Nafasi Za Kazi Katka Sekta Ya Afya


Griseofulvin

Griseofulvin

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2016
Messages
579
Likes
697
Points
180
Age
19
Griseofulvin

Griseofulvin

JF-Expert Member
Joined Sep 15, 2016
579 697 180
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO


TANGAZO LA KAZI
MRADI WA AJlRA YA DHARURA KATlKA SEKTA YA AFYA

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepata kibali cha mpango wa Ajira ya dharura kwa wataalamu wa "fani za Tabibu na Wauguzi. Mpango huu utaendeshwa chini ya mradi, kwa ufadhili wa fedha za Mfuko wa CDC, Award No. 5U2GGH001062-03 kwa muda wa miaka miwili.

Mradi utaajiri watumishi 192 ambao watapangiwa kufanya kazi kwenye halmashauri za wilaya 40 zenye uhaba mkubwa wa watumishi wa kutoa huduma za afya hasa kwa waathirika wenye virusi vya UKIMWI. Watumishi hawa watalipwa mishahara na stahiki nyingine kwa kufuata taratibu na kanuni za serikali. Watumishi wanaotakiwa ni Tabibu Wasaidizi (Clinical Assistant) 95 wenye ngazi ya Astashahada (Certificate in Clinical Medicine) na Wauguzi (Enrolled Nurses) 97 wenye ngazi ya Astashahada (Certificate in Nursing and midwifery).

Wizara inakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa watanzania wenye sifa zilizotajwa hapo juu, wawe na cheti cha kumaliza kidato cha nne pamoja na cheti cha taaluma aliyosomea kutoka kwenye chuo kinachotambuliwa na serikali. Barua ya maombi ioneshe wilaya ambayo mtumishi atapenda apangiwe kufanyakazi kati ya wilaya zilizopendekezwa hapo chini. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 14/12/2016.
Maombi yote yatumwe kwa:-

Katibu Mkuu
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
6 Samoral Machel Avenue,
S.L.P 9083,
11478, Dar es Salaam.
Tanzania
06/12/2016 Orodha ya Halmashauri za Wilaya na idadi Watumishi waliopendekezwa.
Na.
Mkoa
Halmashauri (Wilaya)
Tabibu Wasaidizi
Wauguzi Wasaidizi
Jumla

1
Arusha
1. Arusha CC
3
3
6

2
Dar es Salaam
2. Ilala MC
3
3
63. Kinondoni MC
3
3
64. Temeke MC
3
3
6

3
Dodoma
5. Dodoma MC
2
3
5

4
Geita
6. Geita DC
2
2
4

5
Iringa
7. Mufindi DC
3
3
68. Iringa MC
2
2
4

6
Kagera
9. Bukoba DC
3
3
610. Muleba DC
2
2
4

7
Kigoma
11. Kigoma Ujiji MC
2
3
5

8
Kilimanjaro
12. Moshi DC
3
3
6

9
Lindi
13. Lindi MC
2
2
4

10
Mara
14. Musoma MC
2
2
415. Rorya DC
2
2
4

11
Mbeya
16. Chunya DC
2
2
417. Kyela DC
3
3
618. Mbarali DC
2
2
419. Mbeya CC
3
3
620. Mbeya DC
3
3
621. Mbozi DC
2
2
422. Rungwe DC
2
2
4

12
Morogoro
23. Morogoro MC
3
3
6

13
Mwanza
24. Nyamagana MC
3
3
625. Sengerema DC
2
2
4

14
Njombe
26. Njombe TC
2
2
427. Wanging'ombe DC
2
2
4

15
Rukwa
28. Sumbawanga DC
2
2
429. Sumbawanga MC
2
2
4

16
Ruvuma
30. Mbinga DC
2
2
431. Songea MC
2
2
4

17
Shinyanga
32. Kahama DC
2
2
433. Kahama TC
3
3
634. Shinyanga MC
2
2
4

18
Tabora
35. Igunga DC
2
2
436. Nzega DC
2
2
437. Tabora MC
3
3
6

19
Tanga
38. Korogwe TC
2
2
439. Muheza DC
2
2
440. Tanga CC
3
3
6

Jumla
95
97
192
 
EMII

EMII

Member
Joined
Jul 11, 2016
Messages
71
Likes
34
Points
25
Age
28
EMII

EMII

Member
Joined Jul 11, 2016
71 34 25
Mkuu Tunaomba utupe trusted source coz hii inaonekana Kama editing ya kitu hii hapa chini

