Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 5,527
- 7,121
Mungu alimwahidi Ibrahimu akisema: “Nitawabariki wakubarikio, na atakayekulaani nitamlaani” (Mwanzo 12:3). Kauli hii haikubaki historia tu, inajidhihirisha mpaka leo kwa mataifa na watu binafsi.
Marekani ni mfano wa taifa la watu waliobarikiwa kwa sababu wanaiunga mkono Israeli. Tangu kuanzishwa kwa Taifa la Israeli mwaka 1948, Marekani imekuwa mshirika wake mkuu. Matokeo yake, Marekani ni taifa lililoinuka kiuchumi, kiteknolojia, na kijeshi kuliko mataifa mengi. Hata pale changamoto zinapokuja, bado Marekani imeendelea kuwa na nguvu kubwa katika dunia. Hii ni ishara ya wazi kuwa Neno la Mungu ni kweli na halibadiliki.
Mataifa yaliyoishambulia Israeli mwaka 1967 wakati wa Vita vya Siku Sita ni mfano mzuri wa madhara ya kuilaani au kuipinga Israeli. Katika vita hivyo, Israeli ilishinda majeshi ya nchi nyingi kwa siku chache tu, na hadi leo mataifa hayo bado yanahangaika kisiasa na kiuchumi. Mashirika na viongozi wa kigaidi wanapata uharibifu mkubwa, kila mara wanapoinua mikono yao dhidi ya Israeli. Badala ya mafanikio, wamekuwa wakipata maangamizi na kupoteza uhalali mbele ya dunia.
Wakristo wa mataifa mbalimbali, wale wanaoomba kwa ajili ya Yerusalemu na kuiunga mkono Israeli mara nyingi hushuhudia baraka binafsi: maendeleo, mafanikio ya huduma, na ulinzi wa ajabu wa Mungu. Ndio sababu, wengine hata katika ofisi zao, wanaweka bendera ya Israeli, kuonesha kuwa wanaibariki nchi hiyo.