Nachukia sana hii kitu

KIUNGOMCHEZESHAJI

Senior Member
Joined
Oct 4, 2013
Posts
120
Reaction score
255
Kwanza kabisa mniwie radhi kama post hii hapa sio mahala pake na Mods mnisaidie

Utakuta unaenda ofisi fulani ili uhudumiwe, alafu unakuta mhusika anaanza kujishebedua, mara anakuambia useme shida yako, mara aseme bosi yuko bize, mara njoo baadaye na mengine mengi. Sasa wakati huo kwanza hajakufahamu wewe ni nani na una title gani. Wengine hatupendi kujisema sema, kwa mfano mtu kujieleza kuwa yeye ni mkurugenzi kitengo fulani mahali fulani.

Sasa huyo mhusika anakuja kugundua baadaye sana kuwa wewe ni bosi fulani mahali fulani, anaanza kujinyenyekeza na kujifanya ana adabu kama nini anakuwa kama piriton. Anachomekea maswali ya kijinga jinga tuu..... "ooh, karibu sana, habari za huko, mnatuzidi nini huko, fulani hajambo... ngoja basi nimwambie bosi akuhudumie etc. bla bla bla bla bla kibao. Jamani hii inanikera na kunichefua.

Ni hayo tuu kwa leo
 
^^
Ukikutana na mtu wa aina hiyo ujue anatumia nguvu kutambulika uwepo wake.
^^
 
^^
Ukikutana na mtu wa aina hiyo ujue anatumia nguvu kutambulika uwepo wake.
^^

Kweli kabisa!

ila mara nyingi hawa wapokezi huwa wanaangalia sana na aina ya mtu anayemface kwa wakati huo,
ukiwa smart sana na serious! unapata huduma faster!!
ziada uwe mrefu...
watu warefu tunaogopwa/heshimiwa kila mahali!
 
Mi nasema CUSTOMER CARE, SECRETARY wawekwe WANAWAKE WA MAKAMO!!!!!!!! PERIOD!!!!!!!! Hivi vidada hivi vinchefua vibaya mno!!!!!!!!

Kuna mama pale vodashop mlimani city ni mbuzi mzee kidogo ila ni BEST CUSTOMER CARE!!!!!!!!!! Ningeweza ningempandisha cheo!!!!!!!! Ana ethics za kazi! VOD FASTER NIMAJANGAAAAAAAAAAAAAA!!!!!!!!!!!
 
Kuna office zingine wanaringia wateja wao sana
 
Pole sana ndugu Mkurugenzi....
 
Kweli kabisa!

ila mara nyingi hawa wapokezi huwa wanaangalia sana na aina ya mtu anayemface kwa wakati huo,
ukiwa smart sana na serious! unapata huduma faster!!
ziada uwe mrefu...
watu warefu tunaogopwa/heshimiwa kila mahali!

Na sis wafupi tuna shida sana tukionwa tu wanadhani tumepeleka barua za field....
 
Sasa ukishampandisha cheo si tutakosa customer care jamani?

Mimi ni receptionist, mrembo wa haja (usiulize nimejuaje, Paw tells me that even when he is drunk) na sina shobo. Nahudumia wateja wote hata wanaoleta barua za ems kwa heshima na taadhima.
 
Last edited by a moderator:
Hahaha usitembee na bahasha basi. Ukibeba mkoba wa haja mbona tunakuangalia kwa jicho la pembe?
Na sis wafupi tuna shida sana tukionwa tu wanadhani tumepeleka barua za field....
 
kaka kiukweli wanakera sana, tena akiwa amesukia manywele ya bandia ya kaangukia usoni akaweza kurudisha kama wazungu utajuta..kutokujali na kuipenda kazi yake ndo maana wanakuwa wanashindwa kuheshimu hata wageni. si sawa... kama mapokezi huwez uliomba kazi ya nini.?.....
 
Kweli kabisa!

ila mara nyingi hawa wapokezi huwa wanaangalia sana na aina ya mtu anayemface kwa wakati huo,
ukiwa smart sana na serious! unapata huduma faster!!
ziada uwe mrefu...
watu warefu tunaogopwa/heshimiwa kila mahali!

Hongera mr. Tall
 
Yani ma customer care ,ma secretary kibongobongo ni noma aisee!!

Unaweza meza mtu! Esp ukiwa nawe binti binti mbichi af mrembo!!!

Onetime nlienda vodacom customer care nliongozana na kaka yangu akajua mpenzi wangu acha aninunie! Kuja kuona tunataniana na bosi wake na tunaelekea lunch.. Akaanza kujishebedua oh aunt karibu tena..oh viatu vyako umenunua wapi natafuta sijuw fyoko gani!! Hahahah unamkata jicho adi umeme unakatika! Na msonyo juu

Watu wanashindwa kuelewa JUST BE NICE TO EVERYBODY..UL ALWAYS BE HAPPY AND BLESSED!
mygranma aliniambia na naamini! Jus be nice Mungu atakubariki! Hakuna formula ya kubarikiwa zaidi ya kutenda mema na yafaayo kwa wenzio.
Me binafsi sipendagi watu wasiojielewa..dharau za kis*n af huna a wala be.. !
 

msamehe bure jamanii upeo nao finyu
 
Iliwahi kunikuta; sitatoa details; nilikuwa safari mkoani...niliapa kuwa sasa nataka kufanya mabadiliko...nilitaka kulala na huyu binti mbele lakini baada ya muda na u busy hasira ziliniishia...

Tatizo letu tuna uwezo wa kuwachukulia hatua watu kama hao lakini hatufanyi hivyo...

I wish ningeandika yote ila niliwasimulia wshikaji hivyo ma ID itaweza julikana (na sipendi)

Mtu hakujuhi humjuhi kisa ni mwanamke tena mdogo mdogo analeta dharau utadhani umeenda ofisini kwake kuomba kazi. Na hakuwa secretary, ni msomi mzima; ila sijuhi alinichuliaje yaani...

Nina mpango wa kuanza kuwa mkorofi rasmi...ngoja nimalize shughuli zangu.

Nitakuwa nalima barua kwa kila anayeniletea dharau (sio mwajiri wao) ila kama customer na wao ni watoa huduma (hata kama mkurugenzi ni muhudumu tu ...civil servant) lazima wanipe heshima stahiki...
 
huku ughaibuni kwetu hakunaga hayo.mteja mfalme ukizingua mteja unakuta barua mezani inakusubiri
 
Kweli kabisa!

ila mara nyingi hawa wapokezi huwa wanaangalia sana na aina ya mtu anayemface kwa wakati huo,
ukiwa smart sana na serious! unapata huduma faster!!
ziada uwe mrefu...
watu warefu tunaogopwa/heshimiwa kila mahali!

na sie wafupi tunadharaulika lol inabidi tuende na sura za kazi
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…