Nahisi Dogo anataka kuniingiza mjini, ni kweli kuna fomu za kulipia elfu 40 ili ufanye mtihani wa QT?

Dogo nimemlipia hela ya usajili wa kufanya mtihani QT(form 4) NECTA, pamoja na kumlipia kituo cha kufanyia huo mtihani.

Ila sasa anasema kuna fomu za kujaza kwa ajili ya huo mtihani ambazo zinalipiwa kwa Tsh 40,000/=.

Hiki kitu sijawahi kukisikia nimepata mashaka, nimemwambia dogo aende kwenye kituo cha mtihani akapewe hiyo fomu aniletee nije niione ila kasema fomu zinajazwa huko huko na haziwezi kutoka nje.

Nikaamua kuulizia kwa mtu amesema hamna kitu kama hiki(fomu) na kasema nimedanganywa.

Naomba kuuliza tena hapa jukwaani, je hizo fomu za kulipia elfu 40 kwa wanafunzi wa QT ili waje wafanye mtihani, zipo? Au Dogo anataka kuniingiza mjini
ulichoshindwa ni nini kwenda kwenye hicho kituo kuulizia? Hebu kuwa mkuu usiwe kama dogo.
 
Wengi waliochangia mada hawakupita Qt, ni kweli kuna pesa ya usajili ambayo inaenda kulipiwa Benki, pesa ya usajili hulipwa kwenye account ya Necta, pesa ya kituo Cha mtihani hulipwa kwenye account ya kituo husika, Mara nyingi usajili huanza January mpaka March, ni vizuri kabla ya yote uende anaposoma ili ukajiridhishe
 
Kama umeshamlipia gharama ya kituo cha kufanyia mtihani hii kila kituo na bei yake vingine hadi 150k.
Pamoja na gharama inayopelekwa kwenye acc ya necta.Nenda ukaulize kuhusu hiyo 40k
Ila kama bado hujalipa ndugu mpatie huyo yanki hiyo pesa
 
vitu vingine tunaaamuaga kupotezea tu kama wazazi, mtotot hawez kukuomba hela ya kuhonga au kununua vocha, otherwise unataka akaibe, mpe ile mwambie siyo kweli nexttime atafute uongo mwingine!!
Huyu dogo akimaliza pepa atatakiwa arudi mkoani(nyumbani), nipo namuandalia safari na mahitaji mengine madogo madogo ila kama kaamua kujipatia hela kwa njia hii, hapana
 
40,nimetoa kilo 2+ leo hii kadai kesho wanaenda field lazima ilipwe..
Mi namgoja tu hapa alete risiti.
Vinginevyo ntajua nimkate vipi
Hawa madogo sijui wanadhamiria nini, starehe?
Binafsi sikuwahi kufanya mambo kama haya
 
Wengi waliochangia mada hawakupita Qt, ni kweli kuna pesa ya usajili ambayo inaenda kulipiwa Benki, pesa ya usajili hulipwa kwenye account ya Necta, pesa ya kituo Cha mtihani hulipwa kwenye account ya kituo husika, Mara nyingi usajili huanza January mpaka March, ni vizuri kabla ya yote uende anaposoma ili ukajiridhishe
Hayo yote ya usajili NECTA na malipo ya kituo kashafanya tangu March.
Kumbuka ili usajiliwe NECTA lazima uwe na kituo cha kufanyia mtihani, kwa hiyo malipo yanaanzia kulipia kituo ili apewe details za kituo ambazo atazitumia kujisajili NECTA kupitia POSTA.

Nyaraka zote anazo, ila nashangaa hii imetoka wapi ya kulipia tena ambapo ametoa taarifa juzi kati tu
 
Dogo nimemlipia hela ya usajili wa kufanya mtihani QT(form 4) NECTA, pamoja na kumlipia kituo cha kufanyia huo mtihani.

Ila sasa anasema kuna fomu za kujaza kwa ajili ya huo mtihani ambazo zinalipiwa kwa Tsh 40,000/=.

Hiki kitu sijawahi kukisikia nimepata mashaka, nimemwambia dogo aende kwenye kituo cha mtihani akapewe hiyo fomu aniletee nije niione ila kasema fomu zinajazwa huko huko na haziwezi kutoka nje.

Nikaamua kuulizia kwa mtu amesema hamna kitu kama hiki(fomu) na kasema nimedanganywa.

Naomba kuuliza tena hapa jukwaani, je hizo fomu za kulipia elfu 40 kwa wanafunzi wa QT ili waje wafanye mtihani, zipo? Au Dogo anataka kuniingiza mjini

Ubahili ndo unamfanya Dogo atafute njia za mbadala, msaidie Dogo, mpe tu, 40,000/- mpaka mswali huku Hamu forums!
 
Yupo sahihi tena vituo vingi ni elfu 50 huyo hata walau wamempunguzia,

Mpatie pesa kijana akasome kwa amani, ndio wa kukuuguza hao ukipata stroke na mke akakukimbia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom