Nafikiria kuuza hati miliki ya maisha yangu ili nifurahiie maisha ningali hai

incredible terminator

JF-Expert Member
Aug 1, 2016
2,229
3,525
Habari wakuu,

Nawasalimu kwa jina la mungu wetu sote anaetupa uhai pasipokubagua dini na imani.

Kwanza kabisa niseme tu wazi kuwa wazo hili sijalipata kwa kushawishiwa au kushinikizwa na mtu, shida, au dhiki kama wengine wengi wanavyoshinikizwa na njaa, shida na dhiki, Mimi hapa naandika huu ujumbe nikiwa nimeshiba vizuri na utimamu wa akili.

Wazo hili nimelifikiria kwa kina na kwa mda mrefu na haya ndio majibu nilioyopata.

01. Kwanza kabisa kifo hakiepukiki na hakikwepeki, kwa njia yoyote ile lazima nitakufa tu iwe ni kwa kuwahi au kuchelewa ila kufikia 2070 huko sitakuwepo na kama nitakuwepo ndio nitakuwa naelekea mwisho, mwishoni.

02. Sijawahi kupata ushuhuda wa aliekufa na kurudi duniani kutushuhudia haya tunayoambiwa kuwa tukifa kuna adhabu kali, na kama kuna maisha baada ya kifo yalitupasa tuwaachie wafu wenyewe sio suala letu sisi tulio hai kuwawazia wafu na maisha yao.

03.Ulichonacho mda huo ndio chako na ndicho kinachoweza kukufaidisha na kukusaidia, ukikipoteza pasipokukusaidia kwa mda huo majuto yake na maumivu yake hayasimuliki.

Kwa mantiki hiyo basi najifungua minyororo ya ujinga na uzuzu wa kujisahaurisha kuhusu kifo.
Naamini kufa nitakufa tu iwe kwa kuchelewa au kwa kuwahi ila nitakufa tu nipende, nisipende kifo kipo tu.

Na ikiwa kifo kipo tu na hakiepukiki ni bora nipate changu mapema, nipate pesa niile, nienjoy, nitese, nifurahie maisha na niheshimiwe, niyafurahie matunda ya maisha yangu, nile matunda ya nafsi yangu nikiwa hai, kuliko kuliko kukaa na nafsi ambayo ninajua mda wowote nitaipoteza pasipo manufaa yoyote, wala mimi kuifaidi. Ikiwa adhabu ya kabri ni moja kama maandiko yanavyosema sioni haja ya kufa, nifukiwe, nitelekezwe makaburini niteseke na upweke huko, ile hali pia Duniani sijapata furaha, yaani nikubari kupoteza vyote duniani niteseke na baada ya kifo niteseke no,

Siwezi kupoteza vyote, Ninao ushahidi wa wawatu ambao walitambua hili mapema na wakakubali kuuza nafsi zao, (hati miliki za maisha yao) akina GINIMBI, MAIKO JACKSON, 2FACE, DJ ARAFAT, DON IVAN, STEVEN KANUMBA na wengineo, Licha ya kuondoka kwao bado majina yao na heshma zao zinaishi na bado jamii inawakumbuka, walijizolea umaarufu na walifaidi uhai wao, na licha kufaidi uhai wao ila hadi leo tunawakumbuka na kuheshmu uwepo wao,

Tofauti kabisa na Bodaboda aliejichanganya barabarani akikimbilia abiria wa Buku akaingia 18 za Fuso, akapelekewa moto akapasuka kichwa akajinyoosha barabarani katikati, akang`ata ulimi na kukodoa macho akafa

Polisi wakifuata mwili wake wanaupakia kwenye Defender chali, ikawashwa kibati kwenda mortualy wakifika mwili ulishageuka umelala kifudifudi na majeraha mengine yaliyotokana na mwendo yameongezeka, Mwili wa maskini hauheshimiwi ndio maana hata kwenye misiba ya kimaskini marehem hutumwa apeleke salamu kwa wenzie waliokufa, hata vilio vya kifo cha masikini ni fujo tupu

Ndugu umasikini ni laana, Umasikini ni ujinga, Umaskini ni ukosefu wa Fikra na hata hao wanaojiita wafia Dini ni laana za umasikini zinawaandama wanatafta pakuponea, Finally Ndugu tutafte pesa zikishindikana uza nafsi usikubali kufa maskini.
 
Uza nafsi na sisi tuige, na utuambie unauza kwa bei gani
hebu ongoza maandamano kama Raila tukuone basi
Watu wanaogopa maisha et wanasema unaishi kwa masharti, nani kawambia kuna masharti ya mganga magumu kuliko masharti ya Dhiki?

Yaani mwanaume timamu uamke asubuhi uvae suruali imechanika mataqoni uende sokoni ukae front mbele za watu, uanze kubebea wanaume wenzio mizigo, wake kwa waume wanakupa jero, kisha unarud hom wife hajaoga hana viatu nguo ya ndani imechanika katikati, watoto hawana viatu shule wanazosoma ni st kayumba, baba mwenyenyumba mwisho wa mwezi yuko mlangoni, alafu unasema kuna shart gumu kwa mganga zaidi ya hili????
 
Umaskini ni hatari,

Na ndio maana, kila mmoja anapaswa kuukimbia na kupambana nao kwa kufanya kila linalowezekana kihalali.

LAKINI SI KUUZA NAFSI ndugu, Wazo ilo ulilonalo jaribu kuliondoa and see the beauty of this life through hustling.
 
Umaskini ni hatari,

Na ndio maana, kila mmoja anapaswa kuukimbia na kupambana nao kwa kufanya kila linalowezekana kihalali.

LAKINI SI KUUZA NAFSI ndugu, Wazo ilo ulilonalo jaribu kuliondoa and see the beauty of this life through hustling.
nakujibu ndugu maisha ya mtanzania wa kawaida ninayo niga tembea bila kutumia mguu nina ishi sidaiwi kodi, ila kuhusu maisha yangu i will never die free,.. sihitaji nife bure,,,, maisha ninayoyaishi bado najiona niko nyuma na watu flan japokuwa nakutana na comment za watu wanaotaman hata hii nafasi niliyonayo,,, ila ikiwa mimi nina uhakika wa kula na kulala na usafiri and still najidharau na napamabana kujiona am nothing how kuhusu hawa wasiokuwa hata na uhakika wa kula wala kulala wanatoa wapi usingizi wa kusinzia ile hali njia zipo nyingi za kutafta pesa ukiachana na kuiba ?
 
Nimeacha kusoma tu hapo uliposema una ushahidi wa kina kanumba, Michael Jackson, don Ivan kuuza nafsi zao

Una ushahidi gani zaidi ya story za vijiweni?
 
Hivi unajua kuwa kuuza nafsi (selling your soul) ni pamoja na baada ya kufa hapa duniani? Maisha ya hapa duniani ni kivuli tu cha maisha yajayo, hivyo ukiuza nafsi yako hapa duniani ujiuza forever. Na maana ya kumilikiwa na shetani ni kuwa chini ya utumwa wake ambao hakuna mfano wa mateso na fedheha kama hiyo. Muuzie Yesu Kristo maisha yako.
 
Hizi ni fikra za kimaskini.
Ungekua na hela usinge waza ujinga wa ainahii.
Kwahiyo nakushauri tafuta pesa, endelea kupambana huku ukimuomba Mungu wako unae muamini akupe afya njema
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom