MAKOLE
JF-Expert Member
- Feb 5, 2012
- 618
- 280
Kwa wale wanaohitaji kuomba nafasi za udahili katika vyuo vikuu kwa kupitia mfumo wa udahili wa pamoja NACTE sasa hawataweza kufanya hivyo hadi Mwezi May mwaka huu baada ya matokeo ya kidato cha sita 2016 kutoka....
Habari kamili iko hivi:
TAARIFA KWA UMMA
TAREHE 11 MACHI 2016
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuutangazia umma kuwa waombaji wenye Stashahada (Ordinary Diploma – NTA Level 6) wanaoomba kujiunga na Shahada ya Kwanza zinazotolewa na Vyuo Vikuu (Universities) au Vyuo Vikuu Vishiriki (Constituent Colleges of Universities) hawataweza kufanya hivyo sasa. Hii ni kwasababu Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) bado haijafungua rasmi Mfumo wa Udahili wa pamoja (CAS) unaoratibiwa kwa pamoja kati ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU). Tume ya vyuo vikuu inatarajia kufungua mfumo huo wa kudahili kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza mara baada ya matokeo ya kidato cha sita kutangazwa na Baraza la Mitihani la Tanzania kuanzia mwezi Mei 2016.
Hivyo basi, ikifika muda huo ndipo waombaji wenye Stashahada (Ordinary Diploma – NTA Level 6) wanaotaka kujiunga na Vyuo Vikuu au Vyuo Vikuu Vishiriki kwa ajili ya kusoma Shahada ya Kwanza, wataweza kuanza kuomba kudahiliwa kwa kupitia kwenye Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS).
Hata hivyo, tunapenda kutoa taarifa pia kuwa kwa wakati huu, waombaji wenye Stashahada (Ordinary Diploma – NTA Level 6) wanaotaka kujiunga na Shahada za Kwanza zinazotolewa na vyuo vya Elimu ya Ufundi au Taasisi zilizosajiliwa na Baraza (NACTE) waendelee kuomba kudahiliwa na Taasisi hizo kupitia Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS) unaoratibiwa na Baraza ambao umezinduliwa tarehe 4 Machi, 2016.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA UDAHILI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
au tembelea TAARIFA KWA UMMA - NACTE kwa maelezo zaidi