NADHAMIRIA KUISHTAKI Zain kwa UCHOCHEZI

NADHAMIRIA KUISHTAKI Zain kwa UCHOCHEZI

Kama ni kudai fidia sio charge ni plaint, naunga mkono. Tukishakuwa wengi italeta maana
Mkuu charge niliyosema ni uchunguzi kwa kosa la jinai halafu hiyo plaint ipo njiani maana ni suala langu na wakili. Lakini jinai ndo ishu ya polisi.
But nashukuru kwa ufafanuzi
 
mkuu tuko pamoja maana hata mimi ni muathirika wa hizi sms za maji taka ...
 
mkuu tuko pamoja maana hata mimi ni muathirika wa hizi sms za maji taka ...
Mkulu umechagua haki. Nikipata barua muhimu kutoka polisi nitawajulisha hapa ili tuweze kujumlisha kesi za madai kwenye plaint moja. ila jinai itabidi niendelee nayo kwani nilistep in kwa statement yangu.

Lazima tuilinde nchi dhidi ya wachochezi na wafadhili wao.
 
Mkuu charge niliyosema ni uchunguzi kwa kosa la jinai halafu hiyo plaint ipo njiani maana ni suala langu na wakili. Lakini jinai ndo ishu ya polisi.
But nashukuru kwa ufafanuzi

Kwa malalamiko ya namna hii ni muhimu kuwe na kesi mbili ili wasichomoke
1. Criminal (mostly as accomplices).
2. Civil

List ya walalamikaji iwe kubwa ili kutia uzito katika kutoa ushahidi kuonyesha jinsi jamii ilivyoathirika na kitendo chao hicho.
Ni muhimu kujua kuwa ile hali ya kutochukua hatua kudhibiti sms za kichochezi hata kama wao hawajahusika moja kwa moja kuziandaa inatosha kuwatia hatiani!
 
kwenye mkataba wako na Zain mlikubaliana nini?

kuwa hutaki kupokea ujumbe wowote kutoka namba usiyo ijua?

au uliweka mkataba kuwa hutaki kupokea ujumbe wowote wa kisiasa?

au uliweka mkataba kuwa hutaki kupokea ujumbe wowote unaoegemea kwa chama tawala?


lkn kabla ya yote hayo, una mkataba wowote na hao Zain kweli?

Msanii, hakika message zilikuwa na usumbufu mkubwa. Wakati fulani usiku wa manane unapokea message, unafikiri ina mantiki, kumbe hakuna kitu ni propaganda za kisiasa. Lakini pointi alizotoa huyu ndugu ni za msingi, ili usije ukafungua kesi kama za EPA, ambazo hatima yake iko kwenye maamuzi ya serikali siyo mahakama!!!!!!!!!!
 
Nimepata pia hiyo kutoka namba ya ajabu ya zain. Namba zilikuwa 5 za mwisho
 
Mkuu ebu anza then tutasesa toka kwako maana mimi nina hasira na VODACOM
 
Nilikuwa nazani bado watanzania tupo gizani na masuala ya sheria na haki za mtu.

Hilo wazo ni zuri sana naninaomba wale wote waliotumiwa msges hizo wasifute ili kutunza ushaidi hii ulaya kwa wenzetu ni big scandal sasa tunatakiw atuwe na mshikamano wa haraka sana ili ikiwezekana week ijayo tufungue hiyo kesi.

Tumechoka kuonekana watanzania ni wajinga mpaka leo hii haiwezekani miaka hii na elimu zetu tunafanywa kama tuna beba mabox ugenini?

Please we need your seriousness on this ... We are together....Kama wakili hatoshi tutaongeza wengine pia wasaidie kulete utetezi mzuri.
 
Wakuu,
bado suala lipo kwenye miguu yangu. mpaka sasa sijapata wakili, nilisema kwamba nilienda LRHC nikakuta msaidizi ambaye alinikatisha tamaa. yaani aliniambia hawawezi kunisaidia mpaka wapate barua kutoka zain. mpaka sasa sina wakili wa kuniongoza but ubishi wangu ndio unaonivusha vikwazo vya polisi kutaka kulifunga jalada. Tumekubaliana na mandata kwamba jumatano hii niende kuonana na mpelelezi wa kesi yangu na tutaenda kufuatilia ZAIN kwa uchunguzi ili niweze sasa kuchukua hatua za kisheria zaidi. Nashukuru baadhi ya wanausalama wameniunga mkono ila bado najiona nipo peke yangu.
Natoa shime kwamba ikifikia kuandaa isu ya CIVIL tuungane woote tiulioathiriwa na hizi sms.

I am serious. and I am doing my party.
 
Msanii Chonde Chonde ndugu yangu usikate tamaa, komaa nao, ukifanikiwa utaweka precedence nzuri sana, na huo utakuwa mwanzo wa makampuni kufanya mambo kwa kuzingatia sheria.

