NAGU: Sikushinda uchaguzi kwa fedha za Lowassa

Wambugani

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2007
Posts
1,757
Reaction score
277
Nagu amlipua Sumaye

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk. Mary Nagu, amevunja ukimya na kuzungumza kwa mara ya kwanza akisema hakupewa fedha na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, wala hakutumia rushwa mtandao kumuangusha Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye.

Kauli hiyo ya Nagu imekuja wakati ambapo Sumaye anadai kuwa rushwa ya kimtandao iliyokigubika Chama Cha Mapinduzi (CCM), ndiyo iliyomwangusha wilayani Hanang wakati akipambana na Dk. Nagu katika uchaguzi kuwania ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Taifa.

Wakati kukiwa na taarifa kuwa kuna baadhi ya wanachama wameandika barua kwa Katibu Mkuu wa CCM, kutaka ushindi wake utenguliwe, Nagu akizungumza na gazeti hili jana katika mahojiano maalumu, alisema kuwa anamshangaa Sumaye kudai aliangushwa kwa rushwa.

Alisema hakupewa fedha na aliyekuwa Waziri Mkuu, Lowassa, kwa ajili ya kumuangusha Sumaye na kwamba wananchi wa Hanang walimchagua kwa ridhaa yao.

Nagu alisema wanaosema kuwa alitumia rushwa, wana mfumo dume kwa sababu hawaamini kama mwanamke anaweza kushinda bila rushwa.

"Huu ni mfumo dume, usiotambua uwezo wa mama unatawala. Tushirikiane kuutokomeza," alisema Dk. Nagu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hanang.

Dk. Nagu ambaye hakutaka kuzungumzia suala hilo kwa undani kwa sababu Sumaye alikuwa bosi wake wakati akiwa Waziri Mkuu, alisema alinyanyasika sana wakati wa uchaguzi huo wa Hanang.

Alisema ilifika mahala watu aliokuwa akipingana nao walikuwa wakisema wakati wa mwanamke kuchukua nafasi hiyo umekwisha na kwamba amuachie mwanaume aongoze.

Alisisitiza kuwa, yeye kwa upande wake hakutoa rushwa wala hakufadhiliwa na mtu yeyote na kuwashutumu wapinzani wake kuwa ndio waliotumia rushwa kuhakikisha wanamuangusha, lakini walishindwa.

"Kama nilitoa rushwa, TAKUKURU wapo, kwanza sikuona umuhimu wake kwa sababu ukitoa rushwa wale waliokuchagua wanakutazamaje?" alihoji Nagu.

Alikwenda mbali na kusema kuwa hata wananchi wake wa Hanang hawakufurahishwa na jinsi ambavyo alitendewa katika uchaguzi huo, na kwamba na wao wameamua kuchukua hatua ya kumuandikia barua Katibu Mkuu wa CCM.

Kauli hiyo ya Nagu imekuja ikiwa ni takribani mwezi mmoja tangu Sumaye atoe dukuduku lake, na kubainisha kuwa rushwa ya kimtandao, ndiyo iliyomwangusha wilayani Hanang.

Bila kumtaja Lowassa, huku akisisitiza kuwa hana uhasama naye, lakini kauli zake zilionekana wazi kumlenga Waziri Mkuu huyo wa zamani.

Sumaye ambaye mara baada ya kubwagwa na Dk. Nagu alikutana na wanahabari kuelezea mwenendo mzima wa uchaguzi huo na hatma ya CCM, alisema uchaguzi huo uligubikwa na matumizi makubwa ya rushwa, vitisho, uharamia wa kuhamisha wapigakura usiku na ukiukwaji mwingine mkubwa wa uchaguzi.

Alisema hajakata rufaa kupinga matokeo hayo wala kupeleka malalamiko katika chama chake kwa sababu yaliyokuwa yakitendeka yalikuwa yanafahamika.

Akifafanua kuhusu vitendo vya rushwa ndani ya CCM, Sumaye alisema kuwa nchi nyingi hasa zenye demokrasia changa kama Tanzania zimeingia katika vurugu na kuhatarisha amani na utulivu nyakati za uchaguzi.

CHANZO: Tanzania Daima
 
Sasa umeshinda kwa pesa za nani? RUSHWA haijalishi imetoka kwa nani ndiyo iwe mbaya. Akitoa mwana mama ni TAKRIMA, ila akitoa mwanaume ni MFUMO DUME. Kweli tumeshafika pabaya.
 
Sio kila jambo linapaswa kujibiwa.
Huyu mama hakua na sababu ya kujibu hili.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Je uhusiano wake na waziri mkuu mstaafu Sumaye ulikuwa ni mtu na bosi wake pekee, au kabila moja, mkoa
mmoja au kuna zaidi??? ni nini kimetokea? tumebakia midomo wazi. Kweli never trust a ....
 
Nagu amlipua Sumaye

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk. Mary Nagu, amevunja ukimya na kuzungumza kwa mara ya kwanza akisema hakupewa fedha na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, wala hakutumia rushwa mtandao kumuangusha Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye.

Kauli hiyo ya Nagu imekuja wakati ambapo Sumaye anadai kuwa rushwa ya kimtandao iliyokigubika Chama Cha Mapinduzi (CCM), ndiyo iliyomwangusha wilayani Hanang wakati akipambana na Dk. Nagu katika uchaguzi kuwania ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Taifa.

Wakati kukiwa na taarifa kuwa kuna baadhi ya wanachama wameandika barua kwa Katibu Mkuu wa CCM, kutaka ushindi wake utenguliwe, Nagu akizungumza na gazeti hili jana katika mahojiano maalumu, alisema kuwa anamshangaa Sumaye kudai aliangushwa kwa rushwa.

Alisema hakupewa fedha na aliyekuwa Waziri Mkuu, Lowassa, kwa ajili ya kumuangusha Sumaye na kwamba wananchi wa Hanang walimchagua kwa ridhaa yao.

Nagu alisema wanaosema kuwa alitumia rushwa, wana mfumo dume kwa sababu hawaamini kama mwanamke anaweza kushinda bila rushwa.

“Huu ni mfumo dume, usiotambua uwezo wa mama unatawala. Tushirikiane kuutokomeza,” alisema Dk. Nagu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hanang.

Dk. Nagu ambaye hakutaka kuzungumzia suala hilo kwa undani kwa sababu Sumaye alikuwa bosi wake wakati akiwa Waziri Mkuu, alisema alinyanyasika sana wakati wa uchaguzi huo wa Hanang.

Alisema ilifika mahala watu aliokuwa akipingana nao walikuwa wakisema wakati wa mwanamke kuchukua nafasi hiyo umekwisha na kwamba amuachie mwanaume aongoze.

Alisisitiza kuwa, yeye kwa upande wake hakutoa rushwa wala hakufadhiliwa na mtu yeyote na kuwashutumu wapinzani wake kuwa ndio waliotumia rushwa kuhakikisha wanamuangusha, lakini walishindwa.

“Kama nilitoa rushwa, TAKUKURU wapo, kwanza sikuona umuhimu wake kwa sababu ukitoa rushwa wale waliokuchagua wanakutazamaje?” alihoji Nagu.

Alikwenda mbali na kusema kuwa hata wananchi wake wa Hanang hawakufurahishwa na jinsi ambavyo alitendewa katika uchaguzi huo, na kwamba na wao wameamua kuchukua hatua ya kumuandikia barua Katibu Mkuu wa CCM.

Kauli hiyo ya Nagu imekuja ikiwa ni takribani mwezi mmoja tangu Sumaye atoe dukuduku lake, na kubainisha kuwa rushwa ya kimtandao, ndiyo iliyomwangusha wilayani Hanang.

Bila kumtaja Lowassa, huku akisisitiza kuwa hana uhasama naye, lakini kauli zake zilionekana wazi kumlenga Waziri Mkuu huyo wa zamani.

