kindikwili
JF-Expert Member
- Oct 5, 2016
- 1,862
- 2,871
Kwanza nachukua fursa hii kumpongeza waziri wa elimu prof Ndalichako japo najua wachache watanielewa kutokana na mtazamo hasi zilianza kujengwa kwake. Ukweli ni kwamba sisi watanzania kwa sehemu kubwa hatujui hasa tunachokitaka. Tulilia mabadiliko sana lakini hatukujua ni kipi tulitaka, watu walitaka rushwa na ufisadi udhibitiwe bila kujua kuwa kwa kufanya hivyo kuna impact kubwa utaonekana hadi kwa watu ambao walikuwa hawali rushwa wala si mafisadi. Watu walitaka mabadiliko kwenye sekta ya elimu lakini wakiwa na ndoto kuwa hawatayumbishwa hata kidogo. Ukitaka mabadiliko jiandaye kuyapokea maumivu yake maana ni kama kubomoa na kujenga upya nyumba yako.
Nasikitika sana jinsi kauli ya prof Ndalichako ulivyopotoshwa kwa makusudi, mimi nilipoisikia kwenye You tube nilisikia kipande alichokuwa akiongelea foundation courses kwa aliyefeli form six. Akidai kuwa foundation haimpi mtu uhalali wa kusoma chuo kikuu, lakini watu walipotosha kuwa kasema hakuna kwenda chuo kikuu kupitia certificate kisha diploma. Hadi wasomi walikuja juu na kumshambulia prof Ndalichako bila hata kusikia kauli yake. Dk Bana alipoulizwa na mwandishi kuhusu kauli hiyo alisema ''kama kweli kasema hivyo basi kakurupuka na hakushauriwa vizuri''. Hivi ilikuwa inamgarimu dk Bana kitu gani kumwambia mwandishi samahani mimi hiyo habari sijamsikia akisema nipe muda niitafute kisha nitatoa maoni baadaye. Kwani ni lazima kutoa maoni kwa kauli ambayo hujaisikia tena ukijua kuwa baadaye utanukuliwa kwenye hiyo habari?. Kwa maoni yangu wale wote waliomshambulia prof Ndalichako ni WASOMI UCHWA HATA KAMA WANA PhD ngapi. Mtu mwenye Phd huwezi kukosoa kitu ambacho hujakisikia.
KUHUSU NACTE KUWA NA MITIHANI YA TAIFA KAMA NECTA
Baraza la mitihani la taifa (NECTA) kama tunavyojua huwa na mtihani moja kwa shule zote za sekondari nchinzi nzima. Mtihani hii huwa ni kipimo cha marifa na uelewa unaotakiwa mwananfunzi apate ili kukidhi vigezo vya kuendelea na masomo ya advance au chuo kikuu. Ni vyema NACTE ikatoa syllabus kwa vyuo vyote vya kati kwa ajili ya kufundishia courses zao kisha Nacte itunge kna kuratibu mitihani ya cheti na diploma ili anayefaulu mtihani huo wa NACTE aendelee na diploma au degree. Vyuo vingi vya kati vimegeuza elimu hiyo biashara, mtoto anaandikishwa katikati ya muhula maana kinachoangaliwa ni pesa. Hawataki mtoto afeli ili kuvutia wengine waje kusoma kwao. Kinachoangaliwa kwenye usahishaji ni jinsi mwanafunzi alivyomwaga wino na si vitu alivyovijibu. Kuna baadhi ya vyuo hivi ambavyo uongozi wa shule hutoa memo rasmi kwa walimu kutokuwafelisha wanafunzi kwa madai kuwa watahamia vyuo vingine au kufanya wengine wasije kusoma kwao . Maafisa mitihani wa baadhi ya vyuo hivi wametajirika kwasbabu wana uwezo wa kubadili matokeo ya mwanafunzi na hata matokeo ya mwisho na kumfanya mwanafunzi kuwa na GPA isiyo yake. Hapa rushwa ya ngono na pesa hutawala kwa sehemu kubwa. Wakuu wa vyuo hivi hutoa ruksa wanafuzi kuongezewa marks ili kupandisha GPA ili wapate nafasi ya kwenda vyuo vikuu. Haya ninayoyasema nina uhakika nayo. Kama umesoma degree angalia uwezo wa wanafunzi wanaotoka form six na hawa wa equivalent utanielwa. Hawa wanafunzi huwa ni wazito hatari, Wakati fulani nikisoma degree waliwahi kudisco wanafunzi 12 na wote walikuwa kutoka diploma.
Nashauri Mheshiwa ndalichako aamuru NACTE kutunga na kusahihisha mitihani ya certificate na diplama kama NECTA wanavyofanya hii itapunguza uholela kwenye elimu hii ya kati. Waziri ana nia nzuri ya kugeuza elimu yetu kutoka ilipokuwa ikitolewa kiholela bila usimamizi. Meshimiwa waziri nitabaki nawe hata ikibidi kubaki wawili, nakutakia kila la heri na Mungu akubariki.