Ni kwambie kitu kimoja tu kumbadilisha tabia mtu mzima ni ngumu na ukifanikiwa basi ni baadhi ya vitu kama sio kimoja basi viwili,
Kwa swala lako yaani nyie ni( incompatible)you have different ideologies. siwezi nikamjudge sana kwa sababu wewe unachokiona kibaya yeye ndo kinampa furaha maana yake unapotaka abadilike basi unapoteza furaha yake
Mfano umekuta mtu anakunywa pombe unataka aache,kama kwake ni kiburudisho usimfosi,unataka asokunywa pombe mtafte asokunywa sio umtafte anayekunywa utake kumbadilisha nikuharibiana starehe, anapenda western culture wewe hupend vyema mtafte asopenda
Ushauri
Tafta mtu mwenye misimamo inayokaribiana na yako,mnaeza msiendane kila sekta lakin mkawa mnakaribiana(no one is perfect) kiufupi kesi yako sio kubwa kuamua maana iko wazi sema kinachohitajika ni maamuzi ya kiume
Kama ulichoandika ni sahihi, ukweli ni kwamba hamna compatibility.Unamaanisha nini hapa Mkuu?
kama yote uliyoandika hapa mi sahihi,BASI HUYO MTU HAFAI KUOLEWA KWA SASA,NA NAKUSHAURI HUYO USIOE;Habari zenu wana jukwaa
Poleni na majukumu na pilika pilika za wiki nzima
Nina swala moja linalonisumbua sana kichwa kwa sasa, na nimekuja kwenu kuomba ushauri wa jambo hili.
Mimi ni mwanaume, nina miaka 28 kwa sasa. Nimekuwa kwenye mahusiano ya muda mrefu kidogo wa takribani miaka nane na mpenzi wangu lakini naona mahusiano yenu yanafikia ukingoni.
Namshukuru Mungu nimefanikiwa kupata malezi ya wazazi wote wawili, lakini mwenzangu hajabahatika kupata malezi ya baba, namaanisha mpaka leo amebahatika kulelewa na Mama tu ingawa Baba yake yu mzima mpaka leo na kwa sababu ya kulelewa na Mama tu naona amelishwa sumu ya kumchukia mzazi wake wa kiume.
Mpenzi wangu huyu kwa sasa yupo chuo, ila mimi nipo mtaani nna ajira ambayo ukweli ni kwamba ndo chanzo changu cha kipato kinachonifanya niendelee kuishi hapa Dar Es Salaam.
Toka tumeanza mahusiano, nilikua natamani sana nipate wasaa wa kuishi nae kwa muda kidogo kabla sijamuoa ili nipate kumfahamu mwenza wangu kiundani na Alhamdullilah nilipata wasaa wa kuishi nae mwaka jana kwa takribani miezi mitano nyumbani kwangu na nikapata kumfahamu kiundani kidogo.
Ukweli ni kwamba, Wazazi wangu ni watu waliokulia vijijini kabla ya kuja mjini ukubwani kutafuta Maisha na hivyo. Wamenilea katika maadili mazuri ya kiafrika katika nyanja zote za Maisha na namshukuru Mungu kwa malezi yao.
Mwenzangu, Mama yake ni Mcha Mungu sana ila yeye yupo tofauti kidogo na tabia za Mama yake. Akiwa mazingira ya kwao, Mama ndo huwa anamhimiza kwenda Kanisani lakini anapoondoka mazingira ya Nyumbani huwa anaacha kabisa kwenda huko Ibadani na kama akienda ni Mara mojamoja tu. Mwenzangu huyu amekumbatia sana mila za Magharibi kama kuvaa sana suruali za kubana mpaka anakosa nguo za kwenda kanisani, wallpapers zake kwenye simu ni picha za nusu utupu kwa sana, akikaa kwa TV vipindi anavyoangaliaga ni dhahama tupu (Keeping up with Kardashians) mpaka unajiuliza anajifunza nini huku, Hapendi kabisa kusikia mazingira ya vijijini na ukitaka mkosane mwambie unapenda kuishi huko, atakwambia we kaishi huko mm siwezi kama Kuwasiliana WhatsApp ipo. Duuh! Hivi huyu anafaa kuwa mke kweli na anaweza kuishi nadhiri ya kuishi pamoja katika shida na Raha?
Ana hulka ya uvivu, kila kazi atataka mfanye wote akiamini haki sawa ni kazi zote za nyumbani mfanye wote, Ni mtu anayependa sana mikorogo ambayo kimsingi inapoteza rangi yake nzuri nyeusi ya asili, Nimeshajaribu kumkanya sana kuhusu hili na hata kutupa baadhi ya vipodozi vyake bila mafanikio, Marafiki zake wanaomzunguka ni walevi, wadangaji na mabinti wenye tabia chafu nyingi tuu, Na hili pia nimejaribu sana kumkanya ila huishia kusema wale ni marafiki tu na yeye ni mtu mzima anayejua nini anafanya hivyo hawawezi kumbadili tabia kwa namna yoyote ile.
