NACTE tatizo ni nini?

NACTE tatizo ni nini?

Shebbydo

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2015
Posts
1,174
Reaction score
1,937
0dcca47cd250ddef3219caadcdb15b3f.jpg


Habari Wana JF,
Ndugu wanaJF, naimani wadau wa elimu mnafaamu wazi kuwa NACTE walikuwa tayari wamefungua uombaji wa kudahiliwa katika taasisi za elimu ya juu kwa upande wa wale walio na stashahada kwenda kusoma shahada ya kwanza.

Leo asubuhi kuna mtu aliniomba nimtumie maombi ya shahada ya kwanza kupitia stashahada. Kweli nilipoangalia kwenye "website" ya NACTE nilikuta tayari walishafungua na mwisho ni tar 31 mwezi huu. Nikaona basi kazi hii nitaifanya muda wa mchana nikiwa nimepunguza shughuli zangu.

Jambo ambalo linanishangaza ni pale nilipoamua tena kuingia kwenye "website" ya NACTE ili nifanye kazi hiyo nalikutana na mabadiliko. Nimeona tena kumefunguliwa maombi ya astashahada na stashahada yamefunguliwa, lakini mwisho wake ni leo hii leo usiku. Hali ni kama hivyo inavyoonesha hiyo "snapshot" hapo juu.

NACTE tatizo ni nini ilihali maombi ya astashahada na stashada yalikwishasitishwa na sasa ulikuwa ni uchakataji? Au mifumo yenu si imara? Na kama mifumo yenu si imara, hamuoni hata machaguo yatakuwa yakichakatwa kimakosa? Au kuna mtu aliyechelewa kufanya maombi sasa mfumo umefunguliwa kwa muda huo mfupi ili akamilishe maombi yake.

Rai yangu kwenu NACTE, mambo yaende kwa ratiba. Haya mambo ya mara maombi yamefungwa, mara yamefunguliwa hayaleti maana.
 
Wew usibabaike na hayo maelezo yao wew log in tu saiv admission ni kwa bachelor tu hat mm nimekuta ivo ila nikaingia kwenye account yang fresh
 
Hapo umenena sijui hii mada inahusiana vipi na elimu wakati ni kutuma maombi tu kwa sasa elimu ni huko chuo ukichaguliwa au wataka kutueleza nini maana mie sijaona tatizo hapo.
 
Back
Top Bottom