Nahisi hanifai lakini nimeshindwa kumuacha

5997

JF-Expert Member
Jan 19, 2019
514
1,204
Wakuu,

Nimekuwa kwenye uhusiano na binti. Ni takribani mwezi wa nane sasa.Wakuu siwezi kuficha huyu binti ananipenda sana tena sana

Amekuwa akinitafuta mara kwa mara hata nikiwa kazini kunijulia hali, hataki niende kazini bila kumuaga, au nikirudi nimtumie sms kuwa nimerudi salama,Anakuja kwangu mara kwa mara kunijulia hali, si kwamba anafanya hivi kwa kuigiza maana hata pesa sio kwamba namhonga pesa ndefu. Ni pesa ya kawaida tu ninayompa na hana tabia ya kuniomba pesa mara kwa mara, sasa ishu kubwa ni moja.

Huyu binti amekuwa na tabia ya kuwa kwenye mahusiano na wanaume wengine. Siku moja nilishika simu yake nikakuta chatting zake na mwanaume mwingine aliyeonekana kuwa mtu wake,Nilimuita binti nikamueleza kwanini hakutaka kuniambia kuwa ana mahusiano na mtu mwingine?

Alilia sana na akanibembeleza akadai nimsamehe kwani yule si mtu wake kiuhalisi ananipenda mimi na hawezi kunicheat yule anamchora tu. Nikamsamehe siku hiyo ikapita.

Mara ya pili huyu binti alikuwa amelazwa hospitali nilipoenda kumuona akanipa simu nimshikie aisee nilikuta sms karibu za wanaume watatu wote wanaonekana wana mahusuano nae. Nikasubiri aruhusiwe hospitali nikamuita nikamueleza. Nilikuwa na jazba sana nikamwambia kama vipi kila mtu ashike zake maana sioni mapenzi hapo zaidi ananichora tu na ni mnafiki.

Aisee nilipomueleza hivyo alilia sana akaniambia anajitahidi sana kushinda majaribu ila anajikuta anafeli ila kiuhalisia ananipenda mimi na yuko tayari kuolewa na mimi maana mimi ndo chaguo lake. Sio siri siku hiyo alilia sana mpaka nikamuonea huruma mimi mwenyewe ikabidi nianze kumbembeleza. Hilo likapita.

Juzi nilikuwa natoka kazini mida ya saa moja jioni nilimkuta yuko amekaa kwenye bodaboda na mwanaume na bodaboda imepaki na imezima taa. Nikapita kimya kimya lakini aliniona akaniita sikumuongelesha nikapitiliza. Nilipofika nyumbani akanitafuta nikamwambia tena kuhusu nilivyomkuta akanieleza huyo ni boda boda tu na hana mahusiano nae.

Sasa leo nilikuwa nae nimekuja kushika simu yake ameinyakua haraka haraka nilipomuuliza akajiumauma nikajua alikuwa anaficha tu nisikague vilivyomo ndani.

Sasa mimi nimeona kama huyu mi hanifai kabisa kuwa mke wangu maana nahisi huko mbeleni nitakuja hata kumuua mimi maana kwa sasa simchukulii hatua yoyote kwa kuwa bado ni mpenzi wangu tu sijamuoa na wala hatujatambulishana.

Sasa ishu ni kwamba kumuacha nataka lakini nashindwa kwani mimi kumpenda nilimpenda kweli na anaonekana ananijali sana.

Nikitaka kumuacha analialia mno hadi namuonea huruma. Kuna wakati nawaza labda ametupanga anatuchora tu, lakini nawaza mbona mimi amenikomalia wakati hata simpi hela kubwa yani unaweza kukuta ananiomba buku mbili au buki tano au hata mwezi mzima nikampa elfu ishirini tu?

Wakuu naombeni ushauri nitumie njia gani mpaka nimuache kabisa?

Ameniganda kama kupe, ila kashindwa kubadili tabia kabisa.
 
Uyo.anakufaa sana shida yako.wewe ni moja unataka kumuoa yeye na simu yake
Inawezekana kweli nioe mwanamke halafu nisiwe nashika simu yake?
Kama nilivyomuaminifu nataka awe muaminifu pia
 
Sio rahisi akuombe pesa kila wakati na akati ana vikoba vingi, usipo mpa wewe juma anarejesha, juma asiporejesha moses yupo:D:D:D
 
Acha na ACHAAAAAAA KABISA kugusa simu ya mpenzi wako..hata mkeo...muamini anachokwambia...ikibidi mupe kabisa....
Utakuja kufa nakwambia au kuja ua...
Narudia acha kuingilia uhuru wa mpenzi wako wa kimawasiliano..
Yeye ni mwanamke na lazima wamtamani na kumtongoza, na kuna mabaharia kama mimi hata tuambiwe anampenz tuna ng'ang'ana tu...
Kingine ww kwanini unapenda kumkagua sana inaonekana hata weww pia ni Kubuhu kwa ukahaba wa kiume ....over
Acha
Acha
Acha kuingilia na kukagua mawasiliano ya mkeo au mpenz au mchumba na hata rafiki tu hata wakiume...utaumia sana...
 
5997
Acha ujin*";@$g mkuu achana nae, ushapata sababu nyingi za kumuacha, niamini ukimuoa atakusumbua sana, muache atapatawakwendana nae
 
Back
Top Bottom