Anapenda sana kula vyakula vya kisasa kama Chipsi na Ice Cream na sio vyakula vya kiafrika. Ugali hapendi kula na akila ugali ni lazima anywe na maziwa mgando la sivyo hataki kusikia ugali. Uvivu wake unanifanyaga nimuulize, " Hivi mama kwa uvivu wako huu, utaweza kuingia Leba, kujifungua kwa njia ya kawaida na kutoka salama kweli", kuamka mapema kwake ni ndoto, kwenye mazingira yake ya chuo huko hata nguo zake binafsi anafuliwa, Sasa huyu ni mke au Slay Queen?
Nimeahidi kumuoa akimaliza chuo, ila kila nikiwaza tabia zake naona hafit kuwa mke na Mama Bora wa familia na kwa maana hiyo nafikiria kumuacha na kuanzisha mahusiano mengine. Je niko sahihi kwenye hilii?
Naombeni ushauri wenu katika hili tafadhali
Mengi nimeyajua siku za karibuni baada ya kuwa nae karibu MkuuMwanamke huyo uliwezaje kuishi nae miaka nane????kama hamuendani kiasi hicho
Maana kwa mtazamo wangu huyo hamkupaswa hata kudumu miezi 3...
Hao wanawake wa kizungu wana watu wake na kwa sisi tusiwaweza tunawafanya michepuko tu maisha yaende
Nashukuru kwa Ushauri wako nduguHuyo ni mwanamke mzuri,tatz anaakili za kichuo na utoto sana. Kifupi bado hayuko tyr kuwa mke na maisha ya ndoa,anaimagine maisha na ushamba wa kichuo. Nae yuko dilema blv me.
Kama unao muda mpe muda,kama huna tafuta mwingine wa kukufaa kwa wakati huu na wkt wote.
Wewe umejua maisha halisia,yeye bado anayaota maisha kwa namna yake kichwani.
[emoji120]Kama unaona atakusumbua huko mbeleni achana naye.
NotedNasisitiza hapa.
Mkuu sorry to say this ila kwa jibu hili nadhani hukuja kuomba ushauri ila ulikuja usikie kile ambacho ungependa kusikia kuhusu huyo she wako,maanake naona unaanza kutafuta vijisababu vya kutushawishi na sisi tuone good side yake licha ya kash kash zake ulizoziandikaSawa Mkuu
Nashukuru kwa ushauri
Ingawa ukweli ni kwamba bado nampenda for sure
Then despite of Mapungufu yake ila ni mvumilivu maana nilianza date nae nikiwa sina kitu mpaka leo ninapoona mwanga kidogo wa Maisha
mkuu sorry to say this,lakini naaminigi kabisa kuwa jambo baya Zaidi mtu analoweza kufanya ni kumpa mimba mwanamke anayeona kabisa anamsumbua sana kwa kuamini kuwa mtoto atamtuliza,yaani hii ni bonge la mistake,Huo ujana tu na kampani za kichuo chuo.
Mvumilie, akikua ataacha. Au ukitaka akue haraka mzalishe.
Asante kwa ushauri wako PendoMimi naaminigi tabia ni kama ngozi. Ni wachache sana hubadilikaga. Haya mambo ya magroup ni changamoto. Jumlisha ulevi ndo kabisa.
Si dhambi kunywa kbs ila anajicontrol vipi?
Lakini pia naona hamtawezana maana mko tofauti katika interests zenu. Nadhani muachane tu mapema
Nashukuru kwa ushauri G wa BluuMkuu sorry to say this ila kwa jibu hili nadhani hukuja kuomba ushauri ila ulikuja usikie kile ambacho ungependa kusikia kuhusu huyo she wako,maanake naona unaanza kutafuta vijisababu vya kutushawishi na sisi tuone good side yake licha ya kash kash zake ulizoziandika
Anyway mkuu akili kumkichwa,mambo ya wawili ni magumu sana kushauri
lakini tumia kichwa chako kufikiria vizuri kabisa weka hisia pembeni maanake wahenga walisema koseaa vyooooooote duaniani hapa ila usikosee kuoa/kuolewa maji utayaita mma,hakuna rangi utaacha kuona
heri nusu shari kuliko shari kamili
al the best mkuu
Asante kwa ushauri Ndugu MusaNimepapenda hapo anapotaka kila kazi ufanye nae hili jambo lako kupata maamzi sahihi ningumu sana mwenyewe umekiri unampenda kumwacha sio jambo jepesi wakati mwingine ubora wamwanamke hutegemea ubora wamwanaume nahisi hujasimama kwenye nafasi yako binafsi siamini mambo ya 50 /50 hizo asilimia baadhi yetu tunaangalia mtu yukoje unaweza kumpa hata zaidi yahizo kama anastahili lakini anaweza kukosa hata 20 kadri alivo kwakuwa huyo anakasoro jaribu kumwambia usiyoyataka hapo kwako ili achague mwenyewe umekiri nimvumilivu kilamtu anamapungufu yake hata wewe uko hivo kama unamwacha muache ila kusema watu waseme nn ufanye sidhani kama unaweza pata muongozo sahihi maana umeeleza machache sana hayatoshi kumhukumu mtu zaidi utapata kujua kwamba kwaaina yamkeo wengine wanafanyaje tusiwe wepesi kukata tamaa mengine niyamda tu jaribu kuonyesha msimamo usiyumbe ukweli kwahayo machache umesema hayaonyeshi mwelekeo mzuri