Nafasi la kazi za Wadadisi 560 - NBS

Robati

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
701
683
NAFASI ZA KAZI ZA WADADISI (NAFASI 560)

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)inawatangazia watanzania wenye sifa kuomba kazi ya muda ya udadisi au ukusanyaji wa takwimu nafasi 560 kwa ajili ya Utafiti wa Kilimo wa Mwaka 2016/17 utakaofanyika katika mikoa yote ya Tanzania Bara. Utafiti huu unahitaji mwombaji atoke kwenye mkoa anaoishi na awe tayari kufanya kazi kwa kipindi chote cha mwezi mmoja (1)

Waombaji wanatakiwa kuwa ni watanzania wenye sifa zifuatazo

a)sifa za msingi:-

i.Umri wa miaka 18 na kuendelea,
ii.Elimu ya kuanzia Kidato cha Nne,
iii.Mkazi kutoka katika Mkoa husika.

b)sifa za ziada:-

i.Elimu ya Cheti cha Ukusanyaji Takwimu rasmi kutoka Chuo cha Takwimu Mashariki
mwa Afrika (EASTC),
ii.Uzoefu wa kazi ya kukusanya takwimu katika tafiti mbali mbali zilizofan
ywa na NBS,
iii.Uzoefu wa kufanya Utafiti wa Kilimo wa Mwaka 2014/15.

Barua za maombi ziandikwe kwa mkono wa mwombaji akionesha anuani kamili na namba yake ya simu pamoja na kuambatisha nakala ya vyeti vyote vya elimu na mafunzo, wasifu wa mwombaji (CV). Barua ya maombi ya kazi itumwe kwenye Ofisi ya NBS ya Mkoa ambako unaishi. Maombi yanatakiwa yatumwe kabla ya tarehe 09 Septemba,2017

(Anwani za kila Ofisi ya mkoa ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu zimeambatishwa na tangazo hili.)

NB:
i.Tangazo hili linapatikana kupitia
www.nbs.go.tz pamoja na
www.eastc.ac.tz

ii. Wale watakaochaguliwa kwa ajili ya usaili ndio watakaoitwa.

NBS haitahusika na gharama za kuja kwenye usaili huu.

IMETOLEWA NA
MKURUGENZI MKUU
OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
24 Agosti, 2017
 
Attachments

  • Tangazo-la-Kazi-Utafiti-wa-Kilimo.pdf
    196.5 KB · Views: 87
TANGAZO LA KAZI ZA WADADISI (NAFASI 560)

kamasijaelewa vile ajira ya mwezi 1 au
 
si walitoa zile 400 ,na watu walipeleka barua au wameona hawatoshi?
 
Nendeni mkaombe hizo kazi ili mpate pesa ya ku trade FOREX. Acheni kulalamika, Mwezi mmoja si haba.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom