poposindege
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 456
- 175
​ Ha ha ha balaa!!!!!Mkuu achana nayo hiyo nyumba ya urithi tafuta yako,.... utaanza kuokota makopo bure shauri yako.
Mimi walinikosakosa.
​ Ha ha ha balaa!!!!!
Habari wadau,
Kuna nyumba imeachwa na marehemu baba yetu, mimi na ndugu yangu tupo wawili tu. Yeye amenizidi umri kama miaka 20. Nyumba hiyo amedai ni ya kwake na wala si ya baba yetu kama ilivyokuwa ikifahamika na kutamkwa na marehemu mzee wetu.
Nimejaribu kumwambia ukweli wa kauli ya mzee wetu anadai si kweli nyumba ni ya kwake. Tumefanya vikao kadhaa ameonesha ushahidi wa yeye ndiye mmili halali wa nyumba hiyo.
Ushahidi alioutoa ni leseni ya makazi (sio hati) iliyotolewa mwaka 2012 yenye jina lake. Swali aliloulizwa baada ya kutoa leseni hiyo ya makazi, je ana ushahidi wa umiliki wa nyumba hiyo kabla ya kupata leseni ya makazi mwaka 2012. Alitoa karatasi ya mauziano ya nyumba hiyo ya mmiliki wa awali
kabla ya kuimiliki yeye.
Lakini ushahidi huo alioutoa umegundulika si wakweli. Imebainika mauziano hayo yanaonesha ni nyumba ya eneo lingine na sio hiyo inayokusudiwa. Kumbuka nyumba ni ya miaka tangu 1970s na ipo maeneo ambayo hayajapimwa.
Ukweli ni kuwa nyumba hiyo ilinunuliwa na Marehemu baba yetu na kwa kuwa huyo mwenzangu ni mkubwa aliwahi kuchukua documents zinazohusu nyumba wakati mzee anaumwa. Mzee wetu amefariki miaka sita iliyopita.
Kwa kweli nimekwama nahitaji msaada wenu nifanyeje ili niweze kupata haki ambayo nadhulumiwa.
Asanteni sana.
Asa hii mahakama
pole sana nduguMkuu achana nayo hiyo nyumba ya urithi tafuta yako,.... utaanza kuokota makopo bure shauri yako.
Ahsante kwa ushauri
Mimi walinikosakosa.
Ushauri mzuri ahsante nduguIla ndg yangu poposindege, Achana kabisa na mambo ya urithi kama vp pambana tu ujenge nyumba kwa jasho lako, watoto wengi wa Kitanzania wamelemaa na mali za urithi yaani kukicha wanaomba wazazi wao wafariki wagawane mali .
Ni kweli anajua kama anadhulumu, ila hajali kituKama kaka yako kaamua kukuzulumu, Mwachia Mungu and move forward .... Utaingia kwenye tabu! Ipo Siku Atajua amefanya dhuluma na kujirudi ila usipambane
Ni kweli usemayo, lakini nina haki ya kurithiHuwa sijisikii happy kwa vitu vya urithi napamba nipate changu and will be proud of having my own assets
Ndio ni ndugu wa damu kabisa tena tumbo mojaYaani brother ako wa damu anakudhulumu?
Naendelea kumuomba Mungu aniepushe kwa mabaya yote yanayoelekezwa kwanguPole sana lakini Mkuu ningekua wewe wala nisinge taka ningezidi kumuomba mungu anipe changu,sisi tumezaliwa 13 matumbo mawili,upande wetu tuko 8 na mwengine 5 wao wenzetu ndio wakubwa mzee kufariki aliwacha nyumba 6
kwa upande wetu sie 8 watoto wa kiume ni 5 na kwa upande wa wale wakiume ni 1 basi kabla ya urithi tuliipata fresh,
Tuna lala usiku unashanga unakuta nyoka ndani ya shuka,ukienda jikoni unakuta nyoka kwenye sofa,na hapo wameshajua kama sie ndio tuna pata nyumba nyingi,tumesoma kisomo tuka muachia mungu,tatizo ya wale wenzetu shule zero walikata kusoma wakajua tutaadhirika,tulikuja kuzinunua nyumba zote kwao na sasa bila aibu watoto wao wanalelewa nakusomeshwa na sisi,chamsingi usigombanie mali usioichuma..
Inawezekana ni yeye kaingia humu ha! ha! ha!We lazima utakuwa ndiye kaka wa mtoa mada yule zulumati
Pole sana ndugu poposindege naona watu waliopona kufanyiwa juju wamekutisha sana hadi umetokomea..
Unaweza kupata haki yako. Baada y mazazi wenu kufariki mlikaa kikao cha familia na kufungua jalada mahakamani kuteua msimamizi wa mirathi? Kama sio huyo ndugu yako anapata wapi haki ya kujigawia nyumba!
Umesema baba yenu amefariki miaka sita iliyopita lakini residential licence aliyonayo ndugu yako imetolewa mwaka 2012, fuatilia huenda hiyo document ni batili
Fungua kesi baraza la ardhi na nyumba kwenye eneo lako. kuna gharama lakini haki yako itapatikana. Unaweza kuwaona NOLA kama huna uwezo wa kugharimia wakili.
Mkuu achana nayo hiyo nyumba ya urithi tafuta yako,.... utaanza kuokota makopo bure shauri yako.
Mimi walinikosakosa.
Ahsante Lusajo11 kwa ushauri mzuri
Maoni ya kwamba ntafanyiwa juju hayajanitisha ila yameniongoza ktkkufanya tahadhari zaidi.
Kuhusu residential licence iliyotolewa 2012 ni halali. Ni kwamba hizo leseni hutolewa bila ya masharti mengi na uthibitisho mwingi. Nilijaribu kupata maelezo kwa watu wa wizara ya ardhi walinambia kwamba hizo leseni zilitolewa kwa yule aliyejitambulisha kwamba yeye ndiye mmiliki wa nyumba bila ya kupata uthibitisho wa nyaraka zingine. Yaani walipopita ktk nyumba kwa zoezi la uandikishaji aliyejitambulisha kwamba ndiye mmiliki basi walimuandikisha yeye. Na hili ndio alilofanya ndugu yangu. Watu hao wa Ardhi walinambia zoezi hilo lilileta kesi nyingi kwa baadhi ya maeneo walipojitokeza watu zaidi ya mmoja kudai wamiliki wa nyumba moja. Kesi ya Mirathi ilishafunguliwa na mimi kuteuliwa kama msimamizi wa mirathi lakini kukawa na utata wa nani mmiliki halali wa nyumba kati ya baba yetu au kaka yangu. Utata huo tukaambiwa twende kwenye mahakama za juu ili kutatuliwa na kujulikana nani mmiliki halali kati ya marehemu baba yetu au kaka yangu. Tatizo lililopo documents za manunuzi ya nyumba alivyonunua baba yetu kaka yangu kazificha kama kupoteza ushahidi wa mmiliki halali wa mwanzo. Gharama za kufungua kesi baraza la ardhi na nyumba ni kiasi gani?
Kuhusu gharama, ingia kwenye website ya Wizara ya Ardhi zilibadilika mwaka 2012 nadhani. Ila ni affordable hata kwa mtu wa kawaida.
Kuhusu utata wa nani mmiliki kati ya mzee wenu na ndugu yako, ni suala la ushahidi tu. Kwa kuwa nyumba yenyewe ipo kwenye squater, andaa majirani waliokuwepo tangu zamani lakini muhimu zaidi yule aliyeuza nyumba kama utampata. Documents alizoficha zisikutishe ukikomaa utamkamata mahali tu. Kuna kesi za documents huwa zunakuwa complex zaidi ya hiyo ila haki inapatikana
Asa hii mahakama