NACTE wanalioa tatizo hili la vyeti kucheleweshwa

bichwa mtoto

JF-Expert Member
Aug 9, 2018
274
563
Mimi ni muhitimu wa stashahada kutoka katika chuo kimoja cha maendeleo ya jamii hapa nchini .chuo hicho ni miongoni mwa vyuo vilivyopo chini wizara ya afya,maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto ambapo miongoni mwa vyuo hivyo ni monduli, buhare, uyole na vinginevyo.

Sasa lengo la Uzi huu ni kwamba ilikuwa Toka mwezi wa saba mwaka 2019 tulipo maliza elimu ngazi ya stashahada (diploma) mpaka muda huu naandika Uzi hatujaweza kupatiwa vyeti takribani miezi kumi imepita sasa.

Nauliza hawa NACTE je vyeti hutolewa kwa kipindi gani tangu mhitimu anapomaliza. ukizingatia bila kuwa na cheti huwezi pata kazi yoyote ile inayohitaji cheti kuna NGOs kibao nimesha jaribu naambiwa cheti

Na vyuoni vyeti havijafika walimu wanasema tatizo ni Huko NACTE mjue mnatuangusha vijana wenu huku mtaani.

NB USINIAMBIE HAKUNA AJIRA HUWEZI JUA MJOMBA NI HR NGOs GANI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, pambana na chuo husika mbona vyeti vimetoka kwa waliomaliza 2019.. Mm ni miongoni mwa wahitimu mwaka jana na nimefuata cheti changu mwezi March mwaka huu
 
Back
Top Bottom