Said
WIZARA YA Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto,
imetangaza nafasi za ajira
192 kwa dharura, kwa
wataalamu wa fani mbili
za afya ambazo ni Tabibu
wasaidizi (Clinical
Assistant), nafasi 95 na
Wauguzi (Enrolled Nurses)
nafasi 97.
Kwa mujibu wa taarifa ya
Wizara hiyo iliyotolewa leo
Jumatatu Mei 23, 2016 na
kusainiwa na Katibu Mkuu
wa wizara, Iimeeleza kuwa
Wizara imeridhia mpango
wa ajira ya dharura ili
kukabiliana na uhaba
mkubwa wa wafanyakazi
katika sekta hii. “Mpango
huu utaendeshwa kwa
Fedha za mfuko wa CDC
(Centre for Disease Control)
Awards No.
5U2GGH001062-03 kwa
mwaka wa Fedha ulioanzia
Aprili 2016 kwa muda wa
miaka miwili. “Taarifa hiyo
imefafanua.
Watumishi watakaopata
ajira kupitia mradi huu
watapangiwa vituo vya
kazi vilivyoko katika
maeneo yenye uhaba
mkubwa wa watumishi
husika na ambayo
mazingira yake ni
magumu, taarifa hiyo
imeendelea kusema.
Taarifa hiyo ya wizara
imeendelea kufafanua
kuwa watumishi hawa
baada ya kumaliza
mkataba wao, wataingizwa
katika ajira za serikali
kulingana na upatikanaji
wa vibali vya ajira kwa
mwaka husika.
Wizara imewataka wote
wenye nia ya kuomba
watume maombi yao
yakiwa yameambatanishwa
navivuli vya vyeti vya
kumaliza kidato cha nne,
cheti cha taaluma pamoja
na leseni, (kwa wauguzi)
Taarifa kamili soma hapo
chini
JAMHURI YA MUUNGANO YA
TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO
YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA
WATOTO
AJIRA YA DHARURA KATIKA
SEKTA YA AFYA
UTANGULIZI
Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imeridhia mpango wa Ajira ya
dharura kwa wataalamu wa
fani mbili za afya. Mradi huu
umelenga kuchangia juhudi za
serikali katika kukabiliana na
uhaba mkubwa wa
wafanyakazi katika sekta hii.
Mpango huu utaendeshwa kwa
Fedha za mfuko wa CDC
(Centre for Disease Control)
Awards No. 5U2GGH001062-03
kwa mwaka wa Fedha ulioanzia
Aprili 2016 kwa muda wa
miaka miwili. Watumishi
watakaopata ajira kupitia mradi
huu wanakadiriwa kuwa 192 na
watapangiwa vituo vya kazi
vilivyoko katika maeneo yenye
uhaba mkubwa na ambayo
mazingira yake ni magumu.
Watumishi hawa baada ya
kumaliza mkataba wao,
wataingizwa katika ajira za
serikali kulingana na
upatikanaji wa vibali vya ajira
kwa mwaka husika. Watumishi
hawa ni kama ifuatavyo:
Tabibu Wasaidizi (Clinical
Assistant) 95 na Wauguzi
(Enrolled Nurses) 97. Maombi
yote yaambatanishwe kivuli cha
cheti cha kumaliza kidato cha
nne, cheti cha taaluma pamoja
na leseni (kwa wauguzi)
MSHAHARA NA MASILAHI
Mshahara (kwa kiwango cha
juu cha mshahara wa kila fani
husika)
Posho ya kujikimu ya siku saba
za mwanzo
Bima ya Afya ya asilimia 3%
Kiinua m,gongo cha asilimia
25% ya mishahara baada ya
miaka (2);
Malipo ya pango ya asilimia
30% ya mshahara
Nafasi ya kupatiwa mafunzo
elekezi.
Mwisho wa kupokea maombi ni
tarehe 06/06/2016, Maombi yote
yatumwe kwa njia ya posta:-
Katibu Mkuu
Wizara ya afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
S.L.P 9083
6 Samora Machel Avenue,
11478
Dar es salaam, Tanzania
 

Forum statistics

Threads 1,274,326
Members 490,664
Posts 30,508,486