Awe negative na majukumu ya kazi ni kupika na mengineyo kadili yatavyojitokeza. Sema unatafuta mke tu kwani shida iko wapi.
Hatuna Uhitaji wa haraka Kwani hata hivyo baadhi ya miundombinu inatarajiwa kukamilika December 2020.Nahisi utapeli kwenye hii kazi kwenye hiyo deadline , najiuliza maswali mengi sana nikizingatia aina ya kazi
Kama hamna uhitaji wa haraka kwa Nini mmetangaza sasahivi?Hatuna Uhitaji wa haraka Kwani hata hivyo baadhi ya miundombinu inatarajiwa kukamilika December 2020.
Wasiwasi ndio akili ila Mara nyingi jaribu kuwa na "mtizamo Chanya" (Positive mind) itakusaidia kufanikisha mipango yako kiurahisi.
Unataka House girl anayetoka chuo OohTerups Familly Wanayofuraha kutangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo
1) HOUSE MANAGER ( Nafasi 3)
SIFA ZA MWOMBAJI
-> Awe jinsia ya kike na awe Amesomea MAPISHI au.
Food&Beverage Production Au Hotel Management
na kuhitimu kwenye chuo kinachotambulika kwa.
ngazi ya Cheti au Diploma
-> Awe na Elimu ya Computer Basics
-> Awe na umri kati ya Miaka 18 hadi 21. Awe na urefu Usiopungia Sentimita 170 (5.5ft).
-> Asiwe mnene awe msafi kupitiliza na mwenye
kujipenda awe na afya njema (H.I.V negative)
-> Awe mwaminifu, mkweli mchangamfu na Mwenye hofu ya Mungu na asiwe na mtoto wa kumzaa
-> Awe mvumilivu na awe tayari kufanya kazi kwenye mazingira tofautitofauti na awe mwepesi kujifunza kitu kipya.
MAJUKUMU YA KAZI
-> Kuandaa chakula
-> Usafi wa ndani ya nyumba
-> Mengineyo (kwa kadri yatakavyojitokeza)
KITUO CHA KAZI
>>Kituo cha kazi ni Dar es Salaam ila awe tayari kwa mabadiliko endapo yatatokea
MALIPO / MSHAHARA
-> Malazi na chakula ni bure na kuhusu mshahara Ni Mazungumzo na pia itatengemea na Utendaji wa kazi
JINSI YA KUTUMA MAOMBI
>> Barua ya Maombi na Wasifu wako (CV) itumwe kwa njia ya E-mail nikota166@gmail.com
*Mwisho wa kutuma maombi Ni Tarehe 30/12/2020 *
HIV Ni ugonjwa kama magonjwa mengine na pia kuna kazi nyingi tu ambazo kunakuwa na vigezo vya afya mfano kazi zingine hazihitaji watu wasiokuwa na Pressure, Pumu au ulemavu wa mcho au usikivu na mengineyo kwahiyo siyo ubaguzi bali tu ni Nature ya kazi.Kama hamna uhitaji wa haraka kwa Nini mmetangaza sasahivi?
Wakati watu waliosomea hizo fani wapo wengi sana.
Halafu mnategemea huyo mtu aanze kazi lini.
Na mwisho kwa ushauri tu sheria zetu za kazi zinakataza kumbagua mtu kwa HIV status yake ulivyoiweka kwenye tangazo lako Ni kinyume cha sheria
Waajiri wanawapima watumishi watarajiwa ukimwi kiuficho wanaenda kuwapima afya Mambo ya uzito,kuona , homa ya ini na ukimwi majibu mfanyakazi hupewi mwajiri anayachukua na kuyafanyia kazi bila muomba kazi kujua mtu anaambiwa hajafauli usaili bila kuambiwa sababu kumbe Ni HIV positive, kiutaratibu huwezi kumwambia mtu umefeli usaili wa kazi kwa sababu wewe Ni hiv postive angalia usije shtakiwa
Sioni tatizo kama atalipwa vizuri na atatimiza majukumu yake ipasavyo.Unataka House girl anayetoka chuo Ooh
Asante kwa Maoni yako ila tu jua kwamba kwenye familia suala la Maadili ya watoto na afya ya familia kwa ujumla ni swala nyeti sana pia hiyo nafasi tunayowapa Wasaidizi wetu wa ndani ni nafasi nyeti na inahitaji iheshimiwe sana."asiwe mnene, awe msafi kupitiliza, hofu ya mungu, HIV negative, urefu cm..." Wewe nguzo1 acha mambo yako hayo bhana, washirikishe ndugu wakusaidie hilo hitaji la msingi kama huwezi kusort mwenyewe!