Naendelea kusikitishwa na NHC

mi_mdau

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
1,104
1,476
Eti linaitwa shirika la nyumba la taifa lililoboreshwa na lenye nguvu kazi mpya. Sioni kama linaendeshwa kwa manufaa ya watanzania wengi, kama nakosea mtanisaidia.

Walivyoanza kutangaza kuuza nyumba za ubungo nikawa na shauku ya kujua ntazipataje na pengine nikichukua mkopo wa miaka mingi ntajikomboa. Bei ikanikata maini kabisa. Leo naona tena wanaanza mchakato wa kuuza nyumba za mchikichini ilala. Ila nyumba 1 ya vyumba vitatu naambiwa itauzwa kwa shilingi milioni 168 na ushehe bila VAT.

Watazania wangapi wataweza bei hii?? Hapo hujakopa, ukikopa utaongeza na riba kwenye hiyo bei. Zipo nyingine kadhaa wameuza ikiwemo za dodoma. Wanamlenga nani?? Je NHC sasa ni shirika la biashara??

Kwa mawazo yangu, NHC si kwa manufaa ya watazania wengi ambao wana kipato cha kawaida sana. Nyumba hizo watanunua matajiri halafu nao watulangue kwenye kodi.

Hili nalo limeniskitisha
 
wako kibiashara zaidi mkuu, linajiendesha halina ruzuku!
 
Kaulize bei kwa private developers hiyo nyumba ya vyumba 3 kabla ya kuwatuhumu NHC au unataka waombe ruzuku serikali wakati wanatakiwa wajiendeshe kibiashara? Tuwe wakweli jamani ukitaka kiwanja tu eneo hilo kwa sasa utapata kwa bei gani?
 
Real estate is one of the booming industry in the region.....I think their prices is reasonable and probably below the market value! Kama una hiyo pesa its worthy for the investment..........

enzi za ujamaa zimekwisha tupo katika zama za ubepari.......
 
Kaulize bei kwa private developers hiyo nyumba ya vyumba 3 kabla ya kuwatuhumu NHC au unataka waombe ruzuku serikali wakati wanatakiwa wajiendeshe kibiashara? Tuwe wakweli jamani ukitaka kiwanja tu eneo hilo kwa sasa utapata kwa bei gani?
Maoni yangu ni hayaHizo nyumba ni flats na sio kuwa kila moja ina kiwanja chake. Ziko takribani hamsini, kwa hiyo kiwanja hakitakuwa ghali sana kama gharama ikitawanywa kwa hizo nyumba. Ilakumbuka hicho kiwanja ni chao kwa miaka mingi tu. Kama tunataka hilo shirika lijiendeshe kibiashara, kodi wanazokusanya toka kwenye maelfu ya nyumba zao haiwezi kutosha kujiendesha? Ila naona wakurugenzi wanatembelea V8, pengine kwa hilo pekee hazitatosha. Maana yangu kama wanataka kujiendesha kwa faida kubwa hivyo inayofanana na mashirika ya watu binafsi basi shirika limepoteza dhana ya utaifa. Dhana ya ubepari haitufai watanzania kwa sababu si mfumo unaoendana na nchi yenye watu masikini kama Tanzania.Watafute njia za kupata mikopo yenye riba nafuu kabisa (au inayokaribia sifuri) toka nje. Wana nyumbanyingi wanazoweza kutumia kama dhamana. Pesa hizo watumie kujenga nyumba za bei rahisi. Vinginevyo tusiendelee kudanganyana kwa kuendelea kuliita hili shirika ni la nyumba la TAIFA
 
Na huu mtindo wa kulipa mamilioni kwenye vituo vyote vya television eti wanajionesha wakurugenzi,sijui walitenga kiasi gani cha pesa kwenye advertisement, na matangazo ya nini kote huko wakati wao ni monopoly?
Huyu mkurugenzi mkuu mpya alikuwa mkurugenzi wa benki kabla ya kuteuliwa kuliongoza shirika hili, nadhani anadhani NHC kuna ushindani kama ilivyo sekta ya mabenki, alipoteuliwa alifukuza wakurugenzi na mameneja wote aliowakuta,kisha akawabeba wenzake kutoka huko alikokuwa akawapa ukurugenzi na umeneja hapo NHC.

Hili la 168m kwa vyumba vitatu floor ya nne sikubaliani nalo.
 
Back
Top Bottom