Naenda kuoa kijijini

Naenda kuoa kijijini

mr vata

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2017
Posts
465
Reaction score
617
Mara nyingine huwa nawaza kuhusu ule wimbo wa mwanaume suruali, mbona kama unanihusu? Wanawake wa Dar es Salaam mmenishinda kiukweli. Jamani, wenzangu mnaomiliki watoto wakali hapa mjini huwa mnafanyaje, embu nipeni mbinu mbadala mwanamke wa hili jiji ana gharama jamani.

Yaani ukimtongoza tu nafikiri yeye anaona tayari kapata kazi. Kila siku vibomu vya hataree, mara anaumwa, mara simu yake imeingia maji, mara kodi yake imeisha, hapo bado kuhusu kula yake, kusuka na mavazi. Usipomtimizia ndio hilo jina la mwanaume suruali linakuganda.

Kinachonishinda sio kumpata mtoto mkali bali kuendelea kuwa nae huku nikimpa mahuduma ayatakayo bila kukosa. Sasa nimekata shauri, na naomba msinielewe vibaya. Uamuzi huu hautokani na hii hali ya hii awamu ya tano

Naenda kutafuta mke kijijini, nimechoka kuitwa mwanaume suruali na wanawake wa hili jiji ambao naona wengi wapo kimaslahi zaidi.

Naomba mnitakie kila la kheri!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani mwanamke wa kijijini yeye ndio hawezi kufanya hivyo?

Ni heri ukaoa kahaba aliyehangaika na maisha kuliko Bikira Wa kijijini umlete mjini mwenyewe. Au oa wasaidizi wa kazi hawa, kidogo wanakuwa wameshaujua mji.
 
Wa kijijini ukimleta mjini bado tuu atakuwa ni wa kijijini? Hujui asilimia kubwa sana ya watu wa dar walitoka kijijini?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom