Maelezo gani?Toa maelezo
watatoa tena mda kuwa na subiraMayoo weee nafwa na kaz yanguu ya ulinziii
ilishalima
naomba kuuliza na je kama umetuma maombi na hujachaguliwa, je unaweza kuomba tena awamu ya pili?Someni hii taarifa kutoka NACTE;
Tarehe 3 Juni 2016 ilikuwa siku ya mwisho ya kuwasilisha maombi ya udahili wa kozi za Cheti, Diploma, Diploma ya juu na Shahada ya kwanza kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja unaoratibiwa na NACTE.
Baraza linapenda kuwaarifu waombaji udahili wa kozi tajwa hapo juu na umma kwa ujumla kuwa, kwa sasa maombi yote yaliyowasilisha mpaka tarehe 3 Juni 2016 saa sita usiku yameanza kuchambuliwa kwa ajili ya kuchagua waombaji wenye sifa stahiki. Zoezi la kuchambua waombaji udahili na hatimaye kuchagua waombaji wenye sifa stahiki na waombaji hao kuidhinishwa na mamlaka husika na kutangazwa litachukua muda wa wiki tatu hadi nne kuanzia tarehe 3 Juni, 2016.
Baraza linatambua uwepo wa waombaji wapya na baadhi ya waombaji walioshindwa kuwasilisha maombi yao kupitia mtandao ilipofika tarehe 3 Juni 2016. Waombaji wa namna hii na wengine wanaopenda kuwasilisha maombi yao kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja wanaombwa kuwa na subira mpaka hapo majina ya waombaji waliowasilisha maombi yao kabla ya kufungwa kwa mfumo watakapotangazwa.
Baada ya kutangazwa majina ya waombaji waliochaguliwa, Mfumo wa Udahili wa Pamoja utafunguliwa tena kwa ajili ya kujaza nafasi za udahili ambazo zitakuwa wazi na waombaji waliowasilisha maombi yao kuanzia tarehe 4 Machi, 2016 hadi tarehe 3 Juni 2016.
Baraza linatarajia kufungua tena Mfumo wa Udahili wa Pamoja kwa ajili ya kozi za Cheti, Diploma, Diploma ya juu na Shahada ya kwanza kati ya wiki ya mwisho ya mwezi wa sita, 2016 na wiki ya kwanza ya mwezi wa saba , 2016.
Imetolewa na
Kaimu Katibu Mtendaji
NACTE
Tarehe: 7 Juni, 2016