Nafsi ni nini

Noswerd malila

Senior Member
Jan 12, 2014
143
75
Habari ya asubuhi wakuu natumaini muwazima wa afya kwa wale ambao ni tofauti napenda kuwapa moyo mtakua vyema na kurudi ktk kusukuma gurudumu la maendeleo

Acha niende moja kwa moja katika swali langu nilouliza wajuzi wa mambo naomba kuuliza

1. Nafsi nini?
2. Je Nafsi ktk mwili huishi ndani ya mwili au nje ya mwili?
3. Je Nafsi huwezi kuumizwa na kupata maumivu kama wengi wasemavyo nafsi umeumia sana?
 
Nafsi "ni wewe usiyeonekana" na ambaye unamiliki kila kitu cha "wewe unayeonekana" ikiwa ni pamoja na roho yako, ambayo ni pumzi ya uhai. Umbo lako kwa ujumla wake pamoja na roho yako vinamilikiwa na nafsi. Kwa mfano huwa wakati mwingine unasema, kichwa changu kinauma, mkono wangu, mguu wangu, ukiwa unamaanisha kuwa wewe siyo kichwa, wala mguu, wala mkono, isipokuwa wewe ni kiumbe unayemiliki vyote hivyo kwa ujumla wake, na mmiliki huyo ndiyo hiyo nafsi yako!
 
Nafs Ni wew
Upo jf sahzi
Nakubaliana na ninyi kuwa nafsi ni WEWE. Lakini mjue kuwa roho sio sehemu ya nafsi. Roho ni pumzi ya Mungu ndani ya mwanadamu. Mwanadamu ana roho, nafsi na mwili. Ukifa nafsi yako huendelea kuishi katika ulimwengu usioonekana, roho yako hurudi kwa aliyeitoa, Mungu na mwili wako hurudi udongoni ulikotoka. Roho humfanya binadamu kuwa kiumbe wa ajabu sana na mwenye nguvu nyingi. Ila kwa bahati mbaya mwanadamu hatumii sana uwezo wa roho yake na hivyo kuonekana kiumbe dhaifu.

Kuna ushahidi kwamba nafsi ya mwanadamu ipo kila mahali katika mwili ila zaidi sehemu ya juu ya mwili na hasa kichwani.

Nafsi huweza kuumia na kuhangaika katika mateso. Hii hutokea hasa nafsi inapokuwa imetengana na mwili na kwenda katika mazingira ambayo sio mazuri kwa nafsi hiyo mfano Jehanam. Hapa ni mahali pabaya sana kwa nafsi za watu. Lakini nafsi huweza kwenda Mbinguni ambapo ni pazuri sana kwa ajili ya nafsi.
 
Kuna Mwili, Nafsi na Roho. Nafsi inamaana kwamba elimu, kazi, kitu ulichokuwa nacho au ulichobeba nk. Hivi vyote vipo kwenye Nafsi.
 
Back
Top Bottom