Nafasi ya balozi wa nyumba kumi

mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
6,379
3,826
kwa kuwa tuko kwenye mchakato wa maoni ya katiba mpya nimekuja na wazo la nafasi ya balozi wa nyumba kumi.
Nionavo mimi hii ni nafasi muhimu sana katika kuhamasiha, kuchochea na kusimamia maendeleo na hata usalama wa nchi.
Kwa hiyo nafasi hii iwe rasmi katika ngazi za utawala kiserikali.
Pili nafasi hii igombewe na vyama katika eneo husika
atakayechaguliwa achukuliwe kama kiongozi wa wanachi wote katika hilo eneo
Baada ya hapo serikali itawelimisha kuhusu taratibu za uongozi na usimamizi hasa katika kuhimiza ukusanyaji wa mapato ya serikali, usafi, ulinzi n.k. lazima wajumbe wajue sera za nchi za maendeleo kama mkukuta, dira ya 2025, mkurabita n.k kisha watumie uelewa huo kuhimiza maendeleo.
Ni imani yangu kuwa kwa njia hii nchi itasonga mbele kwa haraka sana. tujaribu kuhusisha mfumo wa utawala wa nchi na mfumo wa mwilili wa binadamu ambapo seli inaweza kufanananishwa na ngazi hii ya ubalozi... Naomba kuwasilisha wakuu.
 
mmh big no!nyumba kumi zipo ngapi nchi nzima?huo uchaguzi s itakua ni matumizi ya rasilimali za nchi bila sababu!serikali za mtaa inatosha mkuu.
 
Samahani nilikosea kusoma jina lako hapo juu nikalisoma hivi; MZIN.....
Hizi nafasi zinanifaa mpwa ila wangeziongeza ziwe mia moja
 
Back
Top Bottom