ni kweli mkuu ndo maana kupitia JF na mitandao mingine tuwajibike kuwaelimisha hawa wenzetuHaya mambo yanaudhi sana. Umbumbumbu wa watanzania kutojua sheria za mambo ya mawasiliano ndiyo yanayosababisha makampuni ya simu kwa uroho wa kutaka pesa kukiuka misingi na taratibu ambazo kwa nchi za wanajanja hawathubutu kufanya hivyo. Mkuu ni kwamba nasafiri vinginevyo tungekuwa begakwa bega kuhakikisha hiyo kampuni inatoa maelezo ya kina ni vipi wanatoa namba za watu bila taarifa wala maelewano. Hiyo ni sawa na mwenye hoteli kumpatia kitimoto ustadhi bila radhaa yake.
Tatizo namba yenyewe haijitoshelezi. Sasa wamewezaje kufikisha ujumbe wa namba kipande?Msanii, mashirika ya simu hayana kesi ya kujibu kuhusu ujumbe huo. Sana sana wanaweza kuwa mashahidi kwa amri ya mahakama kueleza ujumbe huo umetokea wapi. Kutumia mtandao wa simu vibaya ni kosa la mtumiaji si mrushaji. Toaka lini mjumbe huuawa?
Nimewasoma wachangiaji wengi humu wananivunja moyo kwamba hiyo ninachofanya hakiwezekani. Naamini itawezekana kwani nimeamua kupoteza muda wangu kwa jambo hili ambalo labda kwa wengine ni la kijinga
Kuna sheria za TCRA ambazo husimamia service providers wa hapa bongo kwenye mawasiliano. Pia inaruhusiwa kupeleka malalamiko endapo umelipia service lakini hukupata hiyo huduma.ANGALIZO:- Si nia yangu kukuvunja moyo, bali kukupanga.
Mkuu issue ya mkataba inaweza ikawa kikwazo hapa, nakumbuka wakati wa zoezi la usajili wa number za simu, jamaa wa kampuni za simu anakuuliza maswali huku yeye ndiye anayejaza form mwishoni anakwambia sign hapa, sasa inaweza ikawa kwenye form kulikuwa na small prints zinazowaruhusu kufanya hivyo.
Ukipata spam emails kwenye .co.tz account yako utampeleka ISP wako mahakamani, tujaribu kuangalia angle zote.
Wakuu
nimeshafungua jalada la uchunguzi polisi jana tarehe 28/10/2010 baada ya mabishano makali na polisi ambapo waliniomba nipuuzie ishu hiyo kwani hata wao wamepokea meseji nyingi za kipuuzi.
Nilitumia muda wangu kwaelimisha na wakanisoma vyema. mwisho nikawaambia kwamba mimi nimeumizwa na kukerwa na hiyo sms. kama wao haijawakera basi waniache mimi nitumie mkondo wa sheria kudeal na huyu mchafua amani. Polisi wenyewe wamekiri kwamba wakimpata huyo mchochezi watalia naye sana tu
Jalada limeshafunguliwa na sasa uchunguzi rasmi umeanza.
Kumbukeni hapo bado sijapata wakili. nilienda kule kituo cha sheria na haki za binadamu walikuwa wazito mno kuihandle hii ishu ndo nikaamua kuingia front mwenyewe. Nilipofika zain wakanigomea kuonana na meneja wa huduma kwa wateja ndipo nikawaambia wataisoma kupitia mkondo wa sheria.
Wa kuu kesi hii sijaifungua kwa kutafuta maslahi, bali kuweka heshima kwa nchi kwamba kama vyombo vya dola vinapuuzia chokochoko dhidi ya usalama wa nchi basi sisi wananchi tunaweza kupinga hizo hila kwa kutumia sheria zilizopo.
Zain wana kesi mbili kwangu tayari.
Kwa anayeniunga mkono tafadhali waweza kunitumia PM ili tuelekezane namna ya kufanya huku tukipreserve ID zetu.
Kama ni kudai fidia sio charge ni plaint, naunga mkono. Tukishakuwa wengi italeta maananawasiliana na kituo cha msaada wa sheria wanishauri zaidi how to frame charges