoa flani leo,naomba uniongeze elfu 60,ukimwambia sina,utaona kimbembe.

Unawaendekeza

Umezoea kutoa pesa hovyo

Ukimwambia huna atakuchapa? Au maneno yanachoma?

Jifunze kujisimamia kwenye maamuzi

Usifanye kitu kwa sababu ya mtu
 
Mdogo wangu pole sana usipoangalia ndugu hao baadae watakuja kukucheka na kukuona huna maana. Huna haja ya kubadili no ya cmu waambie ukweli huna pesa . Usitegemee ndugu wakuelewe hakikisha unaenda shule kwani umri wako bado mdogo na ni umri unaofaa sana kusoma sababu huna mtoto wala familia. Simama kwa ujasili usiwe muoga jifanyie maendeleo yako . Wapo watakaokuona huna maana kwenda shule au umewatenga au una roho mbaya haya yote usijali focus kwenye kile unachokiona kinakufaa.
 
Mimi sahiv najiandaa na nimeshapanga pindi ntapoanza maisha kabisa kabisa ntawajengea wazazi wangu nyumba za kupangisha ambazo zitakua zinagenerate income ya kutosha kuwahudumia mahitaji yao almost yote...... ikishakua hivo na mimi ntakuwa nawaza kujiendeleza mwenyewe bila usumbufu..
 
mmmhhh
ngoja nimuite watu8 aje afukunyue nyuzi zako zilizopita.
 
Mmh.. Watu wako vyuoni wanasaidia familia za kwa boom, how comes wewe unalia namna hiyo??

Kaka fanya SWOT analysis ya ndugu zako! Wengine wana minguvu yao mingi tu lakini wanataka wakutegemee kwa lazima!
 
Usibadili namba ya simu! Wale wote wenye nguvu zao na mikono na miguu, achana nao, na hakikisha unawaambia msimamo wako.

Waeleweshe wazazina ndugu wa damu, na wajue kua unenda kusoma, pia wajue kuwa msaada utapungua lakini utajitahidi kusaidia unavyoweza.

Ukiendelea kuwazoesha nduguzo hivyo hutafanya chochote na muda utaisha hujatimiza ndoto zako! Kuwa wazi kwao na timiza malengo yako.

Kila la kheri.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom