Naenda kuanza maisha Iringa sina sehemu ya kufika na nina pesa ya nauli tu

Wakuu walioko iringa nimeamua kuzamia mkoa wa iringa msaada sehem ya kufikia Sina pesa ya guest Naombeni ushauri na mawazo ama sehem ya kufikia kulala

Naenda kuanza maisha nisaidieni wakuu msaada.. Pia naomba ushauri wapi napata kibarua kazi yeyote naifanya lengo nipate pesa ya mtaji asanteni

We uendi kuanza maisha unaenda kuanza matatizo izo zilikua zama za zamani ila sasa jiandae kusukumwa ndani tu ndugu yangu
 
Pambafffff kabisa,yaani unaendaje kichwa kichwa sehemu usiyoijua wala kuwa na ABC za kuanzia? Ulikotoka umeiba ama? Kama akili yako iko sawa nashauri uanzie maisha makaburini, uwe unafanya usafi pale marehemu watakufikiria huku watu wa mazingira wakikutunza kwa chakula na chandarua wakati wa usiku!
 
Huo ujio niwa verse moja au tatu
Wakuu walioko iringa nimeamua kuzamia mkoa wa iringa msaada sehem ya kufikia Sina pesa ya guest Naombeni ushauri na mawazo ama sehem ya kufikia kulala

Naenda kuanza maisha nisaidieni wakuu msaada.. Pia naomba ushauri wapi napata kibarua kazi yeyote naifanya lengo nipate pesa ya mtaji asanteni
 
Mkuu unazikimbia pesa za korosho na gas unafuata umbwa? Utani.
Sehemu nzuri ya kuzamia/kujilipua ni daslam tu kwasababu zifuatazo.
1)unaweza kulala hata vibarazani kariakoo
2)kuna makabila kama yote ni rahisi kukutana na kabila yako akakusaidia.
3)kuna kazi za kutumia nguvu badala ya akili kama kubeba na kufunga mizigo.
4)kuna mama ntilie wengi na chakula ni bei poa hata ukiwa na buku unakula.
5)kama unaakili ni rahisi kukusanya mtaji mdogo ukaanzisha biashara yako kama kuuza maji, biskuti/pipi au pamba za masikioni na ukaweza kujikimu.
Nipo mtwara mkuu nataka kubadilisha mazingira mkuu
 
Nimekupata mkuu sasa dar nazamia vipi nipe maujanja kidogo
 
Huo mkoa uendao si sahihi kama unaenda tafuta maisha na kianzio huna, njoo DSM ukiamua ht kutembeza pweza na ngisi kwny Sinia, ama samaki wa kukaanga kwny Sinia pia na chachandu kwa mtaji mdogo ht wa 20,000 utaishi bila wasiwasi...huku fursa za ujasiriamali ni nyingi...ht utumbo wa kuku watu wanakula, ukipika maharage na chai pia utauza...otherwise ukija Dar nitafute, ila usiache nibebea zawadi ya Ulanzi
Mkuu nimekuelewa nipe plani za kuzamia hapo
 
Mkuu kwanini usiende mbeya Tukuyu kuna plantation ya Parachichi inaitwa Rungwe avocado company? Au nenda Moshi wilaya ya siha kuna plantation inaitwa Kifufu estate wanalipa poa sna na kazi ni nyingi pia kwenye hizi plantation. Iringa pia kuna moja sema jina nimeisahau ipo njiani tu ukiwa unatoka moro unaiona. Jaribu kuswitch kwenye industry ya kilimo huwezi kosa kibarua
 
Jamaa vip ushafika Iringa boss wetu tupe updates za mambo yanavyokwendea uko chief!!
 
Back
Top Bottom