Nitakupa mfano, kuna jengo la sophia house pale karibu na maktaba, wale jamaa wamereserve parking kwa magari yao kiasi kwamba sehemu ya kuvukia ya raia (zebra crossing), nayo wamewekea mnyororo wa kuwaziba raia wasipite, raia wakitaka kuvuka inabidi wazunguuke wakavukie sehemu isiyoruhusiwa kisheria. kwa hiyo unaona jinsi mambo yanavyokwenda shaghala baghala bongo, bila kutiwa kashikashi ya kisheria hawa hawawezi kusikia.

Kitu kingine ninawasiwasi kwamba kesi ikishakuwa Imminent jamaa wanaweza kutaka kuyamaliza kiutu uzima na wewe (kamshiko ka aina fulani). ikitokea hivyo ndugu yangu sijui utaendeleza mchakato?

Ila nakuunga mkono moja kwa moja, yaani ukifanikiwa japo hata kesi kusimama mahakamani itakuwa ni ushindi mkubwa wa kinidhamu na kisheria. Tuko pamoja mkuu.
 
kwenye mkataba wako na Zain mlikubaliana nini?

kuwa hutaki kupokea ujumbe wowote kutoka namba usiyo ijua?

au uliweka mkataba kuwa hutaki kupokea ujumbe wowote wa kisiasa?

au uliweka mkataba kuwa hutaki kupokea ujumbe wowote unaoegemea kwa chama tawala?


lkn kabla ya yote hayo, una mkataba wowote na hao Zain kweli?

''Tatizo tulilo nalo hapa bongo hatuna mikataba na huduma hizi yaani zipo zipo tu. Nikama tunasainishwa automatically that's why watu wa promotion hawapata ridhaa ya wahusika''
 
Msanii Chonde Chonde ndugu yangu usikate tamaa, komaa nao, ukifanikiwa utaweka precedence nzuri sana, na huo utakuwa mwanzo wa makampuni kufanya mambo kwa kuzingatia sheria.

Nitakupa mfano, kuna jengo la sophia house pale karibu na maktaba, wale jamaa wamereserve parking kwa magari yao kiasi kwamba sehemu ya kuvukia ya raia (zebra crossing), nayo wamewekea mnyororo wa kuwaziba raia wasipite, raia wakitaka kuvuka inabidi wazunguuke wakavukie sehemu isiyoruhusiwa kisheria. kwa hiyo unaona jinsi mambo yanavyokwenda shaghala baghala bongo, bila kutiwa kashikashi ya kisheria hawa hawawezi kusikia.

Kitu kingine ninawasiwasi kwamba kesi ikishakuwa Imminent jamaa wanaweza kutaka kuyamaliza kiutu uzima na wewe (kamshiko ka aina fulani). ikitokea hivyo ndugu yangu sijui utaendeleza mchakato?

Ila nakuunga mkono moja kwa moja, yaani ukifanikiwa japo hata kesi kusimama mahakamani itakuwa ni ushindi mkubwa wa kinidhamu na kisheria. Tuko pamoja mkuu.
Hapo kwenye bold mkuu wangu ni muhimu nikapatolea maelezo.
Ni kweli kwamba sina msimamo mzuri kimaisha lakini siyo kigezo cha kuuza utu wangu kwa vipande vya fedha kaka. Sijawahi kuhongwa ili kudelete haki halali.
I am doing this kwa sababu watu wanachezea maisha ya watu halafu dola inachekelea na kupuuzia vitisho kama hivi ambavyo vinasababisha chuki na husda kuongezeka.
Mkuu nashukuru kwa kuunga mkono.
 
Nadhani ikitokea mteja akanunua bidhaa ya kampuni fulani akaitumia (tuseme, akaila) halafu akapata madhara na ikathibitika kitaalamu kuwa madhara hayo yametokana na kutumia bidhaa hiyo, mteja huyo anakuwa na haki ya fidia. Ninavyoiona hii ya mawasiliano ya simu inaweza kuwa katika mkumbo huo, Wataalamu wa sheria wanaweza kusaidia ikiwemo kutupatia vifungu vya sheria. Lakini kuna mikataba ambayo hufungwa kati ya pande mbili kwa kuzingatia vitendo (contract implied by conduct). Maadam kampuni ya simu inakuwa imekubali kukuhudumia, mkataba upo.
 
Naamini kuwa simu ni private asset ya mmiliki ndiyo maana zimesajiliwa. kama msg uliyopata ilitoka Zain direct you have a ground for filing a suit ila kama imetoka kwenye namba nyingine ikapita zain hapo inakuwa ngumu kushtaki. Binafsi nilipata msg katikati ya kampeni toka voda ikikampe nia CCM na nilitaka dhahiri kuwashtaki kwa kuingilia privacY yangu. Bahati mbaya ile simu ikaanguka kwenye maji ILA nilitaka niweke PRECEDENT kwa makampuni yanayokubali kutumika KIJINGA. Nasema BAHATI YENU VODA NAWASUBIRI 2015.
 
Back
Top Bottom