Wala msikate tamaa kila mtu ana siku yake. Sitasahau mimi nilipokuwa natafuta kazi, nikaitwa mahali nikaenda, ikafanyika interview, baada ya interview nikaelezwa kuwa ni mimi niliyepata nafasi hiyo, watanijulisha rasmi. Nikarudi nyumbani na matumaini makubwa baadaye kimya kama wiki mbili wakati walisema watanijulisha wiki hiyo hiyo, siku moja ghafla nilikutana na jamaa aliyekuwa kwenye panel akasema mmoja wa wenzengu alikuwa ni mtoto wa mjumbe wa bodi hivyo kapewa yeye, ingawa ukweli ni mimi niliyeshinda!. Frankly speaking niliumia sana hata hivyo nikaendelea kuomba sehemu nyingine na nilipata naweza sema mambo yanaenda vizuri tu.
Hivyo jipeni moyo endeleeni kuomba -pande zingine na kujikita katika ujasiria mali / kama kuna kazi ya kujitolea fanya mfano shule za kata hazina walimu kama ipo karibu na kwenu omba kufundisha utapata uzoefu fulani na pia kupata wasaha wa kuzungumza na watu wengine ambao waweza kukusaidia, pia kama waweza kujiajiri fanya hivyo tu.
Kila la kheri.