Sumaye ambaye mara baada ya kubwagwa na Dk. Nagu alikutana na wanahabari kuelezea mwenendo mzima wa uchaguzi huo na hatma ya CCM, alisema uchaguzi huo uligubikwa na matumizi makubwa ya rushwa, vitisho, uharamia wa kuhamisha wapigakura usiku na ukiukwaji mwingine mkubwa wa uchaguzi.

Alisema hajakata rufaa kupinga matokeo hayo wala kupeleka malalamiko katika chama chake kwa sababu yaliyokuwa yakitendeka yalikuwa yanafahamika.

Akifafanua kuhusu vitendo vya rushwa ndani ya CCM, Sumaye alisema kuwa nchi nyingi hasa zenye demokrasia changa kama Tanzania zimeingia katika vurugu na kuhatarisha amani na utulivu nyakati za uchaguzi.

CHANZO: Tanzania Daima

Amejikanyaga sana huyu mama
 
“Huu ni mfumo dume, usiotambua uwezo wa mama unatawala. Tushirikiane kuutokomeza,” alisema Dk. Nagu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hanang.

Akitoa mwana mama ni TAKRIMA, ila akitoa mwanaume ni MFUMO DUME. Kweli tumeshafika pabaya.

Hii ni sawa na Hoja zile zile za sasa nizamu ya mwanamke kuwa spika wa bunge (Mh. Makinda dhidi Mh. Samwel Sitta). Na hii ni hatari sana kuchagua mtu kushika madaraka kwa ubaguzi wa kijinsia.

Kiongozi anatakiwa apatikane kwa kuzingatia uwezo wake wa kiuongozi, busara, hekima, utu, nidhamu, kujiheshimu na mengine kama hayo. Hizi habari za kuchuguana kwa fikiria masuala ya mfumo dume hayana tofauti na yale kuchaguana kwa kuangalia mchaguliwa anatoka dini gani (mfumo kristo au uislamu), kabila gani (mfumo kabila), kanda gani (mfumo kanda), na sasa nadhani na kutakuwa na "mfumo rika". Mifumo yote hii yote kuifuata na sawa na kutenda dhambi kubwa kuliko dhambi zote zilizoainishwa katika vitabu vyote vya dini zilizopo duniani ambayo italitumbukiza taifa hili motoni.

Binafsi mfumo unaotakiwa kufuatwa bila ya kuwa na wasiwasi wowote ni mfumo "uwezo wa kiuongozi na uzalendo wa kutoka moyoni na mengine kama haya"
 
Hana lolote bila rushwa CCM huchaguliwi asitudanganye hapa!
 
hahahahahahahaha!nagu !!!!huyu mama anachanganyikiwa,sasa anataka kuwaambia watanzania kashinda kwa pesa zake mwenyewe na sio za lowasa?shuda ya wamama wa ccm hakuna anayeweza kusimama mwenyewe na akafanikisha jambo,mpaka wawezeshwe.lowasa kashatengenezo safu,subirini tu mtaona,.
 
Mama Nagu mbona hasemi Lowassa alifuata nini Katesh wakati wa uchaguzi kwani alikuwa kapiga kambi pale Summit Hotel Katesh?

Kanuni ya 'Natural Justice" inasema mtu hawezi kujihukumu. (Nobody can be judge on his/her own cause).
 
sumaye alzdiwa mbinu kaua soo...kuwa katesh kwan katesh wanaenda kwa pasport au visa...siasa majitaka mtu akshndwa basi akajpange upya..tatzo walshazoea zdumu fkra za mwenyekti..
 
hivi hawa CCM wanapataGa muda kufikiria namna ya maana ya kuendeleza nchi?

Maana kusema CCM inanuka rushwa hakutoshelezi madudu yanayoendelea huko CCM
 
Hakushinda kwa fedha za Lowasa bali kwa fedha zake! So ukishinda na za Lowasa ni rushwa,zako si rushwa! jamani huko CCM kuna Mambo ya ajabu sana!
 
Back
Top Bottom