Nafasi za Kujitolea JKT 2014 Zimetoka

Nafasi za Kujitolea JKT 2014 Zimetoka

haya kwa wale vijana wazalendo na tuliokuwa na mapenzi mema na nchi na vyombo vyake vya ulinzi, nafasi za jkt kwa mwaka 2014 zipo hewani, tangazo kuta katika website yao yathibisha hilo. Kwa maelezo zaidi fuata link hii:-
vijana kujitolea

uuwiii umri umeendaaa dah nimeikosa hii
 
acha uvivu
acha uboya, vitu simple tu unalalama, kila kitu milawama. piga kimyaaaa kama hata link huioni. utaweza utambuzi kwa hisia wewe kweli KJT?

Uliza taratibu ujibiwe.
 
Watakaoenda maramba kamsalimien afande malesa na ndumbaro
Halafufu wawambie wanasalimiwa na nani? haya mkuu wamekupata, ni msisitizo kuonesha ya kwamba na wewe ulivaa zile karanga za kule haya big up!!!
 
Kwa maoni yangu binafsi kwa kigezo cha umri tyari nafasi sina,ingawa nilipenda pia kujiunga ila nawapongeza kwakuwa umri walioulenga ni sahihi kabisa,hawa watafundishika halafu pili watatumikia jesh mda mrefu!
 
link gani sasa hapo ya kuifuata? acha kufanya mambo kijingajinga!

Uvivu co mzuri, nyie ndio kwenye magazeti. huwa mnasoma heading tu then mnajifanya mna habari yooote, mbona kilakitu kikowazi? Sasa hapo mjingamjinga cjui nani
 
Haya kwa wale vijana wazalendo na tuliokuwa na mapenzi mema na nchi na vyombo vyake vya ulinzi, nafasi za JKT kwa mwaka 2014 zipo hewani, tangazo kuta katika website yao yathibisha hilo. kwa maelezo zaidi fuata link hii:-
vijana kujitolea

hyo link iko wapi au umetumwa au unatumika leta data za maana
 
Haya sasa kwa wale mliokuwa mnalilia oh usalama wa taifa,oh jinsi ya kujiunga. . . .chance hiyo hapo!! Hakikisha una vigezo vyote! Ndipo uende kujiandikisha na ikitokea umechaguliwa ndipo utapakapotakiwa kwenda kambini tayari kwa mafunzo ifikapo hapo mwezi march mwakani. Kwa wale wanaotaka kwenda JWTZ hiyo JKT ndio njia ya kuingilia. . .lakini mind you kwamba nchi yetu kila kitu ni kujuana....ukifika kambini baada ya miezi sita,majina ya watu(wenyewe wanaita BOG) watakaochaguliwa kwenda kupata mafunzo ya kijeshi(jwtz) kule Monduli. Kama una mtu unamjua anaweza akakufanyia mpango jina lako lika'appear ktk hyo list ya BOG! Lakini kama humjui mtu basi utaendelea kusugua makalio yako kwenye vumbi hadi itimie miaka miwili!! Na pia TISS huchagua watu wanaowahitaji hukohuko! Lakini mpaka mchujwe sana na mfuatiliwe sana!!
 
Zamani watu walikuwa wanajiunga moja kwa moja na mafunzo ya kijeshi(JWTZ) kule Monduli. Lakini kutokana na UGUMU wa mafunzo,watu wakawa wanatoroka,lakini ilikuwa ukitoroka ukikamatwa unapigwa risasi hadharani!! Hii kwa sasa haipo wameifuta na ili kuwafanya watu wasitoroke ndio maana wanataka lazima kwanza ukale vumbi jkt! Ujue namna ya kuruka kichurachura n.k ili mtu ukienda kwenye mazoezi yenyewe ya JWTZ(Wenyewe hutamka JEIWII) mtu asiyaone mafunzo magumu na asiweze kutoroka!
 
Msaada kidogo hivi vyeti mtu anaenda navyo kambini ama huwa vinakaguliwa wapi
 
hyo link iko wapi au umetumwa au unatumika leta data za maana
Boya mwingone huyu nae, hauoni maandishi ya "vijana kujitolea" yana rangi ya blue, ndo link hiyo ifuate, acha uzembe, jaribu kwanza kabla ya kulaumu.
 
Back
Top Bottom