Nagombea urais 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nagombea urais 2015

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mbunge wa CCM, Dec 18, 2009.

 1. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baada ya kusoma mada ya "baraza dogo la mawaziri" iliyowekwa leo na ndugu john mnyika wa chadema, nimeshawishika nami nieleze japo kidogo juu ya dhamira yangu ya kugombea urasis wa JMT katiaka uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 (kama nitajaaliwa kuuona).

  Kilichonilazimisha nitoboe siri hii, ni hili baraza lenyewe alilopendekeza. japo anapunguza wizara na kufafanua mabadiliko ya hapa na pale kuhusu mpangilio wa shuguli za serikali na baraza la mawaziri, bado inaonekana anatumia muundo huu huu tulionao sasa na si ajabu serkali ya namna hiyo ikawa na mabadilko ya mara kwa mara ya baraza la mawaziri kwa lengo la kuliimarisha!

  kwa kifupi, endapo nitashinda uchaguzi 2015, baraza langu litakuwa tofauti sana. kwanza sitakuwa na functional minsters, bali strategic ministers. na hawa watakuwa responsible na mikakati (strategies) waliyokabidhiwa kisimamia na watawajibika kwa mafanikio au kushindwa kwa mikakati husika. watakuwa wakipimwa na wadau wote mara moja katiak kila kipindi cha miezi 6. Utaratibu wa wazi utawekwa

  mikakati enyewe itakayokuwa na mawaziri ni hii fuatayo
  1. mkakati wa maendeleo ya jamii na utamaduni (elimu na maendeleo ya ujuzi, michezo, lugha, sanaa, ustawi wa jamii, afya)
  2. mkakati wa siasa na utawala wa kiraia (sheria, utawala bora, tamisemi, bunge)
  3. mkakati wa diplomasia ulinzi na usalama (mambo ya nje, afrika mashariki, ulinzi, usalama wa taifa, mambo ya ndani)
  4. mkakati wa maendeleo ya utumishi (kazi, ajira, utumishi wa umma, hifadhi ya jamii)
  5. mkakati wa maendeleo ya uchumi (fedha, uwekezaji, viwanda, biashara, masoko, mipango, utalii, ushirika)
  6. mkakati wa uthabiti wa ndani (maendeleo ya kilimo, uvuvi, mifugo, utalii, maendeleo ya misitu na mazingira)
  7. mkakati wa maendelo ya rasilimali za kiuchumi (maendeleo ya nishati, madini, maji, miundombinu)
  8. mkakati wa maendelo ya rasilimali za huduma na ustawi wa taifa (maendeleo ya ardhi na hazina za asili, mipango-miji, makazi, maji)

  Makamu wa rais atakuwa pia waziri asiye na wizara maalum na kama chief of government organization, atahusika na mkakati wa ufanisi wa muundo wa serikali (oganaizesheni ya serikali) na atafanya kazi kwa karibu na (na akiwa chini) ya rais

  kila wizaya ya mkakati itakuwa na naibu waziri mmoja, na makatibu wakuu zaidi ya mmoja kutegemeana na mahitaji. Kila katibu mkuu atakuwa ni mtaalamu wa eneo husika na atateuliwa baada ya kupambamishwa na wengine katika usaili huru, au kama rais rais atamuhitaji kwa sababu maalum. Katibu muu atatoa hesabu ya utumishi wake kwa rais kila baada ya miezi sita na utaratibu unaoruhusi assessment ya wadau utawekwa.

  Wakuu wa mikoa watakuwa na hadhi sawa na mawaziri ila tofauti na mwawziri wanaohusika na mkakati mahususi, wao watahusika na utekelezaji wa kila mkakati kwenye maeneo yao wakishirikiana na makatibu wakuu, wakuu wa wilaya. Nao watapimwa kila baada ya miezi sita. Waziri mkuu atasimamia hili na Waziri wa mkakati wa siasa na utawala wa kiraia atahusika hapa kama coordinator tu.

  Uteuzi wa wakurugenzi wa maendeleo wa wilaya utaidhinishwa na waziri mkuu baada ya mchakato wa uteuzi utakaofanywa wilayani kwa kusimamaiwa na kamati ya maendeleo ya wilaya, lakini watawajibika kwa kamati za maendeleo za wilaya na zitapewa uwezo wa kuwawajibisha kama haziridhiki na ufanisi wa wakurugenzi hao.
  Mkuu wa wilaya takuwa kiongozi wa jumla wa wilaya akiwa na wajibu kamili chini ya mkuu wa mkoa kuhusu utekelezaji wa mikakati ya maendeleo katika wilaya yake. Anaweza kuwajibishwa na mkuu wa mkoa baada ya kupata idhini ya waziri mkuu.

  Japo kwa ufupi, nadhani haya yanatoa picha inyojadilika, tuombe Mungu.
   
Loading...