kwisha
JF-Expert Member
- Sep 9, 2021
- 1,793
- 5,053
Jambo ndugu zangu
Mimi ni kijana ninaishi katika nchi za wenzetu weupe huku nina takriban miaka 9. Na katika hiyo miaka 9 nina miaka 6 ninafanya kazi. Ila cha ajabu na cha kusikitisha pamoja na kufanya kwangu kazi hivyo sina hata kipanda cha njia katika nchi yangu ya asili sio huko tu hata huku niliko sina mafanikio yoyote kabisa
Najikuta nafanya kazi kwa shida na nikipata pesa matumizi yake yanakuwa ya ajabu ajabu tu. Kila nikipata pesa najikuta nazitumikisha kwenye njia ambayo sio sahihi hata nikipanga mipango yangu kuwa wiki hii nikipokea tu nitanunua kitu fulani lakini matokeo yake inakuwa tofauti
Yaani nikiwa na pesa kuliko kutumia kwenye njia ambayo ni sahihi na ya faida kwangu najikuta na zitumikisha kwenye njia ya anasa.
Nimejaribu kutafakari nini tatizo majibu Sipati nimejaribu kukaa na watu wenye akili labda watanisaidia najikuta nagombana nao na ugomvi unakuja pale ninapopata pesa ninakuwa katika hali nyingine tu wakijaribu kunishauria ugomvi unaanza hapo hapo
Halafu ninakuja kutambua nikishaharibu mambo. Walinishauri kuoa, nilioa mwanamke lakini akachukuliwa na wenye nguvu kisa alishindwa kuishi na mimi.
Naombeni msaada kama kuna yeyote anajua kuhusu tatizo hilo anipe dawa basi maana nahisi kama huu sio uchawi basi nitakuwa nina matatizo ya akili kabisa
Nateseka saana hapa nilivyo hivi ninaishi kama homeless tu tofauti yao na mimi ni kuwa wanao wanaishi mitaani na hawana kazi mimi naishi kwa mama na nina kazi
Nilijaribu kuhamia kwangu nilishindwa kulipia nyumba sio kwangu pesa nilikuwa sina nilikuwa nazo lakini nilikuwa nazitumia kwenye njia ya ujinga tu nikaona nitoke niishi na wazazi wangu na wao wamenipokea kwasababu mimi ni mtoto wao tu lakini wameshindwa na tabia zangu