Nafasi 2 za kazi (office secretary & sales representative)

Nafasi 2 za kazi (office secretary & sales representative)

MarkD

Member
Joined
Jan 10, 2012
Posts
75
Reaction score
46
Plus Finance Company Limited ni kampuni inayojishughulisha na utoaji wa huduma za ushauri wa kibiashara ikiwemo kuandaa mchanganuo wa biashara na maelekezo ya tafiti za kitaaluma (Facilitation on Masters Degree level proposal & dissertation write up) na masoko.

Tunatangaza nafasi mbili (2) za kazi kama ifuatavyo:

1. OFFICE SECRETARY (inafaa mtu wa kike): Elimu kuanzia kitado cha nne hadi Diploma, awe mbunifu na mtu anayejituma kufanya kazi bila usimamizi wa karibu.

2. SALES REPRESENTATIVE (inafaa mtu wa kiume): Awe na elimu kuanzia kidato cha nne hadi Diploma, awe na ufahamu wa maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, awe na uwezo wa ushawishi na kujieleza kwa ufasaha, awe mbunifu wa mbinu mbalimbali za kimasoko hasa ya huduma za ushauri wa kibiashara. Pia awe tayari kutembea na kuzunguka sehemu mbalimbali Jijini.

Mwisho wa kupokea maombi ni Alhamisi tarehe 14 November, 2013 saa 12 jioni. Kwa maelezo zaidi fika ofisi yetu iliyopo eneo la Magomeni- Morocco hotel karibu na DD Pharmacy katika jengo la ghorofa mpya inayojengwa, kuanzia muda wa saa 11:00 jioni hadi saa 12:30 jioni, au piga simu 0753 12 54 74, barua pepe ni: plusfinancemd@gmail.com
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom